Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Sijui nani karuhusu huu uhuru wa atusi tz. Chapa chapa wooote wenye matusi!lol!

Upumbavu sio tusi, ni wasifu wa ndani wa mtu, yaani mtu anayejui kama hajui na hataki kujua, huyo ni mpumbavu. Lakin yule ambaye anajua kuwa hajua na akataka kujua, huyo ni mjinga anataka kuondoa ujinga wake
 
nchi hii ilishakombolewa na wazee wetu wakiongozwa na mw. nyerere miaka dahali iliopita sasa anakuja mtu anasema anataka kutukomboa ni ukosefu wa akili tena narudia mpumbavu mkubwa
Wazee wetu hao walitukomboa toka makucha ya mkoloni. Wakatudanganya tupo huru kumbe wakatuweka kwenye makucha ya CCM . Mtu mweusi anatutawala. Anatuchagulia viomgozi wetu. Anatuchagulia dawa gani ziwe hospitali, anaamua watoto wetu waende shule gani. Je ndugu unajiona umekomboka! Biblia inatufundisha kuziwa mara ya pili. May be this Tanzania need a second birth!
 
</script>width:100%; height:100px" dir="ltr">
Kwa kumjuwa sana hivyo na bado akamweka waziri mkuu kwa miaka kumi na huo upumbavu wake, je mpumbavu hapo ni nani??

swali zuri sana hili na ikiwezekana wakati akiomba msamaha kwa kuwatukana wapiga kura wake atuambie ni kwanini alituteulia waziri mkuu mpumbavu na lofa kutuongoza kwa miaka kumi? Lengo lake lilikuwa nini?
 
Huyo mtoto wa kike mweusi nishafanya kazi naye kona moja hivi...
 
Uongozi Ni Mkufa Kuja Kwa Sumai Ni Kuwa Sehemu Ya Mkufu Hakuja Kufundisha Kaja Kusaidia
 
Jana mzee Mkapa alimwaga radhi, CCM nayo ikamwaga radhi.

Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipopata wasaa wa kuhutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliokuwa uwanjani wa Jangwani, alirusha kijembe kwa wapinzani na kusema wanaosema wanatafuta ukombozi ni wapumbavu na malofa.

“Kuna vyama vinajifanya vinataka kuleta ukombozi, ukombozi uliletwa na ASP na Tanu, hao wanaojiita vyama vya ukombozi ni wapumbavu, … ni malofa, nchi hii ilikwisha kombolewa na sasa inaendelea kuiomboa kwa kupambana ana umasikini, ujinga na maradhi na ndo kazi imekuwa ikifanywa na serikali zote zilizopita kuanzia ile ya awamu ya kwanza na hii inayokuja itafanywa na serikali ya Dk. Magufuli,” alisema.

Mzee niliyemzoea kwa hoja zenye mashiko na takwimu akageuka mlevi asiyejiheshimu.

Kweli ufalme wa CCM umefitinika.Kati ya mambo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiitofautisha brand ya CCM na Upinzani ni kule kutumia lugha zenye staha,kuhubiri amani na kuiishi.Jana rasmi CCM imevunja ndoa yake na sifa hizi.

Sasa tunaanza kupata picha tukimtazama Makonda, baadae Nape,Wasira,Kamani,Job Ndugai na sasa Mkapa tunaona CCM mpya inayozaliwa; brand ya ngumi,matusi na lugha za mihemko.

Mimi niwaambie tu,busara na hekima ni tunu ila ujinga hafundishwi mtu.Ni suala la kuamua tu!

Magufuli karibu UKAWA,you are a good manager but not a leader.

BURIANI CCM!

Uko sahihi kwa jambo moja..CCM safari hii wanatumia lugha ambazo Chadema wamekuwa wanazitumia sana kwenye majukwaa yao.
Sugu alishaita viongozi bungeni na alitetea sana hajatukana na akasema upumbavu ni "lack of knowledge or understanding".

Mnyika naye alishakuwa maarufu kwa kutumia neno "dhaifu" bungeni. Sina haja ya kukwambia neno hilo lilichukua kasi kiasi gani.

