Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Wadau Salaam,
Ni wazi sasa mgombea urais kupitia UKAWA Mhe. Edward Lowassa amekuja kuwaonyesha aina mpya ya siasa ambayo wapinzani hawakuizoea, siasa ya kukaa karibu na wananchi kwa kuwatembelea katika mazingira yao na kujua shida zao.

Kweli wewe lofa, unashindwa kutofautisha siasa na futuhi...

We want our Slaa back
 
wadau salaam,
ni wazi sasa mgombea urais kupitia ukawa mhe. Edward lowassa amekuja kuwaonyesha aina mpya ya siasa ambayo wapinzani hawakuizoea, siasa ya kukaa karibu na wananchi kwa kuwatembelea katika mazingira yao na kujua shida zao. Kwangu mimi hii ni mbinu kali sana kisiasa, utakumbuka mbinu hii imetumiwa sana na katibu mkuu wa ccm ndugu kinana hivi karibuni na imefanikiwa kuirejesha ccm angalau kwenye mstari maana ilikuwa icu.

Hakika mhe. Lowassa anafanikiwa kwenye hili kwa maana tulizoea upinzani wa kuporomosha maneno makali ya kejeli lakini cha kushangaza mtindo huo wa kejeli tena usio na hoja umehamia kwa jirani zao wa ccm tena ma senior wa chama kama mzee mkapa ndio vinara wa hili. Mkapa aliamua kuwatukana watanzania wenzake kwa kuwaita wapumbavu na malofa kwa sababu tu wanadai ukombozi wa mtanzania. Mzee wangu mkapa amesahau kuwa neno ukombozi ni dhana na sio lazima limaanishe ukombozi kutoka kwenye ukoloni tu bali mtu unaweza kuhitaji ukombozi katika mazingira mbalimbali ya kisiasa,ki jamii, na hata kiuchumi.

Kwa fikra zangu za kipumbavu na ki lofa nakiona kifo cha ccm kama itaendeleza siasa za aina hii tena zikiendeshwa na watu wakubwa kama mzee wangu mkapa

nyie propaganda za namna hii nafikiri unajifanya kuelimisha kumbe ni kutafuta umaarufu ,
nakuuliza kuna sehemu mkapa alisema watanzania ni wapumbavu na malofa kweli?

Haitasaidia maana hata wewe unachotaka kuelimisha bado miemuko ya siasa ndo imekuzunguka tu,

ukiamua kuelimisha simama katikata usiongeze chunvi wala sukari ili kuwasidia viongozi unaotaka kuwaelimisha,

 
attachment.php

miaka 35 serikalini lowasa amelifanyia nini taifa ambacho tunakiona kila kona ya nchi hii,

ukijiuliza haya utaweza kujua tunatafuta rais au ni uchaguzi wa kubadirisha vyama maana ikulu hakiingi chama bali wanaingia watu ambao tunawapima kwa waliyotufanyia miaka yao ya utumishi katika kila kona ya nchi hii,

 
kweli wewe lofa, unashindwa kutofautisha siasa na futuhi...

We want our slaa back

mkuu ungemuliza akiwa waziri mkuu na mtendaji mkuu wa serikali alishawai kwenda kuona maisha ya sisi wa chini?
Monduli jimboni kwake miaka yote ya ubunge alishawai kupanda daradara?
Je miaka yote ya umbunge alishawai kutembelea mayata(manyumba ya udongo ) yaliyojaa monduli mjini na kuingia kuona wanavyolala na kuishi ?

Mkuu akikujibu hayo
utamsaidi kujua maigizo ya siasa na siasa halisi,

 
Nimeamini mafuriko hayazuiliki kwa mikono.Yaani yameibukia tandale tena!!!Duh!!!
 
Napenda kuchukua fursa hii adhimu kumpongeza kwa dhati kabisa Rais mstaafu, Mh William Benjamin Mkapa, kwa kuwaambia watanzania ukweli pasipo kumumunya maneno, kupepesa macho wala kutikisa masikio. Ijapokuwa hata makada wengine wa CCM wamekuwa wakisema ukweli katika kauli zao mbalimbali lakini Mh Profesa Mkapa amesema ukweli zaidi. Ametamka ukweli usioweza kupingwa na mtu yeyote, awe zezeta au mwenye akili zilizotimia. Nianze na kauli za mkapa kabla sijaangazia kauli za makada wengine waandamizi wa CCM.

