TANZIA Mzee Nicodemus Manase Banduka afariki dunia hospitali ya Mloganzila

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Wapendwa! Kwa masikitiko makubwa, Familia ya Banduka inasikitika kuwatangazia kifo cha Mhe. Nicodemus Manase Banduka kilichotokea ghafla jana, Ijumaa jioni, wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mloganzila.

Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwake Kibaha - kwa Matias. Taarifa kamili ya mazishi itatolewa baada ya mipango kukamilika.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amen

Pia soma > Yupo wapi kada maarufu wa CCM Nicodemus Banduka?

Nicodemus M. Banduka alikuwa mwanasiasa na kiongozi mashuhuri nchini Tanzania. Alishika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuanzia Juni 1998 hadi Februari 2003.

Kabla ya hapo, alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera.

Shule ya sekondari inayoitwa Nicodemus Banduka Secondary School ipo, ikionesha heshima kwa mchango wake katika jamii.


Mzee Nocodemus Banduka wa tatu kutoka kushoto waliosimama akiwa na Wajumbe 18 kati ya 20 wa Tume ya watu 20 iliyotayarisha Katiba ya CCM​
 
Yani mlienda mloganzila ,bora angebaki home tu
 
Moja ya majina maarufu wakati huo yaliyotawala RTD na Redio one apumzike kwa amani!
 
Tafuta historia yake vizuri, mkuu
  1. Aliwahi kuwa RC Iringa
  2. Aliwahi kuwa RC nadhani ni Mtwara au Lindi
  3. Nadhani alidunguliwa kuna kauli tete aliitoa somewhere ndipo akapotea kwenye siasa
 
Tafuta historia yake vizuri, mkuu
  1. Aliwahi kuwa RC Iringa
  2. Aliwahi kuwa RC nadhani ni Mtwara au Lindi
  3. Nadhani alidunguliwa kuna kauli tete aliitoa somewhere ndipo akapotea kwenye siasa
Pwani pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…