wadau salaam,
ni wazi sasa mgombea urais kupitia ukawa mhe. Edward lowassa amekuja kuwaonyesha aina mpya ya siasa ambayo wapinzani hawakuizoea, siasa ya kukaa karibu na wananchi kwa kuwatembelea katika mazingira yao na kujua shida zao. Kwangu mimi hii ni mbinu kali sana kisiasa, utakumbuka mbinu hii imetumiwa sana na katibu mkuu wa ccm ndugu kinana hivi karibuni na imefanikiwa kuirejesha ccm angalau kwenye mstari maana ilikuwa icu.
Hakika mhe. Lowassa anafanikiwa kwenye hili kwa maana tulizoea upinzani wa kuporomosha maneno makali ya kejeli lakini cha kushangaza mtindo huo wa kejeli tena usio na hoja umehamia kwa jirani zao wa ccm tena ma senior wa chama kama mzee mkapa ndio vinara wa hili. Mkapa aliamua kuwatukana watanzania wenzake kwa kuwaita wapumbavu na malofa kwa sababu tu wanadai ukombozi wa mtanzania. Mzee wangu mkapa amesahau kuwa neno ukombozi ni dhana na sio lazima limaanishe ukombozi kutoka kwenye ukoloni tu bali mtu unaweza kuhitaji ukombozi katika mazingira mbalimbali ya kisiasa,ki jamii, na hata kiuchumi.
Kwa fikra zangu za kipumbavu na ki lofa nakiona kifo cha ccm kama itaendeleza siasa za aina hii tena zikiendeshwa na watu wakubwa kama mzee wangu mkapa