Uchaguzi 2020 Mzee Kikwete: Ninakopanga sijafukuzwa

Uchaguzi 2020 Mzee Kikwete: Ninakopanga sijafukuzwa

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Huyu Jakaya kikwete Rais mtaafu amenishangaza sana jana kwa kauli yake ya kuishi nyumba ya kupanga na bado ana mkataba na mwenye nyumba.

Kichangia neno katika kupokea nyumba za vingozi mzee Kikwete bila aibu ametoa kauli ya kuzua chuki na taharauki kubwa sana kwa mtu kama mimi mwenye kumfahamu Kikwete kwa upana.

Kikwete amekuwa Naibu Waziri kwa miaka mingi, Waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka 10 na Rais miaka 10, leo analalamika kupanga.

Amelipwa zaidi ya million 12×10 kama Waziri wa Mambo ya Nje achiliambali vyeo vyake huko nyuma.

Amelipwa million 36×10 kama Rais na marupurupu kibao. Pamoja na kiinua mgongo cha karibu nusu Billion, bado Kikwete analipwa mafao ya kutia simanzi kwa mtu wa kawaida.

Amejengewa nyumba (Ikulu ndogo) msonga na Suma JKT akiwa hata hajastaafu. Ukiingia Msoga utashangaa sana ukubwa wa Ikulu ile na miundombinu yake ya nchi zilizoendelea.

Amejengewa nyumba Bagamoyo kwa mamake na Suma JKT. Ni nyumba ya kufuru.

Ana nyumba karibu kila mkoa na mitaa kibao hapa Dar, achilia mbali alizojenga nje South Africa na Dubai.

Kwa kauli aliyoitoa jana, inatia simanzi na unafiki mkubwa sana kuwa amepanga. Je, mzee Kikwete anataka kumdanganya nani kuwa anaishi maisha ya shida na amepanga so wamjengee taratibu tena kwa uimara mkubwa?

Kama ulimsikiliza na kumwangalia Kikwete usoni, alionesha kutofurahishwa na ujenzi na kuona kama hakuridhika na ile nyumba ambayo kwa mtu wa kawaida hata tajiri ungeiona kuwa ya mapesa mengi.

USSR
 
Bora uyo tunayejua amekula wanananchi walikula wakiwemo wafanyakazi hewa walilipwa, nao vyeti feki walikuwemo ajira zimo pamoja na kundi lote ilo mishahara kila mwaka inaongezeka na barabara zimendelea . sasa huyu sijui pesa anapeleka wapi wakati izo flyover ni isani mengine yote ameyakuta tena yy ndo akayaharibu standard yake
 
Heri wenye nazo wanagawana huku kwangu kukavu tia mchuzi sijui kajamba nani.. gurudumu bado ni kubwa kweli na hata kulizungusha ni shida!

Sikuona haja ya wao kujengewa nyumba kwani wamekosa nini? Tayari wanauhakika wa mfereji wa pesa,chakula,ulinzi,mavazi n.k
Wanatumia mipesa kunufaishana walio nufaika huku kuna wanafunzi wanakosa mikopo!,Kuna watu hawajalipwa mafao!..

Hii na ikawe taswira kwa wengine na watambue kuwa unatakiwa ujipiganie utoke kwenye Lindi la umaskini hawa viongozi wapo kwaajili yao hizo nyengine mbwembwe.
 
Nawewe gombea urais ili tukujengee, waache wazee wa watu wale matunda yao. Wewe unadhani kuongoza nchi ni jambo jepesi, kama tu umonitor unawashinda baadhi ya watu usilete mchezo na uongozi.
Nchi hata ikipata natural disesters mwisho wasiku jicho na masikio kwa Rais atasemaje hakika ni kazi ngumu usiku hulali ni kupitia pitia vitu kidogo uwe na ufaham wake kiundani ni kazi
 
Huyu Jakaya kikwete Rais mtaafu amenishangaza sana jana kwa kauli yake ya kuishi nyumba ya kupanga na bado ana mkataba na mwenye nyumba...
Mimi nilimwelewa kuwa amepanga kwa maana ya kuwa anaishi na kutumia nyumba ya familia kama ofisi wakati sheria za nchi zinataka apewe nyumba ya vyumba vinne na ofisi inayojitosheleza na serikali
 
Kwa kauli aliyoitoa jana, inatia simanzi na unafiki mkubwa sana kuwa amepanga. Je, mzee Kikwete anataka kumdanganya nani kuwa anaishi maisha ya shida na amepanga so wamjengee taratibu tena kwa uimara mkubwa?
Lile lilikua dongo kwenda kwa gari la mkaa, wakwere hujawajua vizuri wewe.

Hivi kwa akili zako kabisa JK awe amepanga? Labda Kama kajipangisha nyumba yake mwenyewe.
 
Huyu Jakaya kikwete rais mtaafu amenishangaza sana jana kwa kauli yake ya kuishi nyumba ya kupanga na bado ana mkataba na mwenye nyumba...
Kama wewe unajua kiswahili haswaa rejea alichoambiwa juu ya kuwashwawashwa! Mtu mzima kuwashwawashwa inamaana gani, ninaamini hilo halijamtoka moyoni kwani hakuwahi kuombwa radhi.

Je, niseme na wewe unawashwawashwa? Huu ni wakati wa uchaguzi aliyeko madarakani alipoupata alisahau kuwa saa daima haisimami, alitoa maneno mengi sana mabovumabovu na leo anajaribu kuwapoza! Ampoze mzee Mwinyi kwani yeye nyumbani mwake anawagombea watatu.

Unanipa nyumba leo! Mimi bado sijafukuzwa nyumba niliyopanga.
 
Huyu Jakaya kikwete Rais mtaafu amenishangaza sana jana kwa kauli yake ya kuishi nyumba ya kupanga na bado ana mkataba na mwenye nyumba.

Kichangia neno katika kupokea nyumba za vingozi mzee Kikwete bila aibu ametoa kauli ya kuzua chuki na taharauki kubwa sana kwa mtu kama mimi mwenye kumfahamu Kikwete kwa upana...
Uelewa wako mdogo sana, aliongea kwa mfano kama angekua amepanga na yuko ktk presha yakuhama..ile speed ya ujenzi sio sawa!JK awe amepanga?
 
Back
Top Bottom