Mzee Mwanakijiji: Tume ya Samia inatia mashaka, haitaweza kumuhoji

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Tume iliyoundwa leo nina mashaka kama itakidhi haja. Haitaweza kumuhoji Samia Suluhu wa Makunduchi.

Mzee Mwanakijiji kasema;

1. Haiwezi kumhoji Rais kutokana na kuhusika kwake

2. Haina mwakilishi wowote (kwa sasa) toka Ofisi ya AG au DPP ili watengeneze kesi unless hawa nao wakitoa ripoti yao watatuambia wanapendekeza DPP naye aanzishe uchunguzi mwingine!!

3. Ili mchakato wake uaminike ni lazima iwe huru kweli kumhoji na kumleta mbele ya Sheria mtu au kikundi cha watu wowote waliohusika na mauaji.

Soma Pia: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia za Uchaguzi mwaka 2025

Mwisho wa kunukuu.

CCM mumeshikwa Pabaya.
 
Samuya anataka kutuaminisha mbuzi anaweza kuzidiwa uzito na ndevu zake.
 
Tume iliyoundwa leo nina mashaka kama itakidhi haja. Haitaweza kumuhoji Samia Suluhu wa Makunduchi.

Mzee Mwanakijiji kasema;

1. Haiwezi kumhoji Rais kutokana na kuhusika kwake

2. Haina mwakilishi wowote (kwa sasa) toka Ofisi ya AG au DPP ili watengeneze kesi unless hawa nao wakitoa ripoti yao watatuambia wanapendekeza DPP naye aanzishe uchunguzi mwingine!!

3. Ili mchakato wake uaminike ni lazima iwe huru kweli kumhoji na kumleta mbele ya Sheria mtu au kikundi cha watu wowote waliohusika na mauaji.

Soma Pia: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia za Uchaguzi mwaka 2025

Mwisho wa kunukuu.

CCM mumeshikwa Pabaya.
amini Mungu pekee gentleman,
kua na mashaka ni ushirikina na kuabudi masanamu 🐒
 
Tume iliyoundwa leo nina mashaka kama itakidhi haja. Haitaweza kumuhoji Samia Suluhu wa Makunduchi.

Mzee Mwanakijiji kasema;

1. Haiwezi kumhoji Rais kutokana na kuhusika kwake

2. Haina mwakilishi wowote (kwa sasa) toka Ofisi ya AG au DPP ili watengeneze kesi unless hawa nao wakitoa ripoti yao watatuambia wanapendekeza DPP naye aanzishe uchunguzi mwingine!!

3. Ili mchakato wake uaminike ni lazima iwe huru kweli kumhoji na kumleta mbele ya Sheria mtu au kikundi cha watu wowote waliohusika na mauaji.

Soma Pia: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia za Uchaguzi mwaka 2025

Mwisho wa kunukuu.

CCM mumeshikwa Pabaya.
Mambo mengine huwa tunapenda kujisahaulisha tu.

Hiyo tume imhoji yeye kama nani?

Kura milioni 31 za waTanzania kuna anayejuwa zilitoka wapi?

Kwa hiyo mara hii tujisahaulishe kwamba yupo rais madarakani kwa mujibu wa katiba; na tukubali uhalali wake na wala tusihoji uhalali wa anayoyafanya sasa hivi kama mtawala haramu!

Tutumie muda mwiiingi kujadili Haramu; na jinsi tunavyokubali uhalali wa hiyo haramu?

Samia amekuwa rais halali wa nchi hii; kwamba sasa tukubali yote anayofanya ni halali vilevile!

Kwa vipi tutegemee uhalali uzalishwe na haramu.
 
Tume haziundwi kutafuta majawabu, zinaundwa kwa malengo!
Tume ya Chande ilipita pale pale waliposema CCM na Viongozi wao na Polisi

Kuna sababu kwanini ripoti haiwekwi wazi, maswali ni mengi kuliko majibu!

Hii Tume imeundwa kuzuia hoja! watakamatwa watu 2 au 3 na askari wa mchongo na kesi kuanza mahakamani

Tutasikia kauli za kesi ipo mahakamani isiuzngumzwe. Mahakama itaangalia kalenda kwa umakini hadi 2029

Ni suala la muda tu, watu watazuiliwa kuongelea nini kilichotokea Oct 29, kwasababu shauri lipo mahakamani
 
Ni suala la muda tu, watu watazuiliwa kuongelea nini kilichotokea Oct 29, kwasababu shauri lipo mahakaman
Hiki ndio kina tafutwa.
Na ikisha fanikiwa hii hili la October 29 ndio limepita .
Watu wale walifariki wenye hatia na wasio na hatia ndio habari yao itakuwa imeishia hapo.

Kama kuna maisha mengine baada ya kufa basi acha tu tuwatakie heri huko waendako lakini ijulikane damu ile haita acha kulia ardhini dhidi ya alie imwaga.
 
Back
Top Bottom