Mzee Kikwete: CCM ya sasa ukimtambulisha kiongozi wa Upinzani anaonekana Adui, nilimpigia kampeni Dr Ndugulile WHO, Ummy naye alifanya Kazi Kubwa!

Mzee Kikwete: CCM ya sasa ukimtambulisha kiongozi wa Upinzani anaonekana Adui, nilimpigia kampeni Dr Ndugulile WHO, Ummy naye alifanya Kazi Kubwa!

Akiwa msibani kwa Faustine Ndugulile Rais mstaafu Dr Kikwete amesema kwa CCM ya sasa kumtambulisha kiongozi wa Upinzani hadharani unaonekana Adui yaani Kirusi.

Kikwete amesema hayo wakati akimtambulisha mbunge wa Viti Maalum Halima Mdee (Chadema)

Aidha Kikwete amesema baba yake Faustine yaani hayati Mzee Ndugulile alikuwa ni Rafiki yake na wamefanya Kazi pamoja Wizara ya Mambo ya nje.

Kikwete amesema alishiriki kumfanyia kampeni za WHO marehemu Faustine kwa kuongea na Viongozi mbalimbali wa Africa nao walikubali kutuunga mkono hata Senegal alipiga Simu kwa Waziri Mkuu naye akakubali Moja kwa Moja kuunga mkono Tanzania.

Pia Ummy Mwalimu alifanya Kazi Kubwa sana kuhakikisha Faustine anashinda.

Nawatakieni Dominica NJEMA 🌹
Hivyo siowote ni wabaya ila virusi vilivyo miongoni mwao?
 
Asante sana mzee Kikwete kwa kuliona hili. Bila shaka umejionea mwenyewe kuwa mambo yameharibika, yamekuwa mabaya sana. Sasa kama ulivyofanya Ndugulile akapata, fanya na huyu aondoke mwakani.
 
Chadema mmesahau mara hii mlivyokuwa mnatuzomea na kuturushia makopo tulivyokatiza mtaani na sare zetu za kijani? Ilifikia hatua tukashindwa kuvaa sare zetu, those days kwenu ilkuwa sherehe sasa ime-backfire mmeanza mayowe!!
Kama bwana mdogo unakumbuka vyema, CCM walikua hawawezi kuvaa sare za chama Chao sio kutokana na kuchukiwa na CHADEMA. Nasema hivi nikikumbusha kwamba Mimi sio mwanachama wa CHADEMA na sijawahi kuwa.
Sababu kubwa ilikua ni kushiriki, kulea na kuishi maisha ya kifisadi kama Ndio order of the day..
Transparency and good governance aliyoishamirisha JK iliweka bayana uzembe na uchafu wa uongozi wa CCM. Kulikua na mijdala huru kuanzia kwenye media, mtaani na kwenye majukwaa ya kisiasa ambayo iliwaweka uchi kiasi kwamba mliona aibu! Kilichokosekana kwa kiasi kikubwa ni accountability and rule of law Kwa kiwango kikubwa.
Watu wa CCM wamekuwa na ujasiri wa kuvaa sare hadharani bada ya Magufuli kuleta aina mpya ya utawala ambao ni undefined na akaamua kufanya "impunity". Kwamba yeyote anayekosoa Ccm alionekana ni adui wa taifa, hivyo mbeleko ya Dola ikiwemo kuwazuilia na kutishia maisha ya walosoaji ikatoa ujasiri huo. Ikiwa una ushahidi wankurushiwa makopo Kwa sababu tu ya kusimamia maslahi ya wananchi, utawala Bora, Haki, uwajibikaji na utawala wa Sheria basi uwasilishe hapa na nipo tayari kukosolewa.

Sasa kinachofanyika sasa hivi hata kama tutakubaliana na wewe kwamba hiyo Ndio sababu., hakuna ukweli wowote wa wanachama wa CDM kuunsa magenge ya askari wasiovalia sare na wasiofuata utaratibu kuwakamata wakosoaji wake. Na hivyo kuwapa Haki ya kufanya hivyo sasa hivyo.
Hakuna ushahidi wa CHADEMA kuandaa uchaguzi na kutumia Dola kupora na kuuwa wananchi hadharani mbele ya wake na watoto wao hivyo wanastahili hivyo hivi sasa.