Watanzania ni MALOFA na WAPUMBAVU. Hapa naomba nisisitize kauli hii ya Profesa Mkapa. Sio tu kwamba watanzania ni malofa mifukoni mwao lakini pia ni malofa katika vichwa vyao. Omba sana uwe lofa mifukoni lakini sio kichwani. Ukiwa lofa kichwani akili zako zitafanana na za kuku au konokono. Ulofa wa watanzania ndio unaowapelekea kuwa WAPUMBAVU. Ni bahati mbaya kwamba watanzania wengi ni malofa na pia ni wapumbavu. Ulofa huzaa upumbavu na upumbavu huzaa ulofa. Ulofa na upumbavu ni sawa na kuku na yai. Haiwezekani kutenganisha sifa hizi mbili kama ilivyo vigumu kutenganisha kuku na mayai.
maisha bora-hali mbaya xana!.jpg maisha bora-masikini wa kutupwa.jpg maisha bora-nyumba bora.jpg
Ni ulofa na upumbavu ndio unaopelekea watanzania kusomesha watoto wao kwenye shule za kata—shule ambazo hazina walimu, madawati, vitabu wala maabara huku wadosi wakisomesha watoto wao kwenye shule za intaneshno na englishi mediamu. Na sio tu kwamba ulofa na upumbavu wao huwafanya wasomeshe watoto wao kwenye shule hizo bali pia huwafanya washindwe kuwanunulia watoto wao walau kigoda cha Tsh 500/= kwa ajili ya kukalia wawapo darasani. Kwa ujumla, ulofa ndio chanzo cha watanzania kutopata huduma muhimu za kijamii.
maisha bora-hali mbaya xana!.jpg bonge ya shule.jpg ambulance ya CCM.jpg ambulance ya CCM2.jpg wanafunzi wamekalia matofali.jpg wanafunzi wamekalia udongo.jpg wanafunzi wakisomea chini ya mkorosho.jpg wanafunzi wakisomea nje ya darasa.jpg wanafunzi chini ya mbuyu.jpg
Aidha ulofa na upumbavu wa watanzania hupelekea kutibiwa kwenye hospitali za umma huku wadosi wakitibiwa India, Ujerumani, Uingereza na kwingineko huko ughaibuni. Hali kadhalika ulofa huwafanya wakose pesa za kununua dawa kwenye maduka yaliyopo ndani ya hospitali na pia kushindwa kuwanunulia wagonjwa wao magodoro na vitanda ili pindi waendapo hospitali walalie. Kama mtu unakosa Tsh 200/= za kununua panadol kwenye maduka yaliyomo ndani ya hospitali za umma utasemaje wewe sio lofa?
huduma bora.jpg huduma safi.jpg
Ni ulofa huo huo ndio unaopelekea watanzania kuuza kura zao kwa bakuli moja la ubwabwa, kopo moja la mataputapu, gram 200 za chumvi ya Tsh 100/=, kofia na vitenge kutoka kwa wadosi wenye nazo. Pia ulofa wetu unatufanya tukose Tsh 50/= za kununulia fungu moja la mchicha kwenye soko la Mchambawima wakati wadosi wana uwezo wa kuchukua milioni 10 za kununulia mboga. Ulofa wa wazazi wetu ulisababishwa tusomeshwe kwenye shule za kata na hivyo kukosa fursa ya kupata elimu iliyo makinika na itakayotuwezesha kutoa “ushauri” ili tulipwe Tsh 1.6 bilioni kwa kazi hiyo ya kutoa “ushauri wa kiufundi”. Huu ndio ukweli ambao watanzania hamuwezi kuupinga. Kama kuna mtu atapinga basi anahitaji akapimwe akili zake Milembe.
maisha bora-mbege.jpg maisha bora,.jpg View attachment 280381
Jamani hebu tuwe wakweli. Ulofa ni sifa ya watanzania na wala hakuna anayeweza kukataa ukweli huu. Tunapaswa kumpongeza Mh Mkapa kwa dhati kabisa kwa kauli zake za kweli na zinazozingatia maslahi mapana ya kitaifa.

