Mzee Mwandisya na Mhongo: Msimlaumu Mwanafunzi Kupata PHD jilaumuni Ninyi (Dr and Prof) mlioacha taaluma mkakimbilia siasa kwa makundi makundi

Mzee Mwandisya na Mhongo: Msimlaumu Mwanafunzi Kupata PHD jilaumuni Ninyi (Dr and Prof) mlioacha taaluma mkakimbilia siasa kwa makundi makundi

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Siku zote Mwanafunzi anapokwenda darasani ufanya Kwa mujibu wa maelekezo ya walimu na wasimamizi wake, ufanya Kwa mujibu wa Sheria na kanuni za chuo na ufanya Kwa kuzingatia principles za vyuo husika. Mwanafunzi ajifaulishi anafaulishwa na wanaofaulisha ni wasimamizi wake.

Prof Mwandosya na Mhongo wanakuja na hoja yakuhoji uhalali wa PHd za akina Jafo Kwa kujiuliza muda walionao unatosha kumaliza PhD au Kuna tatizo? Wanakwenda mbali nakuomba wapate puplication na ziwe kwenye international standards. Niwaombe wasijifiche kwenye PhD za wanasiasa, wajikite kujiuliza wao walisukumwa na nini kuwa wanasiasa?

Utamu wa siasa ndio uliowavuta wakaacha kusimamia wanafunzi wapate PHd Kwa principles wakaanza kupata kwa michongo. Wangevumilia kubaki vyuoni may be Leo mfumo wa utoaji PhD usingevurugika.

Awamu ya Tano imeteua most of Drs and Profs kuwapeleka serikalini na kwenye siasa. Ni ukweli uliowazu kwamba vyuo vya Tanzania vimepokonywa wataalam Kwa asilimia kubwa na hivyo wanasiasa kutumia mwanya huo kupenya kuzoa PhD. Hawa waalimu waliopo vyuoni wanatamani watolewe jalalani na wanaowatoa jalalani kwa mfumo wa Tanzania ni wale wenye kupendekeza uteuzi na hao wanaopendekeza uteuzi ni akina Jafo; unadhani Kuna Dr. Au Prof atawakwamisha?

Hivyo niombe wakina Mhongo na Mwandosya waseme ukweli waache kuzunguka, Tanzania mifumo yake ya elimu inuwawa na Ninyi wanasiasa.
 
Unataka siasa iwe na watu wenye elimu ya ^daddy asiyeleta mabadiliko^ (stand-dard) seven tu!??? Hii ni tishable kwa kweli.
 
Back
Top Bottom