Tatizo la Jiwe ni kuitindiga Katiba kama kikaratasi, Kumtwanga risasi Lissu, kuanza michezo ya kuteka na kupoteza watu, kuanza kununua wapinzani. kuweka bunge lake mwenyewe bila ridhaa ya wananchi, kuvuruga chaguzi za serikali za mitaa (2019) kwa kiwango cha aibu. Aliwafundisha viongozi wajao wa CCM kuwa kuna shortcut ya power nayo ni kuteka watu, kuvunjavunja katiba na taratibu, kuiba uchaguzi mzima bila hata kuremberemba, na kuvuruga haki za watu wengine kwa sababu tu una nguvu.