hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,544
Malofa na wapumbavu hawaishiwi na vituko.
Kituko cha mwaka, yule mliyemuita fisadi leo yuko juu kwenye chama cha wapumbavu kuliko Katibu Mkuu wake.
Hivi Katibu mkuu wa malofa kaishia wapi?
CCM mmeamua kutukana wapiga kura mmezidi kumuharibia magufuli.
hichi kibri mlichonacho ndiyokimefika mwisho.
Wana JF Heshima kwenu.
Mithali 26:5
Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.
Aidha neno upumbavu limeandikwa zaidi ya mara 46 katika Biblia. Mfano :-
Mithali 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.
Aidha Rais wa kwanza wa TZ; Mwl Nyerere amekuwa akitumia neno hili mara nyingi sana. Huko ndiko Mhe. MKAPA alipojifunzia. (Nimeshindwa kuweka video clip msaada plz)
Mhe. Sugu alipotumia neno mpumbavu pale mjengoni UKAWA walimtetea. Leo kwao limetumika imekuwa nongwa kwenye mitandao. Kweli nyani haoni naniii yake.
Mhe. Mkapa ni Mkristo mzuri mwenye kusoma Neno la Mungu kila wakati. Alichofanya ni kujibu hoja ambayo ameipima na kuiona ni ya kipumbavu ili walioitoa wasijione wana akili.
Nani asiyejua Mhe. Sumaye alibatizwa jina la utani la ZIRO!!! Kwanini mlimuita hivyo na Kipanya alichora katuni nyingi za ZIRO. Mhe. Mkama anamjua sana Mhe. Sumaye. Hivyo amemjibu SAWASAWA na UPUMBAVU wake. Mbona wanawake tunapohubiriwa tusiwe wapumbavu hawasemi wametukanwa???
Hakuna shida hapo, message sent and delivered.
Queen Esther
Mkapa ni jembe ana kichinjio cha Alshabab, atakisaidia sana kuwashughulikia malofa wanaovunja vituo vya polisi na kupora silaha!Malofa na wapumbavu hawaishiwi na vituko.Kituko cha mwaka, yule mliyemuita fisadi leo yuko juu kwenye chama cha wapumbavu kuliko Katibu Mkuu wake.Hivi Katibu mkuu wa malofa kaishia wapi?
'Birds of the same feather flock together/Birds of a feather flock together' Kama JK ni swahiba wa Lowasa na Lowassa ni fisadi you can do the math!
Mwisho wa yote october 25, aibu yako au aibu yangu. TATU BILA!
Mkuu mimi nimekuonyesha takwimu kidogo tu hapo. Wasiokuwa wanachama wa vyama vya siasa ni wengi sana kuliko unavyofikiria. Waliojiandikisha wanaweza kuwa milioni 22, lakini watakaopiga kura siyo idadi hiyo! Wengi wamejiandikisha kwa sababu zao binafsi kama kusajili line, kuwekeana dhamana mahakamani, kufungulia akaunti benki, kupatia tiketi za treni (Kigoma) n.k. Kwa hiyo usijipe matumaini kuwa nusu ya watanzania ni upinzani au watapigia upinzani.Udiropoke tu mkuu, unaelewa idadi wanachama wote wa CHADEMA, CUF,NCCR,NLD na vyama Vingine? Wasiokua na vyama idadi yao unaijua? Idadi ya under 18 ambao ni sawa na wajukuu wa Mkapa ambao wamemdharau unaijua?
Jana mzee Mkapa alimwaga radhi, CCM nayo ikamwaga radhi.
Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipopata wasaa wa kuhutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliokuwa uwanjani wa Jangwani, alirusha kijembe kwa wapinzani na kusema wanaosema wanatafuta ukombozi ni wapumbavu na malofa.
"Kuna vyama vinajifanya vinataka kuleta ukombozi, ukombozi uliletwa na ASP na Tanu, hao wanaojiita vyama vya ukombozi ni wapumbavu, … ni malofa, nchi hii ilikwisha kombolewa na sasa inaendelea kuiomboa kwa kupambana ana umasikini, ujinga na maradhi na ndo kazi imekuwa ikifanywa na serikali zote zilizopita kuanzia ile ya awamu ya kwanza na hii inayokuja itafanywa na serikali ya Dk. Magufuli," alisema.
Mzee niliyemzoea kwa hoja zenye mashiko na takwimu akageuka mlevi asiyejiheshimu.
Kweli ufalme wa CCM umefitinika.Kati ya mambo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiitofautisha brand ya CCM na Upinzani ni kule kutumia lugha zenye staha,kuhubiri amani na kuiishi.Jana rasmi CCM imevunja ndoa yake na sifa hizi.
Sasa tunaanza kupata picha tukimtazama Makonda, baadae Nape,Wasira,Kamani,Job Ndugai na sasa Mkapa tunaona CCM mpya inayozaliwa; brand ya ngumi,matusi na lugha za mihemko.
Mimi niwaambie tu,busara na hekima ni tunu ila ujinga hafundishwi mtu.Ni suala la kuamua tu!
Magufuli karibu UKAWA,you are a good manager but not a leader.
Nilikuwa na mheshimu sana Mzee Mkapa na nashindwa kuelewa jana either ni nin alitumia kabla ya kupanda pale jukwani haikuwa akili yake...Na amearibu historia yake aliyokuwa amejijengea kwa wananchi .
nchi hii ilishakombolewa na wazee wetu wakiongozwa na mw. nyerere miaka dahali iliopita sasa anakuja mtu anasema anataka kutukomboa ni ukosefu wa akili tena narudia mpumbavu mkubwa
Faiza hi!Malofa na wapumbavu hawaishiwi na vituko.
Kituko cha mwaka, yule mliyemuita fisadi leo yuko juu kwenye chama cha wapumbavu kuliko Katibu Mkuu wake.
Hivi Katibu mkuu wa malofa kaishia wapi?