Mzee Mwinyi alikuwa na nafasi ya kuwa Baba wa Taifa wa pili baada ya Nyerere ila maboko yake yalimkosesha hadhi hiyo

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Ni Jambo lililo wazi kwamba Mzee Mwinyi ni mtu mwema mpole mnyenyekevu na mkarimu asie na makuu. Alipaswa kuwa na nguvu baada ya Mwalimu kuondoka kwasababu ya kigezo cha seniority list.

Lakini maboko yake yalimkosesha hadhi hiyo na kupewa Mkapa. Hebu fikiria mfano huu mdogo.

Eti yeye Mzee Mwinyi anamhusudu Magufuli na kwamaneno yake anaongoza nchi vizuri sana. Mbaya zaidi, anatamani hata tuvunje katiba ili Magufuli abaki madarakani. Kweli hii ni hadhi ya mtu kuwa na hadhi ya pili next from Nyerere?

Mkapa deserved it kwasababu alithubutu kumkemea JPM waziwazi kama tu Mwalimu alivyofanya kwa Mwinyi.
 
Nyerere alikuwa na akili ila akishindwa kutumia akili zake kipindi cha mwisho kuwa na maono juu ya uelekeo wa dunia kutoka ujamaa kwenda ubepari. Kiburi chake ndio kimesababisha hadi sasa tupo nyuma kimaendeleo.
 
Swali , jee inawezekana Marehemu Mzee Mkapa sababu ya kifo chake inaweza kuwa ni STRESS, iliyofanya immunity yake kwenda chini.
 
Muacheni mzee wa wetu atuchekeshe wajukuu zake. Aliwakuta baba/babu zetu wanavaa likundou,kaniki na viatu vya mairi ya gari,wanapanga foleni ya sukari,sabuni na mafuta ya taa,TV alikuwa nayo Nyerere tu pale Ikulu. Akatufanya tujue duniani watu wanaishije ili na sisi tuishi kama wao.
 
Jana kwenye hotuba yake nilipatwa na mshangao, alimsifia sana mkapa kwa kukuza sana uchumi, then akaja kumsifia Magufuli kwa kuipeleka nchi mbele kwamba aliitoa nchi kubaya. Hii inamaanisha yeye Mwinyi na Kikwete waliiharibu nchi au sio?
 
Hakuna rais alieitawala nchi hii kwenye wakati mgum kama mwinyi, nyerere baada ya kuminywa kila kona na mabeberu ili akubaliane na matakwa yao nyerere aliona kukubali ni kujidhalilisha hivo option akaona ni kuondoka...

Mwinyi akapewa kijiti bt nyerere ndo alikua na sauti ya mwisho, jambo hili lilileta mtafaruku baada ya mwinyi kutakiwa kuwa mtu kati baina ya nyerere na mabepari...

Watoto wa sasa mtamuona mwinyi si kitu bt mwinyi ni the great katika zama zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…