Tulikusanyika Mbezi ya Kimara kuanzia saa sita za mchana, saa kumi tukaambiwa Mzee Lowassa muda si mrefu atawasili hapo uwanjani akitokea Kawe, kulikuwa na umati wa watu sijawahi kuona. Mabasi ya mikoani hasa yale yaliyokuwa yakitoka Moshi, Arusha nk kuja Dar yalikuwa yakipita na abiria wote ndani ya mabasi wakitupungia mikono huku nwakionyesha alama ya vidole viwili.
Muda ukafika Mzee Lowass akawasili....nadhani hotuba yake ilikuwa fupi kuliko zote kuwahi kutokea dk 2 au 3 ila sio zaidi. Hata hivyo wana Mageuzi tulifurahi sana.
Nikipata nafasi nitahadithia nilivyotoka kwa mguu Luguluni kuja shule ya msingi Msakuzi kumpigia kura Lowassa na Ukawa.
Sitarudia tena kushabikia Upinzani Njaa Kama Huu wa Tanzania.....
View attachment 1041982