Mzee Kikwete: SGR iliasisiwa na Hayati Mkapa na Mimi wakati namkabidhi Madaraka hayati Magufuli nilimsihi aanze Utekelezaji wa mradi!

Ni kweli. He did not start anything out of nowhere. He just implemented projects which were in the shelves for a long time. Labda lile daraja la Busisi tu ndio maamuzi yake
Miradi mikubwa sio maamuzi ya mtu mmoja ila kuitekeleza inataka mtu smart inaweza kuwa kuna hela ya kutosha ila aliepo ndo bongozozo ninachoamini miradi mikuwa aliyoanzisha magufuli asingezanisha kutekeleza bhasi hadi leo ingekuwa ipo kwenye makaratasi tuu maana mingine imeshaanza kufa.
 
Lakini Arifu maendeleo hayatakuja kwa kupiga story na kushinda kuombaomba misaada huko ughaibuni. JPM ameweka alama ya uthubutu ambayo ni nadra sana kwa sisi tulio wengi.

Ila kuongea tu..hamna mfano. Na vile mdomo hauna kulipa kodi, basi twasema tu. Actions differentiate individuals who succeed and those who just add another numbers in the crowded group of failures
 
Sio mawazo mazuri mkuu, manake unaweza ukafa wewe kabla yake .
Hata kama kufa ni lazima tujitahidi kuepuka kutabiriana vifo tumuachie Mungu mambo ya vifo
Shetani mponde mawe adui mwombee kifo...huyo mzee ni adui namba moja wa taifa hili
 
Tusimuombee kufa, sio jambo jema hata kidogo kuombea kifo kwa mwenzako hata kama alikujlkosea kitu gani.
hii roho ya huruma/kijamaa uliyonayo ndio inafanya nchi iwe masikini.
Maana mafisi yanaendelea kuwanyonya nyie wanyonge huku yakihubiri muwe na utii/mshikamano/huruma na mlinde amani.
 
Kama Mkapa ndiye aliyeasisi kitu gani kilimshinda kutekeleza wakati kila mipango na rasilimali zilikuwa mezani?

Mipango yote migumu iliyowashinda marais wote kuanzia awamu ya kwanza hadi ya nne JPM ndiye kiongozi pekee aliyevaa ujasiri ya kuitekeleza kwa maumivu makubwa bila kuwadharau wananchi wakati kwa sifa zote ziende kwa JPM na Mkapa kama mbunifu wa mradi yeye agalauke na iradi ya kifisadi tu basi.
 
Hii ni kweli.
Ukikaa na wazee kama Rugunyamheto,Rutabanzibwa,Kamba, na Prof A. Mbele watakwambia kuhusu mipango aliyokuwa nayo B. Mkapa.
Ben ni baba wa mabadiliko.
Ile SAP angekuwa legelege,nchi isingekuwa hapa ilipo.
Mheshimiwa... Hao wote uliowataja hapo ni wasomi na wanazuoni (Maprofesa) wakubwa eeh?

Je! Walikuwa washauri wake kipindi yuko madarakani au ni marafiki zake wa miaka mingi tangu mungu hajamfungulia dunia?
 
Ahsante kwa kutuelimisha, sisi ambao hatukuwa kulifahamu hili ndugu JokaKuu 👍🙏
 
Ni hatua kubwa sana! Haikuwa rahisi, ila alifunga macho na akaziba masikio kuhakikisha hili linakamilika! Kweli mheshimiwa Rais ni Mwanamke wa shoka..., anastahili pongezi na apewe heshima yake.

Mapungufu, sote kama binadamu tunayo.
 
..sasa mbona mawaziri wake waliomsaidia ktk wizara ya fedha, kwa maana, Daniel Yona, na Basil Mramba, wakaishia kwenye kushtakiwa kwa ufisadi?
Nafkiri huenda palikuwa na maswala mengineyo nyuma tusiyoyajua (waswahili wanasema chini ya kapeti)
 
Haya mambo ya kesi za ufisadi wa mawaziri, tena wa fedha achana nayo.
Unakumbuka kesi ya Prof C. Mahalu!!!!???
Ndugu JokaKuu unakumbuka I. Msabaha na "bangusilo"!!??
Unaweza ukatupa visa vyao hapa tafadhali, wengine tulikuwa vijana wadogo bado mzee wangu
 
Walidhani wazo lilitoka kwa Mwendazake kumbe tangia "Nzee Nkapa".

Sema Jiwe alithubutu kuianza SGR na Stegolaz(JNHPP). watangulizi wenzake walishindwa.
Mbona tunakuwa washmab sana..Haya mawazo yote hata bwawa la Nyerer yamekuwepo mda mrefu,,sualal akili kupata pesa yakutekeleza ndo muhimu.Lakini kusema tujenge relief ya SGR harafu huna Hera na mwingine akaja akatumia akili kupata glfedha nakutekeleza mradi ninani Bora???
 

Great minds discuss ideas.

So idea ndiyo muhimu ,kongole kwa waliotoa ideas.
 
Haha wazo la mkapa halafu yeye akaangalia Tu miaka 10 akamaliza bila kufanya chochote [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mzee anazeeka vibaya sana

..hoja yake ni kwamba Jpm ameweza kujenga Sgr kwasababu watangulizi wake walipunguza kwa kiwango kikubwa hitaji la ujenzi wa barabara.

..mfano mwingine ni ujenzi wa barabara za mikoa na wilaya. Ujenzi huo uliwezekana kwasababu awamu zilizotangulia tulijenga barabara kuu.

..au kuanzishwa kwa Tarura. Bila kuwa Tanroads imeanzishwa na imetekeleza majukumu yake kwa ufanisi, tusingeweza kufikiria kuanzisha Tarura.

..kinachoongelewa hapa ni CONTINUITY. Yaani muendelezo toka awamu moja ya uongozi kwenda awamu nyingine
 

..Tz kipindi fulani ilikuwa haina fedha, na haikopesheki, kuweza kuanzisha mradi mkubwa kama Stieglers.

..Lakini msisahau miradi ya umeme ya Mtera, Kidatu, Kihansi, iliyojengwa na watangulizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…