Mwaka huu kwa mtizamo wangu CCM wameamua kujibu mapigo na kutumia maneno na mbinu zile zile za ukawa..mafuriko kwa mafuriko..lugha kali kwa lugha kali.
CCM wamebadili gia angani na kiwaacha wengi wameduwaa maanake walitegemea wakae kiCCM na wapigwe kiCCM. Hata Dr. Shieni ambaye huwa ni mkimya na mtulivu alipiga kijembe kikali cha "wembe utawanyoa pande zote..mbele na..."

Mara nyingi CCM imeitwa sana Fisiemu hata humu jukwaani.Na wafuasi wao wamezomewa sana hadi kipindi flani JK akawaambia wasiwe wanyonge.

CCM ya mwaka huu maji yako shingoni..ni jino kwa jino na jicho kwa jicho.

Kama sababu yako ya kupigia Ukawa ni "matusi" ya Ukawa pole sana.

Angalizo tu; mgombea ni nani kati ya Magufuli na Mkapa? Angalia usijejikuta unatafuta jina la Mbowe kwenye karatsi wa kupigai kura.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani ungeuliza kwanza ukombozi upi maana nchi haijakombolewa katika mambo mengi.uchumi,wizi,elimu etc
 
13.jpg
 
Kila siku huwa najiuliza , na nimejaribu kuwaza sana sijapata jibu ,ebu watu wenye akili zao wanisaidie kunipa majibu kwani kuuliza si ujinga .

Hivi mtanzania anayeishi na mke wake tangu ujana wake hadi uzeeni na yule ambaye aliyeachana na mke wake kwa miaka kadhaa halafu akaenda kumrudia tena na kukubali kutunza watoto wa mtu mwingine nani lofa hapo.

Lakini mbili mzee ambaye anaishi na mke wake hadi uzeeni na mzee ambaye anaishi pekee yake huku akidai anaishi maisha ya kizungu wakati mswahili pure, nani lofa hapo .

Tatu , mzee uliyeruhusu kufungwa gori la nje wakati wa ujana wako na ukalazimishwa na watu ulikubali kwa sababu wewe ndio chanzo la goli hilo kwa sababu ya kutotimiza majukumu yako kama straiker katika uwanja kwa kutofunga magoli na mtanzania wa kawaida uliyeweza kuzuia magori ya nje katika mechi zako za home ground yako kwa kipindi chote cha ujana wako ,nani lofa hapo na mpumbavu.

Nne na mwisho mzee aliyeamua kukimbia kwake baada ya kupata cheo na kuhamia sehemu nyingine kabisa na mzee aliyeamua kula uzee wake na ndugu na jamaa zake katika eneo lake alilozaliwa , nani lofa na mpumbavu Hapo.

Story hii haina mahusiano na mtu yeyote wa Tanzania kwa sababu Tanzania ni nadra sana kukuta matukio kama hayo.
Mbona meambiwa ni malofa ninyi kwa vigezo vizuri tu kama chama
Jibuni hilo.
 
Walioshindwa wote wamehamia chadomo, huwajuwi?

Makapi yamenunuwa nafasi ya kugombea Urais. Uliona wapi dunia hii?

Mchagga anauzza utu wae kwa pesa na hilo Mbowe kalidhihirishia Ulimwengu.

Kama kuna watu wataechaguwa mgombea kama huyo na chama kama hicho, basi nnayakubali maneno ya Mkapa, hao watakuwa ni Wapumbavu na malofa - Mkapa.

Nilikuwa nakuheshimu sana Faiza,lakini toka leo sikuheshimu tena na nnawaambia wanajamvi,"msimuheshimu Faiza,amekuwa mlevi yeye,amekuwa mjinga yeye, alikuwa na heshima lakini msimuheshimu tena,amekuwa kama mtoto mdogo aliyevaa pampas,anajinyea yeye!
Yani amekula chakula chake sijui kala maharage ya wapi yeye!Nilikuwa namheshimu ila simuheshimu tena!
 