Nawasilisha
 
Akiwa msibani kwa Faustine Ndugulile Rais mstaafu Dr Kikwete amesema kwa CCM ya sasa kumtambulisha kiongozi wa Upinzani hadharani unaonekana Adui yaani Kirusi.

Kikwete amesema hayo wakati akimtambulisha mbunge wa Viti Maalum Halima Mdee (Chadema)

Aidha Kikwete amesema baba yake Faustine yaani hayati Mzee Ndugulile alikuwa ni Rafiki yake na wamefanya Kazi pamoja Wizara ya Mambo ya nje.

Kikwete amesema alishiriki kumfanyia kampeni za WHO marehemu Faustine kwa kuongea na Viongozi mbalimbali wa Africa nao walikubali kutuunga mkono hata Senegal alipiga Simu kwa Waziri Mkuu naye akakubali Moja kwa Moja kuunga mkono Tanzania.

Pia Ummy Mwalimu alifanya Kazi Kubwa sana kuhakikisha Faustine anashinda.

Nawatakieni Dominica NJEMA 🌹
Yuko sahihi,tumefikishwa hapa na awamu ya 5 na hali hii inaendelezwa na awamu ya 6.

Watawala wameonja Raha ya udikteta.
 
Akiwa msibani kwa Faustine Ndugulile Rais mstaafu Dr Kikwete amesema kwa CCM ya sasa kumtambulisha kiongozi wa Upinzani hadharani unaonekana Adui yaani Kirusi.

Kikwete amesema hayo wakati akimtambulisha mbunge wa Viti Maalum Halima Mdee (Chadema)

Aidha Kikwete amesema baba yake Faustine yaani hayati Mzee Ndugulile alikuwa ni Rafiki yake na wamefanya Kazi pamoja Wizara ya Mambo ya nje.

Kikwete amesema alishiriki kumfanyia kampeni za WHO marehemu Faustine kwa kuongea na Viongozi mbalimbali wa Africa nao walikubali kutuunga mkono hata Senegal alipiga Simu kwa Waziri Mkuu naye akakubali Moja kwa Moja kuunga mkono Tanzania.

Pia Ummy Mwalimu alifanya Kazi Kubwa sana kuhakikisha Faustine anashinda.

Nawatakieni Dominica NJEMA 🌹
Wasiwasi upo kwa Team Msoga
 
Magufuli aliua nguvu ya wazee kwenye maamuzi ya chama. Nguvu ya wazee iliasisiwa na Nyerere. Kwankulitambua Hilo Magufuli akaamua kuwapunguza nguvu na kuwato katika sehemu ya maamuzi magumu ya chama. Akàanzisha kilichoitwa Baraza la ushauri ambalo halina meno. Kama mnavyojua ushauri ni ama ukubaliwe au ukataliwe. Baada ya kuwanyima nguvu akaanza kuwang'ong'a hadharani wazi wazi akijua hakuna WA kumfanya chilochote. Akaingiza kundi la wajinga na watumia nguvu kwenye chama kuliko hoja huku wakiimarisha ndoa Yao na vyombo vya Dola sambamba na mabadiliko lukuki ya Sheria za usalama na ulinzi!
Uadui miongoni mwa watanzania kwa misingi ya chama iliasisiwa na huyo na Wala hakiwezekani kupingwa. Kikwete alipeleka maendeleo kwa maeneo yalichagua upinzani kama njia ya wlkwashawishi wananchi wakuunge mkono na chama chake. Magufuli aliweka bayana kwamba hawezi na hatopeleka maendeleo Kwa watu wenye itikadi tofauti na chama chake. Alienda mbali kuwafananisha na magunzi na kutaka hadharani. Hii ilichochea na kurasimisha ukatili na uadui dhidi ya upinzani.
Na huu ndio ukweli,unategemea nini mpaka hapo? Kwamba Samia hataki Madaraka?

JK ni sehemu ya hapa tulipo Kwa sababu alizotaka yeye so asilaumu watu.
 
