TANZIA Mzee Nicodemus Manase Banduka afariki dunia hospitali ya Mloganzila

Radio tudanganyane daresalaam , nilimsikia sana ...alikuwa mzima hata Dr creluu angekuwa mzima
 
Naona Wazee waadilifu wa Enzi za Mwalimu wanaondoka!
Mmh.

Hatutakiwi kumsema vibaya Marehemu, lakini hili la uadilifu sio kweli!

Mzee alikuwa akiona kiwanja/ardhi anawehuka!

Aliwahi kuuza msitu wa kupanda pale Maili Moja mkoani! Kasheshe lake ndilo lililomaliza mbio zake za kisiasa!

BWT, huyu hakufikisha miaka 100 kweli? Maana alikuwa kizazi cha Daudi Mwakawago!
 
Wapendwa! Kwa masikitiko makubwa, Familia ya Banduka inasikitika kuwatangazia kifo cha Mhe. Nicodemus Manase Banduka kilichotokea ghafla jana, Ijumaa jioni, wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mloganzila.

Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwake Kibaha - kwa Matias. Taarifa kamili ya mazishi itatolewa baada ya mipango kukamilika.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amen

Pia soma > Yupo wapi kada maarufu wa CCM Nicodemus Banduka?

Nicodemus M. Banduka alikuwa mwanasiasa na kiongozi mashuhuri nchini Tanzania. Alishika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuanzia Juni 1998 hadi Februari 2003.

Kabla ya hapo, alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera.

Shule ya sekondari inayoitwa Nicodemus Banduka Secondary School ipo, ikionesha heshima kwa mchango wake katika jamii.

View attachment 3229192
Mzee Nocodemus Banduka wa tatu kutoka kushoto waliosimama akiwa na Wajumbe 18 kati ya 20 wa Tume ya watu 20 iliyotayarisha Katiba ya CCM​
Banduka ni jina nililolisikia sana miaka ya zamani, apumzike kwa amani.
 
Mmh.

Hatutakiwi kumsema vibaya Marehemu, lakini hili la uadilifu sio kweli!

Mzee alikuwa akiona kiwanja/ardhi anawehuka!

Aliwahi kuuza msitu wa kupanda pale Maili Moja mkoani! Kasheshe lake ndilo lililomaliza mbio zake za kisiasa!

BWT, huyu hakufikisha miaka 100 kweli? Maana alikuwa kizazi cha Daudi Mwakawago!
Aise! Sikulijua hilo kwamba alikuwa na makandokando kama hayo.
 
Wapendwa! Kwa masikitiko makubwa, Familia ya Banduka inasikitika kuwatangazia kifo cha Mhe. Nicodemus Manase Banduka kilichotokea ghafla jana, Ijumaa jioni, wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mloganzila.

Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwake Kibaha - kwa Matias. Taarifa kamili ya mazishi itatolewa baada ya mipango kukamilika.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amen

Pia soma > Yupo wapi kada maarufu wa CCM Nicodemus Banduka?

Nicodemus M. Banduka alikuwa mwanasiasa na kiongozi mashuhuri nchini Tanzania. Alishika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuanzia Juni 1998 hadi Februari 2003.

Kabla ya hapo, alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera.

Shule ya sekondari inayoitwa Nicodemus Banduka Secondary School ipo, ikionesha heshima kwa mchango wake katika jamii.

View attachment 3229192
Mzee Nocodemus Banduka wa tatu kutoka kushoto waliosimama akiwa na Wajumbe 18 kati ya 20 wa Tume ya watu 20 iliyotayarisha Katiba ya CCM​
Shinysnga Pia. Alishawahi kuwa RC
 
Tafuta historia yake vizuri, mkuu
  1. Aliwahi kuwa RC Iringa
  2. Aliwahi kuwa RC nadhani ni Mtwara au Lindi
  3. Nadhani alidunguliwa kuna kauli tete aliitoa somewhere ndipo akapotea kwenye siasa
Ilikuwa Lindi, kule Kuna eneo mpaka Leo kinaitwa banduka. Aliwatoa watu sehemu hatarishi na kuwahamishia huko na hatimaye kupata jina hilo.
 
Stephen Mashishanga yupo anaishi Kihonda Morogoro ni mtu tofauti na huyu Nicodemus Banduka aliyefariki
Wapi nimeandika Stephen Mashishanga amefariki ebu weka hiko kipande ulichonukuu.
Uwe unasoma vizuri kilichoandikwa kabla ya kukosoa.
 
Back
Top Bottom