Mzee Kikwete: SGR iliasisiwa na Hayati Mkapa na Mimi wakati namkabidhi Madaraka hayati Magufuli nilimsihi aanze Utekelezaji wa mradi!

Mzee Kikwete: SGR iliasisiwa na Hayati Mkapa na Mimi wakati namkabidhi Madaraka hayati Magufuli nilimsihi aanze Utekelezaji wa mradi!

Rais wa awamu ya 4 mzee Kikwete Leo amesafiri kwa TREN ya SGR kutoka Dar es salaam hadi Morogoro na kusema safari yao wametumia muda wa saa 1 na dakika 49 tu

Mzee Kikwete amesema mradi wa SGR iliasisiwa na hayati Mkapa na ilipofika awamu ya Shujaa Magufuli ndio alianza Kuutekeleza lakini kwa bahati mbaya hakushuhudia matunda ya Juhudi zake

Mzee Kikwete amemshukuru Sana Mpendwa Wetu Mh Rais Samia kwa kuendelea kuukamilisha mradi huu ambapo Kesho Treni ya SGR itatoka DAR ES SALAAM hadi Dodoma ambayo ni mafanikio ya kihistoria

Source: ITV Habari
Sasa mbona Jk hajanialika ili tupande wote ?
 
Nakubali. Ni kweli.kabisa Kuna miradi mingi sana iliasisiwa na Mkapa, Kikwete pia. Tena hii miradi inayokwenda na wakati mingi ni ya Kikwete...framework ziliwekwa na hayati Ally Mwinyi...
Ni vile tu wakati huo haukuwa kama siku hizi, Rais alikuwa akifanya kitu hasemi sana .

Na pia Kuna watu inawauma sana Samia kufanikiwa kumaliza miradi. Walijua hataweza, Alhamdulilah ameweza
SSH kumaliza miradi nani anachukia na je pesa anatoa mfukoni mwake , sie kama watz ndo tumemaliza miradi kupitia kodi na tozo naomba kumbukumbu iwekwe sawa
 
Back
Top Bottom