Huu ujumbe upo coded sana.

Yajayo YANAFURAHISHA
Wapinzani hamuwezi kujikausha mkitegemea mbeleko ya JK.

Wanaonufaika na uwepo wa SSH unadhani ni wajinga tuu kwamba watakubali kirahisi? Jidanganye na ndio wameshika mpini.

Siku za karibuni JK anajilalamisha sana 😆😆
 
Kabisa, hivi Mbeya kwa Sugu Chadema hata mtaa mmoja hawajapata na Magufuli ni marehemu!
Chadomo ya mitandaoni ndio wapigakura wa Mbeya?

Kama wamedhulumiwa mbona hawalalamiki? Hujawona Chauma wakifurahia maisha?

Mwisho siasa za kijinga za zamani hazipo tena Mbeya watu wanaangalia siasa Zenye Tija.
 
Kikwete hakuwa makini kama mwenyekiti wa ccm, ndio akampa nafasi bwm akatuletea jiwe akaharibu demokrasia ya nchi hii na upuuzi wa jiwe ndio umekuwa kanuni kuharibu uchaguzi Kila mwaka! Jiwe alikuwa Mpuuzi sana!
Jaman mm jiwe sikumpenda kwa vijimambo vyake bt kwa sasa inatosha tumpumzishe kwa shutma za kweli na za kutunga
 
Ndio nilichosema, kwani napi ana nini cha maana hadi kuwa katika top levels za maamuzi ya nchi zaidi ya kuwa baba yake yupo kwenye network? Watu wanatambulishana baba yake nilifanya naye kazi, nilisoma naye, nilikuwa naye JKT, au JWTZ tukiwa maafisa wadogo, ninasali naye, alinipokea wkt naanza kazi, alinipa nyumba ya kupanga bure, alikuwa ananipa lift wakati naanza maisho so nampambania mwanae. Kumbuka huyuhuyu Jk alisema Manji alikabidhiwa na baba yake na anapokuja US anafikia kwa baba yake, so ujue ukwasi wa manji ulioteketezwa na jiwe pia ulitokana na network then yeye na makamba wakasema baba yake napi alimkabidhi yeye na makambaz. So tungekuwa its ethnic network inafanya kazi kula mafao ya nchi. Wewe na maarifa yako kaanzishe shamba au genge la mbogamboga kule, wafanya maamuzi ni wenye surname za mongela, kikwete, mkapa, msuya, natepe, marwa, mboma, pinda, msekwa nk, pia maofisini kote uliza wakurugenzi na wakubwa wote ni nani ndo utajua
Imefikia muda hata bora tusingesoma bora tungekua waasi tu watu tunaumia hatutoboi hapo
 
Nami nilikuwa nashangaa sana.
CV ya Ndugulile ni ya kawaida sana, bila godfather asingeweza kufika hatua hiyo kamwe
Halafunsio Dr per say kuna waendesha boda hapa kibada wanamzidi ila ndo hvo mafuriko yalimpandisha kobe juu ya muembe
 
Akiwa msibani kwa Faustine Ndugulile Rais mstaafu Dr Kikwete amesema kwa CCM ya sasa kumtambulisha kiongozi wa Upinzani hadharani unaonekana Adui yaani Kirusi.

Kikwete amesema hayo wakati akimtambulisha mbunge wa Viti Maalum Halima Mdee (Chadema)

Aidha Kikwete amesema baba yake Faustine yaani hayati Mzee Ndugulile alikuwa ni Rafiki yake na wamefanya Kazi pamoja Wizara ya Mambo ya nje.

Kikwete amesema alishiriki kumfanyia kampeni za WHO marehemu Faustine kwa kuongea na Viongozi mbalimbali wa Africa nao walikubali kutuunga mkono hata Senegal alipiga Simu kwa Waziri Mkuu naye akakubali Moja kwa Moja kuunga mkono Tanzania.

Pia Ummy Mwalimu alifanya Kazi Kubwa sana kuhakikisha Faustine anashinda.

Nawatakieni Dominica NJEMA 🌹
Kwanini uadui wa kisiasa uanaongezeka nchini?
 
Back
Top Bottom