REA, Shule za Sekondari, Barabara za Lami nk ni baadhi ya miradi uliyoiasisi au kuiendeleza ulipokuwa Raisi wetu. Mungu akubariki kwa kuwa mkweli.
Tulifika mahala tukaaminishwa kwa nguvu za ajabu kuwa awamu zilizopita hazikufanya kitu!
Nilimsikia mgombea mmoja akisema kuanzia wakoloni hadi maraisi wa awamu zilizopita nao walijenga barabara, miradi kadhaa nk. Kuwa, kazi ya serikali inayokusanya kodi ni kuleta maendeleo ya vitu na watu.
Hivyo, kwa kijana anayekuwa, ni vyema ajue tulikotoka tuliko na tunakoenda kwa usahihi bila kujisifu.
Nimefurahi pia kusikia kuwa wewe ndo ulitoa wazo la elimu bure kwa shule za msingi na sekondari na kuweka kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Chetu. Lakini ukisikiliza miziki ya Diamond na wasanii wengine utafikiri kila kitu kimebuniwa na kuwekwa kilipo na awamu ya tano.
Hongera sana Mh. Dr. Kikwete kwa kuweka wazi mambo haya japo hukugusia Mradi Umeme wa Gesi ya Mtwara kuwa uliishia wapi.
Naamini iko siku utaweka wazi tujue kwani tulishaamini tungepata umeme wa nafuu kuliko ilivyo sasa.