Sasa nisemee ukweli uliomo kwenye kauli zingine zilizowahi kutolewa na makada maarufu hapa nchini. Oil ikishatumika sana kwenye gari huchafuka na hatimaye humwagwa chini. Naunga mkono kwamba watanzania ni OIL CHAFU. Kama mmetumiwa tangu mwaka 1961 mpaka leo na hamna namna nyingine ya kujinasua kutoka kwenye matumizi hayo mtakataaje kuitwa oil chafu? Nawashangaa sana! Ndio, sisi watanzania ni oil chafu…baada ya kutumiwa kwa muda mrefu sasa hatuna thamani tena…tunahitaji kumwagwa chini ili tusije tukaleta mushkeli kwenye gari la mabwana wakubwa.

Mtu akishatufuna muwa au kula ndizi hutupa MAKAPI chini na kuyaacha yaozee pale. Hakuna mtu mwenye akili zilizotimia ambaye akimaliza kutafuna muwa au ndizi huhifadhi makapi. Baada ya kutumikishwa kwa zaidi ya miaka 54 sasa watanzania tumekuwa makapi. Hatuna tahamani tena mbele ya watafunaji. Tunapaswa ama kuchomwa moto au kuzikwa ardhini tuwe mbolea. Sharti tukubaliane kwamba watanzania tumetafunwa na kunyonywa sana hadi tumebaki makapi tupu tusiokuwa na chembe ya thamani mbele ya watafunaji. Na uzuri ni kwamba mtu akishashiba hakumbuki kama kesho atapata njaa. Ifike wakati tukatae kutafunwa na kubaki makapi kama tulivyozoea kutafunwa kila msimu wa mavuno unapokaribia. Yatupasa tutengeneze sumu kali ambayo itawafanya watafunaji washindwe kututafuna tena msimu huu wa mavuno.

VIBAKA huiba mali za watu wengine baada ya kukosa kazi ya kufanya au baada ya kutelekezwa na jamii inayowazunguka. Baada ya serikali kuuza viwanda na ardhi kwa mabeberu na magabacholi, watanzania wamebaki hawana kazi wala ardhi ya kulima. Wamegeuka kuwa vibaka na kero kwa wawekezaji. Ndio maana kila kukicha tunashuhudia vibaka hawa wakipora mali za wawekezaji. Dawa yao ni kuwapiga mabomu na virungu mpaka watie akili. Hakuna hata haja ya kuwafikisha mahakamani—wananchi wenye hasira watashughulika nao mpaka wajute kuzaliwa kwenye ardhi hii ya Tanzania. Waacheni “wawekezaji” waifaune nchi na “wawekezwaji” wafurahie 10% zao walizozipata baada ya kuuza viwanda na kupora ardhi ya watanzania.
panya road.jpg
Kila mwenye akili timamu atakuwa ameng’amua ukweli uliojificha kwenye mafumbo haya yanayosemwa na makada kila kukicha. Watanzania mnapaswa kubungua bongo zenu muelewe kwamba mafumbo haya hayasemwi kwa bahati mbaya bali yanasemwa kwa makusudi ili kuwafungua akili zenu zilizofungwa na wachawi kutoka kuzimu. Lakini kwa kuwa mu malofa na wapumbavu, itawachukua muda mrefu kuelewa ukweli uliojificha kwenye mafumbo haya. Na akili zenu zikifunguka mtakuta rasilimali zote za taifa zimefyonzwa na kusalia makapi. Kwani hamuoni jinsi ardhi yetu inavyochimwa na kuachwa mahandaki? Ardhi isiyokuwa na kitu ni sawa na makapi. Ni juu yako ewe mtanzania kuamua uendelee kubaki kwenye fungu la malofa, wapumbavu, oil chafu, makapi na vibaka. Saa ya kujikomboa kutoka kwenye makundi hayo ni sasa. Fumbo mfumbie mjinga, mwerevu ataling’amua. Tafakari, chukua hatua!
:yield:
 
