Mzee Mwinyi alikuwa na nafasi ya kuwa Baba wa Taifa wa pili baada ya Nyerere ila maboko yake yalimkosesha hadhi hiyo

Mzee Mwinyi alikuwa na nafasi ya kuwa Baba wa Taifa wa pili baada ya Nyerere ila maboko yake yalimkosesha hadhi hiyo

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Ni Jambo lililo wazi kwamba Mzee Mwinyi ni mtu mwema mpole mnyenyekevu na mkarimu asie na makuu. Alipaswa kuwa na nguvu baada ya Mwalimu kuondoka kwasababu ya kigezo cha seniority list.

Lakini maboko yake yalimkosesha hadhi hiyo na kupewa Mkapa. Hebu fikiria mfano huu mdogo.

Eti yeye Mzee Mwinyi anamhusudu Magufuli na kwamaneno yake anaongoza nchi vizuri sana. Mbaya zaidi, anatamani hata tuvunje katiba ili Magufuli abaki madarakani. Kweli hii ni hadhi ya mtu kuwa na hadhi ya pili next from Nyerere?

Mkapa deserved it kwasababu alithubutu kumkemea JPM waziwazi kama tu Mwalimu alivyofanya kwa Mwinyi.
 
Swali , jee inawezekana Marehemu Mzee Mkapa sababu ya kifo chake inaweza kuwa ni STRESS, iliyofanya immunity yake kwenda chini.
 
Muacheni mzee wa wetu atuchekeshe wajukuu zake. Aliwakuta baba/babu zetu wanavaa likundou,kaniki na viatu vya mairi ya gari,wanapanga foleni ya sukari,sabuni na mafuta ya taa,TV alikuwa nayo Nyerere tu pale Ikulu. Akatufanya tujue duniani watu wanaishije ili na sisi tuishi kama wao.
 
Hakuna rais alieitawala nchi hii kwenye wakati mgum kama mwinyi, nyerere baada ya kuminywa kila kona na mabeberu ili akubaliane na matakwa yao nyerere aliona kukubali ni kujidhalilisha hivo option akaona ni kuondoka...

Mwinyi akapewa kijiti bt nyerere ndo alikua na sauti ya mwisho, jambo hili lilileta mtafaruku baada ya mwinyi kutakiwa kuwa mtu kati baina ya nyerere na mabepari...

Watoto wa sasa mtamuona mwinyi si kitu bt mwinyi ni the great katika zama zake.
 
Back
Top Bottom