Mzee Kikwete: SGR iliasisiwa na Hayati Mkapa na Mimi wakati namkabidhi Madaraka hayati Magufuli nilimsihi aanze Utekelezaji wa mradi!

Mzee Kikwete: SGR iliasisiwa na Hayati Mkapa na Mimi wakati namkabidhi Madaraka hayati Magufuli nilimsihi aanze Utekelezaji wa mradi!

Sgr inapaswa kufika Mwanza na Kigoma ili kuleta faida kwa nchi, kuishia Dom haina faida wala maana yoyote.

Halafu lengo mama la SGR ni kubeba mizigo ya nchi jirani na kuvuna pesa zao kuijenga tz kiuchumi na kuwapunguzia raia mzigo wa tozo na kodi ili tusihamie Burundi, lengo mama sio kubeba abiria kina Mr Tabasamu, kubeba Abiria hiyo ni bonus tu na ni ujuha na ushamba kushangilia vitu vidogo maana tukibweteka reli ikaishia njiani kilio na kusaga meno viko mbele kama wenzetu wa Kenya!!

SGR Ikiishia Dodoma au Mwanza tu bila kufika Kigoma yanayoendelea Kenya yatafika huku maana Reli yao ya SGR iliishia njiani Naivasha kutokana na ufisadi wa kutisha na sasa mkopo waliokopa kuijenga unadaiwa na China huku wananchi wakitakiwa kuulipa kwa kukamuliwa tozo na kodi kubwa wakati SGR haileti faida iliyotarajiwa na si wao walioiba pesa za mradi.

Huu si wakati wa kupongezana na kusifia yaani ngoma bado mbichi sana, hadi siku ile SGR imefika Mwanza na Kigoma na kubeba mizigo ya nchi jirani, hapo ndo sasa Bimkubwa apewe maua kedekede, mgolole, mkuki, ngao, shuka, nyimbo na mapambio.
Nilimsikia kadogosa juzi kalizungumzia hilo kwa msisiyizo mkubwa sana,kwamba malengo na faida ya SGR ni mizigo sasa sijui alikuwa anawapa ujumbe mamlaka na sijui kama watanzania walimuelewa pale msukuma wa watu.
Na ndio maana ukute wanatumia nguvu kubwa sana kuzuia mizigo mule ili mamlaka ichangamkie huo upande wa mizigo lakini ndio kama ilivyo kawaida ya viongozi wetu wanaenda na upepo.

Pengine tumsaidie kadogosa humu kupiga kelele kwa kuanza huduma za kusafirisha mizigo.
 
Sio kwa ubaya ila huyu mzee anazeeka vibaya asee! Nadhani anaanza poteza kumbukumbu. Ajue tu huku ni anajiaibisha
 
Rais wa awamu ya 4 mzee Kikwete Leo amesafiri kwa TREN ya SGR kutoka Dar es salaam hadi Morogoro na kusema safari yao wametumia muda wa saa 1 na dakika 49 tu

Mzee Kikwete amesema mradi wa SGR iliasisiwa na hayati Mkapa na ilipofika awamu ya Shujaa Magufuli ndio alianza Kuutekeleza lakini kwa bahati mbaya hakushuhudia matunda ya Juhudi zake

Mzee Kikwete amemshukuru Sana Mpendwa Wetu Mh Rais Samia kwa kuendelea kuukamilisha mradi huu ambapo Kesho Treni ya SGR itatoka DAR ES SALAAM hadi Dodoma ambayo ni mafanikio ya kihistoria

Source: ITV Habari
Na bwana la Nyerere alitenga yeye fedha, kuhamia Dodoma yeye alilipia ramani, na daraja la Tanzanite aliacha mchoro, na lile la Busisi alimwambia JPM aanze ujenzi mara moja...
 
Mweee
1719491919799.jpg
 
Rais wa awamu ya 4 mzee Kikwete Leo amesafiri kwa TREN ya SGR kutoka Dar es salaam hadi Morogoro na kusema safari yao wametumia muda wa saa 1 na dakika 49 tu

Mzee Kikwete amesema mradi wa SGR iliasisiwa na hayati Mkapa na ilipofika awamu ya Shujaa Magufuli ndio alianza Kuutekeleza lakini kwa bahati mbaya hakushuhudia matunda ya Juhudi zake

Mzee Kikwete amemshukuru Sana Mpendwa Wetu Mh Rais Samia kwa kuendelea kuukamilisha mradi huu ambapo Kesho Treni ya SGR itatoka DAR ES SALAAM hadi Dodoma ambayo ni mafanikio ya kihistoria

Source: ITV Habari

Ni kweli kwa JK alishaingia kwenye makubaloano ya awali na Wachina wajenge yeye Magufuli akafuta. Kwa hili amesema kweli Bw. Jk
 
Back
Top Bottom