Wahusika wakuu hapa penye hii sindano wanapapita utafikiri kuna moto...

mkuu big up
 
Hizi picha za tangu 2005. Tunapotezeana wakati. Hali haipo kama unavyojaribu kuaminisha watu. Na mkapa hakusema watanzania ni wapumbavu alisema chama kinachojifanya ni cha ukombozi leo baada ya 50yrs of independence ni wapumbavu na malofa. Shida wewe na UKAWA wote mmeona hamna hoja za kuzungumza sasa hivi baada ya kila vipaumbele kuguswa not Dr magufuli mnaanza kutafuta huruma ya watanzania na kuanza kutoa sababu za kushindwa sasa. Poleni sana uchaguzi huu mmeshapoteza ccm watashinda mchana kweupe
 
Lakini huyo Mkapa si alikubali kuwa rais wa malofa na wapumbavu? Basi yeye atakuwa ni mpumbavu mara mbili!
 
mkapa hakusema watanzania ni wapumbavu
alisema chama kinachojifanya ni cha ukombozi
leo baada ya 50yrs of independence ni
wapumbavu na malofa. Shida wewe na UKAWA
wote mmeona hamna hoja za kuzungumza sasa
hivi baada ya kila vipaumbele kuguswa not Dr
magufuli mnaanza kutafuta huruma ya
watanzania na kuanza kutoa sababu za
kushindwa sasa. Poleni sana uchaguzi huu
mmeshapoteza ccm watashinda mchana kweupe
 
Hii ni sawa na kumtukana mtoto wako wa kuzaa "mbwa" wakati ukiwa unafahamu wazi kuwa mbwa huzaa mbwa! Hivyo basi mama yake huyo mbwa ni wewe mwenyewe!
 
Kwa hali mbaya tuliyonayo watz ikulu panahitajika timu mpya sio kepteni mpya. La sivyo timu iliyopo itaendelea kutuona wapumbavu, maana kila mwaka wa uchaguzi tunadanganywa tunakubali. Na timu iliyopo haiwezi kukubali katiba inayotoa usawa kwa wote, ingeshakubali siku nyingi. Hawataki mabadiliko ya katiba yatakayoziba mianya ya ufisadi papa, au kuhoji ukiritimba wa madaraka. n.k.

Kwani ccm ndio watawala wa milele tz? Vyama vingi vya nini sasa? Kumdanganya Obama?
Kwa nini ukihoji mabadiliko ya serikali unaitwa pumbavu?

So tuchague UKAWA ili tupate katiba mpya itakayotoa haki sawa kwa wapumbavu na wasio wapumbavu wa nchi hii.
Hayo ndio maoni yangu ya kipumbavu baada ya kupata kiroba.
 
Hizi picha za tangu 2005. Tunapotezeana wakati. Hali haipo kama unavyojaribu kuaminisha watu. Na mkapa hakusema watanzania ni wapumbavu alisema chama kinachojifanya ni cha ukombozi leo baada ya 50yrs of independence ni wapumbavu na malofa. Shida wewe na UKAWA wote mmeona hamna hoja za kuzungumza sasa hivi baada ya kila vipaumbele kuguswa not Dr magufuli mnaanza kutafuta huruma ya watanzania na kuanza kutoa sababu za kushindwa sasa. Poleni sana uchaguzi huu mmeshapoteza ccm watashinda mchana kweupe

uliona wapi chama hakina watu labda nikueleze chama ni watu

wanaposema ukombozi hawamaanishi ukombozi toka kwa mzungu bali ni ukombozi wa

UMASKINI
MARADHI
UJINGA
UFISADI

mambo ambayo tangu tupate uhuru yanatuksndamiza as if hatuna uongozi

hii ndo sababu huyo ndg kalela hizo PICHA ili wasioelewa waelewe
 
Back
Top Bottom