TANZIA Mzee Paul Sozigwa, aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Mwalimu Julius Nyerere afariki Dunia

TANZIA Mzee Paul Sozigwa, aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Mwalimu Julius Nyerere afariki Dunia

Jamani kifo ni Kibaya, Hivi Ingekuwa Mtu akifa ni kama ameenda safarini, Siku Moja isikike Mwalimu Nyerere amerudi Butiama anatarajia Kuja Dar Kuzungumza na Waandishi naye Watamshikia Bastola au Watahama nchi?
 
Tufafanulie alimpigiaje ,simu wakati miaka kulikuwa hakuna simu za mkononi?

Mwishoni wa miaka ya 90 simu za mikononi zilikuwepo ndugu yangu. 1994 nilikuwa natumia mobitel MOTOROLA japo analogue code 0811, Tritel pia ilikuwepo code 0812, hii ilikuwa Digital zaidi wakitumia Siemens.
 
Huyu ndiye aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga(nadhani na M/Kiti wakati wa kofia mbili) kipindi ambacho watu walifungiwa kwenye kàchumba kadogo na wakafa kwa kukosa hewa. Ikabidi yeye, waziri wa mambo ya ndani(Rais mstaafu, Mzee Mwinyi), afisa usalama wa wilaya(Lyatonga Mrema), Igp (Philemon Mgaya) na wengine wakajiuzulu nyadhifa zao. Philemon Mgaya ndiye IGP aliyekaa kwenye nafasi hiyo kwa muda mfupj sana baada ya kukumbwa na kadhia hiyo.
Hivi una hakika na hiyo data kwamba mzee Sozigwa alikuwa DC wa wilaya ya Shinyanga wakati wa kashfa ile ya wachawi? maana wakati huo mimi nilikuwepo mkoa wa Shinyanga. nakumbuka mkuu wa mkoa wa Shinyanga alikuwa Mustafa Songambele. sikumbuki kuhusu "mkuu wa wilaya ya Shinyanga". sijawahi kusikia mahali pengine akitajwa kushiriki kashfa hiyo ya wachawi, ila muda mfupi baada ya kipindi hicho nakumbuka alitutembelea Shuleni kama Mkurugenzi wa RTD na pia mjumbe wa Kamati Kuu ya Tanu. sasa nashangaa kama alikuwa kwenye hiyo kashfa, maana wote waliokuwa na vyeo kipindi hicho walijiuzulu kabla ya kuibuka tena kitambo kirefu kidogo baada ya hapo
 
RIP Mzee Paul Sozigwa.
P.
Serious, mzee Mayalla? nilitarajia angalau ungemtendea haki, maana wewe wakati huo ulikuwa unafuatilia mambo kwa karibu. nilitarajia ungewahabarisha vijana kuhusu gwiji huyu, ambaye kipindi alipokuwa Mkurugenzi wa RTD, alikuwa anatumia kipindi cha MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI, kuleta ujumbe mzito ambao ulilenga kueleza msimamo wa Serikali. Nakumbuka kipindi fulani aliibuka na neno NYANG'AU wakati kulikuwa na ugomvi kati ya Kenya na Tanzania, kipindi cha "kashfa" ya KENATCO.
 
2005 alikuwa mwenyekiti wa kamati ya maadili ya CCM iliyopitia sifa za waliotaka kuogombea kwa kupitia CCM.

Kwa maoni ya kamati yake Kikwete alikuwa hafai kuwa rais.
Kamati ilifanya kazi iliyotukuka,kwa kuyatupa kapuni maoni matokeo yake sote tunayajua,ni kama vile usemi wa asiyesikia la mkuu.....
 
Mzaramo wa kwanza kupata degree UDSM-this is a fact
Huyu mzee alikuwa mzee simple sana,pamoja na kuwa na vyeo lukuki na vikubwa ukimkuta kule Kigamboni kwenye shughuli za kwenye misiba ulikuwa huwezi kujua kuwa huyu mzee ndio washika''hatamu'' na alikuwa anaimba kwaya akiwa na biblia yake mkononi,huku kavaa sandals za kiwanda cha Bora,RIP Mzee Sozigwa,wazee wenzako waliobaki wamebaki kukumbatia mafisadi na wanapelekeshwa na mafisadi kama ndio wanajua utamu wa pesa uzeeni,kutwa majukwani wakizungusha mikono !
 
Back
Top Bottom