Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Salam zimefika shalis,yani ww acha tu hakuna aijuaye kesho,mwenyewe ndio alikuwa nataoka zake aende job!mpe pole sana , namuomba mungu ahusike kumponya ...pole sana mtambuzi
lol maisha haya jamani
Ameshaanza kupatiwa huduma na sasa wako njian wanampeleka Regency hospital kwa ajili ya x-ray.
Wadau
Nimetoka Regency medical centre muda mfupi uliopita. Nimeonana na ''Mzee'' Mtambuzi, bado amepumzishwa casuality room.
Nimezungumza nae anaendelea vizuri kiasi ingawa bado anasikia maumivu mgongoni pamoja mkononi. Matokeo ya x-ray yanaonyesha amevunjika mifupa ya mkono karibia na kiganja, mkono wa kulia.
Hadi ninaondoka hospitali alikuwa anasubiri kuonana na daktari bingwa wa mifupa kutoka muhimbili(MOI). Alikuwa amepata huduma ya utangulizi na kufungiwa POP huku wakimsubiri mtaalamu wa mifupa toka muhimbili, ambaye anatarajiwa kuwepo regency kuanzia saa 10-11 jioni hii.
Tuendelee kumuombea kwa Mungu, ili amjalie apone haraka. Lakini pia ningependa kutoa rai kama kuna mwanaJF yeyote ambaye ni daktari wa mifupa, ama kuna mtu anayefahamiana na daktari bingwa wa mifupa, angejitahidi kumsaidia huyu mdau. Kwakuwa inasemekana wataalamu hao ni wachache na wanapatikana kwa "appointment" kwenye hospitali binafsi na wakati mwingine hawafiki kutokana na kutingwa na majukumu mengi huko muhimbili. Sijui ni kutokana na hizi boda boda kuvunja watu viuno kila mara!? ama ni uchache wa wataalamu!
Naomba kuwasilisha.
Kwa habari za muda huu, mzee mtambuzi ameshaonana na daktari bingwa wa mifupa kutoka muhuimbili na baada ya kumcheki amesema oparation itafanyika kesho kwan kuna vipimo vingine anatakiwa kufanyiwa pamoja na maandalizi kabla ya operation hiyo,kwa hiyo ataendelea kuwepo pale regency akihudumiwa mpaka kesho,anawashukuru wote kwa ushirikiano wenu.