Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
Tofauti na wazee wengine ambao wakifikia umri kama alionao nao mzee Mangula akili huwa zinashindwa kufanya kazi vizuri lakini kwa huyu MTU sivyo kabisa.
Siku zote ni mtu anayetumia busara na hekima kubwa katika kuzungumza kwake licha ya umri alionao tungeshuhudia vituko vingi katika maneno yake ambavyo vingechagizwa na umri.
Mzee Mangula si mtu wa maneno mengi ,ni mtu anayesema kwa uchache sana na hotuba au maneno yake yakabaki nukuu kwa muda mrefu sana.
Ni nani huyu mzee mpaka awe ni mjadala wa kitaifa? Licha ya kwamba hana mamlaka yoyote ya kiserikali au kidola lakini kauli yake inaweza kufunga mjadala unaondelea nchini, mfano ni kauli yake juu ya bandari ya bagamoyo.
Nchi yetu imejaliwa viongozi wenye busara na hekima licha ya umri walionao bado wanaweza kufanya maamuzi bora na sahihi kwa ustawi wa nchi yetu.
Nimalize kwa kusema kwamba wana bahati kubwa sana wote waliopitia mikononi mwake kiungozi hakika wamepita mikono salama yenye kuaminika kwa watanzania.
Ombi:
Mwenye mawasiliano ya simu ya mzee Mangula naomba anipatie kuna mambo ya msingi sana ya kumwambia.