Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mzee Philip Mangula, Mstaafu wa nafasi ya katibu Mkuu na Makamu Mwenyekiti wa CCM amesema;
"Wakati huo tulikuwa tumeshajipanga ndio kipindi ndio kipindi ambacho walitokea wengi wanataka uongozi. Na Mimi nilianza kwa kufuatilia. Nilianzia mkoa wa Kagera nikaenda Mwanza kwenye ishu ambazo watu walikuwa wametuhumiwa mpaka nimefika Singida. Wakati huo Rais alikuwa Magufuli alinipigia simu nirudi mara Moja kwa ajili ya kikao.
Nilifika nyumbani kwangu hapa, siku inayofuata asubuhi najiandaa kwenda ofisini. Nikipofika ofisini niliwasha AC. Nilipokaa kama dakika Tano nilijisikia kutapika. Nilitapika sana. Baadae niliambiwa Mwenyekiti (Hayati John Magufuli) anawasili ukumbini, Nikipofika kwenye ukumbi nilimwambia Dkt Bashiru Ally hali yangu sio nzuri. Nilimuomba asome ile taarifa. Alipomaliza kusoma Mwenyekiti alisema kikao kimefungwa.
Nikipofika ofisini nilipokaa kama dakika 10 hali ilijirudia tena. Nilitapika sana. Mbavu zikawa zinauma. Nikaanguka chini. Wasaidizi walifika kuniangalia. Wakanikuta ndipo chini chooni na nimezimia. Walimpigia simu Magufuli akasema mbona nilikuwa nae kikaoni? Walinikimbiza hospitali ya Muhimbili. Nilishtuka Saa 12 Jioni. Nilishangaa kujikuta nimewekewa oxygen.
"Bahati mbaya Mkuu wa Polisi alitangaza kuwa nipo hospitalini inasemekana amepatikana na sumu mwilini na watafanya utafiti kumgundua aliyenipa sumu na atachukuliwa hatua. Ile kauli iliwatia watu hofu. Baada siku 10 nilitoka hospitali niliwaambia waachane na ile kauli ni kuwatia watu hofu tu. Nilikuwa nimeshapona. Mpaka leo sijui ilikuwa ni kitu gani!"