Uko sahihi kwa jambo moja..CCM safari hii wanatumia lugha ambazo Chadema wamekuwa wanazitumia sana kwenye majukwaa yao.
Sugu alishaita viongozi bungeni na alitetea sana hajatukana na akasema upumbavu ni "lack of knowledge or understanding".

Mnyika naye alishakuwa maarufu kwa kutumia neno "dhaifu" bungeni. Sina haja ya kukwambia neno hilo lilichukua kasi kiasi gani.

Mwaka huu kwa mtizamo wangu CCM wameamua kujibu mapigo na kutumia maneno na mbinu zile zile za ukawa..mafuriko kwa mafuriko..lugha kali kwa lugha kali.
CCM wamebadili gia angani na kiwaacha wengi wameduwaa maanake walitegemea wakae kiCCM na wapigwe kiCCM. Hata Dr. Shieni ambaye huwa ni mkimya na mtulivu alipiga kijembe kikali cha "wembe utawanyoa pande zote..mbele na..."

Mara nyingi CCM imeitwa sana Fisiemu hata humu jukwaani.Na wafuasi wao wamezomewa sana hadi kipindi flani JK akawaambia wasiwe wanyonge.

CCM ya mwaka huu maji yako shingoni..ni jino kwa jino na jicho kwa jicho.

Kama sababu yako ya kupigia Ukawa ni "matusi" ya Ukawa pole sana.

Angalizo tu; mgombea ni nani kati ya Magufuli na Mkapa? Angalia usijejikuta unatafuta jina la Mbowe kwenye karatsi wa kupigai kura.

Mkuki kwa nguruwe(CCM)kwa binadamu(CHADEMA) mchungu.
Jana wamerushiwa makmbora ya uhakika pamoja na vejembe, na kwa lugha ile ile tunayoiona humu JF.
Na JK ksema antukanwa sana kwenye mablogi, sasa UKAWA wasubiri lugha za KIBAJAJI
 
Toa maoni yako. Unaamini kuwa wapiga kura wengi ni vijana ambao ndio malofa
 
Ukiona mtu familia imemshinda jua hata uwezo wake wa kufiri uko chini hata kama ni kiongozi mkubwa
 
Nilikuwa nakuheshimu sana Faiza,lakini toka leo sikuheshimu tena na nnawaambia wanajamvi,"msimuheshimu Faiza,amekuwa mlevi yeye,amekuwa mjinga yeye, alikuwa na heshima lakini msimuheshimu tena,amekuwa kama mtoto mdogo aliyevaa pampas,anajinyea yeye!
Yani amekula chakula chake sijui kala maharage ya wapi yeye!Nilikuwa namheshimu ila simuheshimu tena!

Gwajima akikusikia atakudai fidia ya hakimiliki au kukupa sinia la malimao &#128518;&#128518;
 
Baada ya kuoneka dhahiri kuwa walioenda ukawa ni waliopoteza dira, Mzee maigizo kaona akwee daladala kutafuta huruma ya wananchi na kuleta usumbufu barabarani.
 
Pole kwa Watanzania kuelewa isivyo kauli "upumbavu na ulofa". Nami mwanzo nilielewa kama maneno hayo ni matus. Lakini maana halisi ya "mpumbavu" ni mtu asiyetumia busara katika maamuzi yake. Mara nyingi ni watu ambao hufuata upepo. Kwa mfano katika hali ambayo mtu anapita kuomba udhamini wa kutaka uongozi, watu badala ya kuendelea na shughuli zao za maisha wanakesha kumsubiri na hata kudiriki kuingia uwanja wa ndege au kupiga deki barabara, hakuna jina linalowafaa hawa watu zaidi ya "upumbavu". Mbaya zaidi ya aina hii ya watu kwa kufanya matendo kama hayo ni katika hali inayoonyesha si tu ufinyu wa fikra ila ni dalili tosha wamefirisika kimawazo. Neno sahihi ni "ulofa". Tujitahidi kutunza heshima na utu wa kibinadamu kwa fikara kutawala matendo.
 
Kwa hio sisi ni Malofa

Au sio bwana?

Ahaaaaa

Poa poa
 
Wewe kweli ni mpumbavu kwa kuonyesha wazi wazi huna busara
 
Back
Top Bottom