..kuna mambo Mkapa aliharibu mfano masuala ya mrahaba. Na kosa lake lilikuwa kusaini mikataba mingi ya uchimbaji dhahabu. Mkapa alitakiwa kusaini mikataba michache ili serikali ipate nafasi ya kujifunza.
..Doa lingine ktk serikali ya Mkapa lilikuwa ni mauaji ya waandamanaji waliokuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar.
..Mkapa pia anastahili lawama kutokana na ubovu wa mfumo wetu wa demokrasia. Yeye ndiye Raisi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi, hivyo alipaswa kuendeleza marekebisho kutokea pale alipompokea Mzee Mwinyi.
..Kwa upande wa UCHUMI, Kikwete na Magufuli, na Samia, ni wafaidika wa misingi mizuri aliyoiweka Mkapa.
..Serikali ya awamu ya 3 ndiyo iliyowezesha tukasamehewa mikopo, hivyo badala ya kulipa mikopo, tunaweza kupeleka fedha kwenye miradi ya maendeleo. Pia kusamehewa mikopo ya awali kuliwezesha serikali ya Tanzania kuwa ktk nafasi ya kupata mikopo mipya hii tuliyoishudia wakati wa Kikwete, Magufuli, na sasa Samia.