Mzee Mangula: Magufuli hakutoa Rushwa kwenye mchakato wa uchaguzi 2015. Wajumbe walimuunga mkono Lowassa

Mzee Mangula: Magufuli hakutoa Rushwa kwenye mchakato wa uchaguzi 2015. Wajumbe walimuunga mkono Lowassa

Yote hayo alikuwa anayafanya kwa maslahi ya taifa zima na wananchi wake na hakuwahi kufanya jambo lolote kwa maslahi yake au ya chama chake

Yeye kipaumbele chake kama mlikuwa hamjui ni MMOJA AUMIE ILI MAMIA WAPONE sasa hapo kosa lake kubwa ni lipi na pia mambo hayo ya utekaji sijui kuuliwa mengine ilikuwa ni mpango wa watu wengine ili kumtengenezea picha mbaya katika utawala wake ila kiufupi JPM ni Rais Bora kuwahi kutokea Tanzania na itachukua mia kumpata kama yeye
Kwa hiyo hata lile zoezi la kuwaengua wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi, au kuwaibia kura zao na hivyo tume kuwatangaza wagombea wa ccm pekee kama ndiyo washindi; lengo lilikuwa kulinda maslahi ya wananchi na Taifa!
 
Tatizo la Jiwe ni kuitindiga Katiba kama kikaratasi, Kumtwanga risasi Lissu, kuanza michezo ya kuteka na kupoteza watu, kuanza kununua wapinzani. kuweka bunge lake mwenyewe bila ridhaa ya wananchi, kuvuruga chaguzi za serikali za mitaa (2019) kwa kiwango cha aibu. Aliwafundisha viongozi wajao wa CCM kuwa kuna shortcut ya power nayo ni kuteka watu, kuvunjavunja katiba na taratibu, kuiba uchaguzi mzima bila hata kuremberemba, na kuvuruga haki za watu wengine kwa sababu tu una nguvu.

Aliinajisi nchi
 
Kwa hiyo hata lile zoezi la kuwaengua wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi, au kuwaibia kura zao na hivyo tume kuwatangaza wagombea wa ccm pekee kama ndiyo washindi; lengo lilikuwa kulinda maslahi ya wananchi na Taifa!
Mkuu kwani JPM ndiye aliyekuwa Msimamizi wa mambo yote hayo uliyoyataja? Kwa nini mnamtaja JPM kwa hayo mambo kwani yeye ni tume? Yeye ni Polisi? Yeye ndiye mhesabuji wa kura? Au yeye ndiye mtangaza matokeo? JPM hakuwa na shida kabisa hata tukifatilia hotuba zake zilikuwa ni zenye akili na afya kwa taifa zima yeye hakuwa tayari kutugawanya hata kidogo.
 
Sahihi kabisa! Na ikumbukwe yeye ndiye chanzo kikuu cha kuporomoka kwa kiwango cha demokrasia nchini! Yeye ndiye muasisi wa hiki kinachoendelea sasa;
1. kwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa!
2. Kuteka na kuwapoteza wakosoaji wake. mfano Ben Saanane, Azory Gwanda, nk.
3. Kuruhusu Lissu na wanasiasa wenzakekukamatwa kwa kesi nyingi za uchochezi, na baadaye kushambuliwa kwa risasi.
4. Yeye ndiyo muasisi wa siasa za kutukuzana (uchawa). Tanzania ya Magufuli, serikali ya Magufuli, nk.
5. Aliasisi dhuluma na uonevu kwenye uchaguzi. Wapinzani walienguliwa na pia kura zao kuibwa waziwazi na hivyo kuifanya ccm ishinde uchaguzi wa serikali za mitaa kwa urahisi 2019, na ule uchaguzi mkuu wa 2020.

Alinukuliwa akisema wananchi watakao wachagua wapinzani hawatapelekewa huduma za kijamii (maendeleo)! Wakurugenzi walitishwa kutumbuliwa iwapo watawatangaza wapinzani (huku yeue Magufuli akiwapataia magari na mafita ya bure)!

Kwa hiyo tusisahau haya mapungufu yake wakati wanajadili hayo mazuri yake.
Umeainisha mapungufu karibu yote,haya mambo ni utaratibu wa miaka yote ila tofauti ni kuwa anko aliweka wazi mambo yake iwe mabaya ama mazuri.
Utekaji,dhulma kwa wapinzani kuanzia awamu ya tatu yalifanyika lakini nyuma ya pazia!
 
Back
Top Bottom