Kutokana na yaliyo andikwa kwenye Kitabu chake Mzee Mwinhi, inaomekana katika Marais walio pata taabu sana ktk uongozi kuanzia alipo teuliwa kuwa waziri basi ni Huyu Mzee wetu Mwinyi.
Pamoja na kuwa mwadilifu na mtiifu lkn bado alichukiwa sana na alifanyiwa fitina za hali ya juu mpaka akajiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani lkn badae alirudishwa tena ulingoni lkn bado alipigwa fitina na kubabaishwa kuwa eti ni mdini anapendelea waislamu n.k, ama hakika walimyumbisha sana lkn kutokana na uadilifu wake na ucha Mungu alibakia kuwa Imara na Hatimaye Mungu alimsaidia.
Hakika kuna mafunzo mengi sana ya kujifunza ktk kipindi cha utawala wake.
tujirekebishe kwa wale wote wenye chuki binafsi na uchu wa vyeo, tuache tabia za kuiguruga nchi yetu, tuwe wazalendo wa kweli.
tuache kutafuta vyeo kwa uchawi au kwa kuhadaa/unafiki kwani cheo/uongozi hutoka kwa Mungu.
Tusibaguane wala kuchukiana au kufanyiana fitina kisa ni mkristo au mwislamu, sisi sote walio na dini na wasio na dini tunaunganishwa na MAMA Tanzania.
tusibaguane kwa makabila au ukanda kwani sisi sote ni watanzania, hivyo yatupasa kudumisha Amani, Upendo na Utulivu kwa masilahi ya nchi yetu.