Yaani mara 100 pesa zote alizoiba angezitumia hapa hapa nchini, kuliko kwenda kuzitupa marekani na kuleta inflation nchini, kumbuka USA huendi na Tshs., lazima ubadili iwe dollar
Bank M, tuache tu maana ashajiondokea. Ila tuache midomo midomo tunajua alipotoa hizo fedha kwa njia ya udanganyifu. Wewe unadhani kwanini JPM hapa JF anapigwa vita sana. Aliwashika pabaya mafisadi na wengi wa viongozi wa CCM na CDM ni wafisadi na hivyo wanaungana kumpiga vita aliyewakomesha. Hii ni kawaida na subiri mama amalize kipindi chake uone kila kitu kikiwekwa wazi.
Sorry mkuu ,labda sikuelewi hapa yaani kupata ile commissions of oath stamp lazima nilipie...hii sio haki kabisa,hivi vitu ni vya bure kabisa tena unaweza kuvipata police stations au post office
Huyo ni tajiri hao akina mbowe wakasome kwa pesa ya huyo mzee zitto wala mbowe hakuna aliewahi kufanya mkutano jimboni kwake huyo mzee akiwa mbunge hata lissu alikua anavuta sana posho hapo,
Usiharibu uzi kwa kuleta siasa. Uzi wa mkono lakini kwa roho yako mbaya unawajadili kina Mbowe , Zitto na Lissu. Tupunguze uchama kwenye baadhi ya mambo.
Siku za nyuma ilikuwa ni wazi kabisa kuwa CCM kilikuwa ni chama cha mafisadi,wezi wa mali ya nchi hii.Orodha ya mafisadi iliyotolewa na aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA na mwanasheria wa chama Dr Slaa na Tundu Lissu kwa mpangilio ilikoleza ufisadi wa CCM.
Mchakato wa uchaguzi mkuu ulimtoa mmoja wa waliotajwa kwenye orodha kutoka CCM na kwenda CHADEMA.Huo ulikuwa ni mwanzo wa debate,kwamba ni chama kipi cha mafisadi? Mpaka sasa makada wa CCM wanawaona CHADEMA kama mafisadi kwa uwepo wa huyo mtu na kujaribu kuhamisha magoli!!
Kuondoa mzizi wa fitina,lazima namba zitumike kwa kutumia ileile orodha ya aibu ya Dr.Slaa ambayo wanaCCM ndio wanaitumia zaidi kuwashambulia CHADEMA.
Gavana wa Benki Kuu (BoT), Marehemu, Dk. Daudi Balali (CCM)
Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM)
Basil Mramba aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo (CCM) na Waziri
Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina (CCM)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa(CCM)
Nazir Karamagi aliyewahi kuwa Mbunge(CCM)
Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM)
Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM)
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CHADEMA)
Rais mstaafu, Benjamin Mkapa(CCM)
Rais wa Sasa, Jakaya Kikwete(CCM)
Kwenye orodha ya mafisadi 11 waliotajwa na Dr Slaa pale Mwembeyanga,kwa sasa CCM inao 9(+mareh.Balali!!) ilhali CHADEMA wanaye mmoja tu.Kama hii orodha ndio kigezo na kama kweli kila aliyetajwa alikuwa fisadi,ni wazi CCM bado wana kazi kubwa ya kuhusu ufisadi nchini.
mytake:Tumuunge mkono kila anayepiga vita ufisadi wakiongozwa kwa sasa na mh.JPM bila kuwabeza wapiga kelele kama Tundulisuu
Siku za nyuma ilikuwa ni wazi kabisa kuwa CCM kilikuwa ni chama cha mafisadi,wezi wa mali ya nchi hii.Orodha ya mafisadi iliyotolewa na aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA na mwanasheria wa chama Dr Slaa na Tundu Lissu kwa mpangilio ilikoleza ufisadi wa CCM. Mchakato wa uchaguzi mkuu ulimtoa mmoja...
Nakumbuka kipindi kile wakati nasoma, bodi ya mikopo ikachelewesha kutuwekea bumu, tukaandamana hadi loan board kipindi hicho msasani. Tukishinikiza bodi ituwezeshe, kipindi hicho Nimrod alikuwa mlezi wa bodi.
Basi bwana alitoa pesa zake binafsi kuipatia bodi tukapata bumu.
Nimrod Elireheema Mkono was a Tanzanian CCM politician and Member of Parliament for Musoma Rural constituency from 2000 to 2015. He was also a practicing advocate in Mkono and advocates and former owner of Bank M.
Asante, hata mimi ni Wakili na mihuri nagonga bure na sasa niko kwenye mchakato wa kujipanga kuwasaidia zaidi Watanzania wasio na uwezo wa kuajiri wakili, kupata huduma za msaada wa kisheria.
p
Safi sana Mkuu hiyo niliona watu wakipanga foleni kwa Mzee nikasema hapa ndio faida ya Elimu na niliona alifikiri mbali sana maana kipindi hiyo board ya mikopo kwa wanafunzi inaanzishwa Mihuri ilikua ni Big ishu..
Sio fix. Tukiwa nkurumah baada ya wanafunzi kutoa malalamiko akauliza viongozi wa chuo wateje ni sh ngaoi wakataja. Akamwomba chawa wake check book akasahini hapo hapo. Akasema kufika kesho yake tutakuwa tumelipwa. Na mgomo ukaishia hapo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.