Mzee Kilomoni Tupo nyuma yako usiyumbishwe

Mzee Kilomoni Tupo nyuma yako usiyumbishwe

Uzi wa vyura mimi Simba nikae kutafuta nini. Nasepa
Na huyu mzee kilomoni nae chura sio?
IMG-20190607-WA0000.jpg
 
Mmepata ubwete wa kuingia Champion league kupitia viti maalum kwa mgongo wa Simba chini ya hela ya Mo na visionary strategies zake.. Sasa mnataka penyeza zile fitina zenu za Timu wanachama (wananchi)wakati hata kutoa bukubuku tu kwenu iliwashinda kwenye lile kapu lenu la kuombaomba... Piganeni na hali yenu nanyi msimame na miguu miwili kiuchumi na muache ufitini, chuki na uzandiki.
Mtegemea cha ndugu hufa masikini
 
Huwa nikipita mitandaoni nasikitika sana kwa mashabiki wa Simba kumbull mlezi mkuu wa simba, kumtukana matusi ya kila aina eti kisa wanamuwekezaji Mo

Sisi tulioapa kuwa simba haiwezi kubadilishwa kuwa timu ya mtu tutasimama na mzee wetu hata wale wapiga kelele wanaotumwa na mo kumtukana mzee wetu wataparaganyika na kutuachia timu yetu

Vijana oya oya wa simba ambao wao huwaza mambo ya Leo tu kamwe hawatatushinda.
Yes we are conservative we will not change

Sisi tunajua mo nimfanyabiashara hatadumu pale milele kwanini anataka akabidhiwe hati ya Mali za simba?
Kwa lipi alilolifanya? Asidhani yeye ndio ametoa pesa nyingi kuliko waliomtangulia kuna matajiri walimwaga pesa simba na hawakuweka mashariti magumu Kama anayodai huyu mo

Mo sisi wazee tunakuambia ijawezekana kwenye mkutano wa simba tukawa tunakupigia makofi ili kukufurahisha ila tambua simba haiwezi kumilikiwa na mtu
Simba ni timu ya wanachama Hilo halitabadilika mpaka mwisho wa dunia

Kama pesa zako ni chungu kuzitoa rudi ukawekeze African lyion uliyoikimbia

Ila simba huku hautapaweza huku hakuna ngombe aliyekatwa mkia huku wote ni makambale, utatamba miaka mitatu mingapi mwisho tutakukata kichwa jifunze kwa manji sio kwamba haipendi Yanga ila alitaka kuichikua yanga iwe ya kwake ila watu wasioonekana walimshinda

Hata Hapo simba inawezekana wanaoonekana kina kingwangwala and kina makonda unawamudu ila nikutoe shaka Hao hawana nguvu yeyote ndani ya simba ni Kama waburudishaji tu

Wenye nguvu ni Hawa aina ya kina kilomoni wapo wengi hawapo mitandaoni utakwama tu

Mzee kilomoni sisi wanasimba Tupo pamoja na wewe acha mashabiki wapige kelele mitandaoni
Simba haitabadilika kwa tamaa ya fedha ya mlo mmoja
Kila kijiji hakikosi wazee
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Back
Top Bottom