mzushi
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 3,094
- 4,252
Yule Mzee Mkongwe na Gwiji la siasa l za Tanzania Mzee Sozigwa amefariki Dunia. Sozigwa alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Mtoto wa Mzee Sozigwa, Mchungaji Moses Sozigwa alisema tatizo la kwanza lililokuwa likimsumbua baba yao ni kupoteza kumbukumbu. Baadaye ilikuja kubainika ana tatizo la moyo, madaktari walisema moyo wake umekuwa mkubwa.
Paul Sozigwa ndiye Katibu wa kwanza wa Rais (IKULU-HABARI).
Mbali na kuwa katibu wa Ikulu, nyadhifa nyingine alizoshika ni Mkurugenzi wa kwanza wa Redio Tanzania(RTD), DO Wilaya ya Kisarawe katika serikali ya kikoloni na katibu Mkuu, Wizara ya Habari na Utangazaji.
Vilevile alishawahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya CCM zikiwemo za Mjumbe wa NEC, CC na M/kiti Tume ya Taifa ya Udhibiti na Nidhamu na M/kiti wa CCM mkoa wa Pwani.
Kutoka kushoto: Habib Halala, Paul Sozigwa, Mwalimu J.K. Nyerere, Brig. Hashim Mbita na Benjamin Mkapa mwaka 1985.
Rest in peace Mzee wetu
=======
Byendangwero Said
Kwa maoni yangu, sifa kuu inayompambanua mzee Sozigwa katika maisha yake yote ya siasa hapa alihubiri kile alichokiamini.
Katika miaka ya sabini, akiwa mkugenzi wa Redio Tanzania, alianzisha kipindi redioni kilichojulikana kwa jina la; "Mikingamo" katika mojawapo ya vipindi vyake, alisema kuwa ubepali ulikuwa unyama. Na kweli, mzee Sozigwa hata baada ya kusambaratika kwa siasa ya ujamaa aliendelea kuishi kama mjamaa.
Nakumbuka mwishoni mwa miaka ya 1990, akiwa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM alikuja Bukoba kwa shughuli za kikazi; mh. Kimiti wakati huo akiwa mkuu wa mkoa (k) alimtumia gari ya kwenda kumpokea melini; dereva alipomtafuta katika vyumba vyote vya daraja la kwanza hasimpate akarudi na kuripoti kwa bosi wake kuwa mzee hakuja; kumbe yeye alikuwa amekuja kwenye daraja ya tatu. Baadaye alimpigia mh. Kimiti kumjulisha kuwa alikuwa tayari amewasili na amefikia coffee Tree Inn.
Baadaye wakati tukinywa chai pamoja yule dereva alikuja kuomba msamaha huku akijitetea kuwa alikuwa amepita kwenye vyumba vyote vya daraja la kwanza lakini hakumuona.
Kitu alichomjibu mzee yule ni;"wewe nani alikwambia kuwa chama kina fedha za kupoteza kwa kusafirisha watu daraja la kwanza." Na aliyasema hayo miaka mingi baada ya azimio la Zanzibar kuiweka CCM katika njia ya ubepari.
Wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa urais kupitia CCM wakati wa uchaguzi mkuu wa 2005, sekretariati ya CCM chini ya Philip Mangula iliazimia kuondoa mgombea yeyote atakakayebainika kutoa rushwa kwenye kinyanganyiro.
Mzee Sozingwa akiwa anasimamia idara ya nidhamu katika sekretariati hiyo akalivalia njuga azimio hilo, Nakumbuka wakati Kikwete alipokuja Bukoba kusaka wadhamini, mzee Sozigwa alikuwepo akifuatilia nyendo zote zilizoashiria kuwepo kwa mazingira ya rushwa.
Inasemekana wakati wa kujadili wagombea urais katika kamati kuu taarifa aliyokuwa ameiandaa ilitupwa kapuni, na hatimaye sekretarati yote ilifungiwa virago baada ya JK kuukwea wenyekiti wa CCM.

Huyu ndiye aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga(nadhani na M/Kiti wakati wa kofia mbili) kipindi ambacho watu walifungiwa kwenye kàchumba kadogo na wakafa kwa kukosa hewa.
Ikabidi yeye, Waziri wa mambo ya ndani(Rais mstaafu, Mzee Mwinyi), afisa usalama wa wilaya(Lyatonga Mrema), IGP (Philemon Mgaya) na wengine wakajiuzulu nyadhifa zao.
Philemon Mgaya ndiye IGP aliyekaa kwenye nafasi hiyo kwa muda mfupi sana baada ya kukumbwa na kadhia hiyo.