TANZIA Mzee Nicodemus Manase Banduka afariki dunia hospitali ya Mloganzila

Angalia wapi nimeandika Mashishanga amekufa
 
Una onekana wa kitambo sana mkuu?
 
Pole sana kwa Familia yake. Mzee Banduka alikuwa RC wangu Mkoa wa Iringa. Ni mtu aliesimamia maendeleo na miradi kwa karibu katika jukumulu lake la kila siku.
 
Mzee Banduka alikuwa rafiki yangu Sana zama hizo.

Wakati wa kuanzishwa Kwa Wilaya ya Mkuranga, nilipata bahati ya kwenda kule na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Kapteni... alitoa fursa ya kupata Ardhi.

Kwa kweli banduka alikuwa na pande tatu. Mbabe, mtu wa kuthubutu na mjanjajanja wa mjini.

Mara ya mwisho nilikutana naye pale kurasini kwenye ofisi yake. Jamaa alikuwa mwanasiasa hasa.

Safari yake ya kisiasa ilimalizwa siyo kwa kutolewa ukuu wa Mkoa wa Pwani, bali kwa kushindwa kwake kwenye kura za maoni Jimbo la Mwanga na Profesa Jumanne Maghembe.

Alikuwa Mkuu wa mkoa mwenye ushawishi na uwezo mkubwa sana wa kusukuma maendeleo lakini hapo hapo na maslahi yake lazima yazingatiwe!

Pumzika Kwa amani Mzee Banduka!
 
RIP Mzee Banduka. Mzee amekuwa RC wangu nikiwa Mkoa wa Iringa. Huyu Mzee ni mhamasishaji mkubwa wa shughuli za maendeleo. Alikuwa akija kwenye Wilaya yako kazi anaianza asubuhi mpaka saa 12 jioni bila kiuchoka. Mzee alikuwa ni adui wa mtu anayeisema CCM vibaya.
 
Hakuna hospitali inayotoa huduma nzuri inayokaribiana na mkoa wa pwani kama Mloganzila. Nilifika pale mwaka jana huduma zao ni nzuri sana. Kwa uzee wake na maradhi utaisingizia tu hospitali.
Sawa kabisa. Floor ya 9 wadi za private wako vizuri mnoooo kuliko hata VIP. Msimamizi wa hili eneo nakupa maua yako. Wako sharp unapiga simu mara moja wauguzi wa zamu wanakuja, huduma safi. Watu wanasikia tu ya kuambiwa wanayabeba juujuu.
 
Yule mzee wa Msoga ni mdogo wake na yule malaika aliyetupwa chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…