Mzee Kinana Umetukataza Kukagua Taa za Magari Mchana, Sawa Tumekuelewa

Mzee Kinana Umetukataza Kukagua Taa za Magari Mchana, Sawa Tumekuelewa

Elimu tunatoa sana, tatizo mnatuona sisi ni vilaza na wala rushwa unamsimamisha mtu unampa elimu yeye anakupa elfu 5 hujamwomba ila ameamua tu anaona kama unamsumbua vile Sasa mtu kama huyo wewe ungemsaidiaje?
Mpe elimu ya USALAMA kama akikupa mwenyewe chukua, sio kumtafutia namna ya yeye kujiona ana hatia ili atoe!!
KITAKACHO PUNGUZA AJAILI NI ELIMU NA SIO FAINI...
 
Mkuu sema ukweli ukipewa mashine ya faini, ukarudisha bila ya pesa INAKUWAJE kwa wakubwa??
Usema mimi nilikwa natoa onyo kwa madereva na kuwapa elimu..
Inategemea na hao wakubwa ila mtaani kuna story nyingi za uongo kuhusu vyombo vya ulinzi, inafika mahali akari tunaona maisha hayana maana.
 
Kumbe povu lote kisa umebadilishwa idara
Poti uraiani utusaidie kukimbiza na mateja na wauza gongo[emoji16]
 
Inategemea na hao wakubwa ila mtaani kuna story nyingi za uongo kuhusu vyombo vya ulinzi, inafika mahali akari tunaona maisha hayana maana.

Pole sana, unaandika kwa hisia hadi sauti inasikika.

Wako askari waadilifu na wasio waadilofu.

Wasio waadilifu kwenye sekta ya usalama barabarani ndo wamebeba hulka kuwa askari wote wa barabarani ni wasumbufu, wala rushwa etc.
 
Inategemea na hao wakubwa ila mtaani kuna story nyingi za uongo kuhusu vyombo vya ulinzi, inafika mahali akari tunaona maisha hayana maana.
Mkuu usikate tamaa, kazi ya Uaskari ni kazi ya wito kama Ualimu na Udaktari na kazi kama hizo.
Tatizo askari huyatumia mamlaka yake zaidi ya kulinda amani ya raia na mali zao., Kwa kuwa akisema 'kaa chini', 'Lete leseni yako', 'Mikono juu' raia hutii.,hayo mamlaka ndio hutumika vibaya...
 
Baada ya agizo lako, tumeitwa na tupo kwenye utekelezaji. Nadhani ajali ya Usiku wa kuamkia leo imesababishwa na Taa.

Tunashukuru, wengine tumebadilishiwa mpaka idara ila sawa tu. Kila la kheri ndugu Kinana endelea kufurahia ku-drive maana hatuta kusumbua.
mnakera. unakaguliwa mara sita ndani ya mkoa mmoja mnauliza vitu vile vile
wekeni utaratibu wa kutokurudia ukaguzi at least on the same day
mfano unatoka kahama unaenda shinyanga, ndani ya mkoa. Unasimamishwa bijampola kwa mbele hapo karibu na daraja, unaombwa leseni, unaomba card ya gari, unaambiwa washa taa
Ukitoka phantom unaombwa vitu hivyo hivyo
kabla ya buwagi hapo vitu hivovivo
kagonwa tena
hali inaendelea hivyo kabla ya isaka na baada tu ya isaka hapo shule ya msingi
itwangi au luhumbo, tinde, baada ya tinde kuna vikosi viwili hadi vitatu kabla ya kuingia shinyanga
 
Pole sana, unaandika kwa hisia hadi sauti inasikika.

Wako askari waadilifu na wasio waadilofu.

Wasio waadilifu kwenye sekta ya usalama barabarani ndo wamebeba hulka kuwa askari wote wa barabarani ni wasumbufu, wala rushwa etc.
Askari Polisi kwa sehemu kubwa wamejawa na tamaa , nahisi wana pepo flani. Mtu akishakuwa askari polisi hata kama ndugu yako ukipata janga kule lazima akupasue mfuko
 
Back
Top Bottom