Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee Sozigwa alielewa, aliamini na kutekeleza fikra za Mwalimu. Walipoamua kubadilisha gia ingekuwa vigumu kuendelea naye hivyo akatupwa kama tambaa bovu. Siye wa kwanza kutendewa hayo katika siasa. Historia itatukumbusha vizazi vijavyo.Yes Alikuwa Mkurugenzi and press secretary of the president. Alishika nafasi nzuri tu. Lakini hakufanya transition nzuri pale mfumo wa vyama vingi ulipoingia. Alibaki kwenye chama na hakuwa na cheo cha kuchaguliwa kama vile ubunge. Hivyo chamani walipomtosa hakuwa mshiko tena.
Huyu Mzee àlikuwa ni mtu ambaye hakuwahi kuwa mnafiki kwa anacho kiamini! Mara zote alikuwa anasimamia kile anacho kiamini! Kutofautiana mitizamo ni kitu cha kawaida sana katika maisha,mbona hata katika ngazi zetu za kifamilia watoto wanaweza Kutofautiana na Baba au Mama mzazi na maisha yakaendelea! Kuchukiwa kwa mtizamo na fikra binafsi na kumhukumu hii sio haki pia sio sawa haki mbele ya mwenyezi MUNGU! Kanamambo mema huyu Mzee amelifanyia taifa na CCM Jee pia hayo mema waliyasahau? Huyu Mzee familia yake ilikuwa inalalamika muda mrefu kwamba walio na madaraka hawajataka kumsaidia Mzee Sozigwa kimatibabu!anyway sijui sana mambo hayo na ukweli wake pia sio hoja yangu humu jamvini! Ila kama ni kweli?Mzee Sozigwa ameshafariki!jee wao waliomchukia na kumtelekeza kimatibabu kama kweli wapo! Jee wataishi milele??? Hapa uliwenguni sote tunapita tuu tujitahidi sana kuwa wema kwa viumbe vyote vya MWENYEZI MUNGU ili tupate kuwa na mwisho mwema INSHAALAH!R.I.P mzee Paul Sozigwa tutakukumbuka mzee wetu, haya ndio maisha ya watu wasio na shukrani, tenda wema nenda zako...
Hawa Wazee walikuwa na Matumizi Mbaya ya Fedha na wakifulia wanasingizia Uadilifu,
Uadilifu sio lazima uhusishwe na Ukosefu wa Maarifa ya kupanga Mipango yako imara ya kiuchumi kabla ya kustaafu!
Walikuwa wanalipwa Mishahara na Marupurupu kadhaa Kama Watumishi wengine wengi tu!
Kama Sie Watumishi wa kawaida tu hatukuwa Wezi na hata tungetaka kuwa Wezi hatukuwa na cha kuiba lakin mbona tuliweza kujipanga vyema kabla ya kustaafu?
Hawa Wazee waliendekeza Nyumba zisizo rasmi na ndipo walipomalizia Fedha zote!
Alichanganyikiwa baada ya Mali zote kuporwa na Mpango wake wa kando ikiwemo Nyumba lakin Wasiojua wanahusisha na Siasa!
Huyu Alistaafu Muda mrefu kabla hata ya kuingia Jk Ikulu, kazi alizokuwa anafanya baada ya kustaafu kwake ni za Kisiasa sio kiutumishi ambazo hazina Pension!
![]()
Katika picha hii mtu aliye hai ni Rais Benjamin Mkapa tu! Wengine hao wengine wametutoka nakumbuka Habibu Harahara alikufa vibaya kwa kukatwa na panga la helikopta waliokuwa wamepanda yeye na Mwalimu Nyerere. Alikatwa na panga hilo kwa bahati mbaya nafikiri ilikuwa kama siyo Mtwara ni Lindi. Msiba wake ulisikitisha sana.
Yule Mzee Mkongwe na Gwiji la siasa l za Tanzania Mzee Sozigwa amefariki Dunia. Sozigwa alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Mtoto wa Mzee Sozigwa, Mchungaji Moses Sozigwa alisema tatizo la kwanza lililokuwa likimsumbua baba yao ni kupoteza kumbukumbu. Baadaye ilikuja kubainika ana tatizo la moyo, madaktari walisema moyo wake umekuwa mkubwa.
View attachment 508065
Paul Sozigwa ndiye Katibu wa kwanza wa Rais (IKULU-HABARI).
Mbali na kuwa katibu wa Ikulu, nyadhifa nyingine alizoshika ni Mkurugenzi wa kwanza wa Redio Tanzania(RTD), DO Wilaya ya Kisarawe katika serikali ya kikoloni na katibu Mkuu, Wizara ya Habari na Utangazaji.
Vilevile alishawahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya CCM zikiwemo za Mjumbe wa NEC, CC na M/kiti Tume ya Taifa ya Udhibiti na Nidhamu na M/kiti wa CCM mkoa wa Pwani.
View attachment 508066
Kutoka kushoto: Habib Halala, Paul Sozigwa, Mwalimu J.K. Nyerere, Brig. Hashim Mbita na Benjamin Mkapa mwaka 1985.
Rest in peace Mzee wetu
=======
Byendangwero Said
View attachment 508072
Kwa maoni yangu, sifa kuu inayompambanua mzee Sozigwa katika maisha yake yote ya siasa hapa alihubiri kile alichokiamini.
Katika miaka ya sabini, akiwa mkugenzi wa Redio Tanzania, alianzisha kipindi redioni kilichojulikana kwa jina la; "Mikingamo" katika mojawapo ya vipindi vyake, alisema kuwa ubepali ulikuwa unyama. Na kweli, mzee Sozigwa hata baada ya kusambaratika kwa siasa ya ujamaa aliendelea kuishi kama mjamaa.
Nakumbuka mwishoni mwa miaka ya 1990, akiwa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM alikuja Bukoba kwa shughuli za kikazi; mh. Kimiti wakati huo akiwa mkuu wa mkoa (k) alimtumia gari ya kwenda kumpokea melini; dereva alipomtafuta katika vyumba vyote vya daraja la kwanza hasimpate akarudi na kuripoti kwa bosi wake kuwa mzee hakuja; kumbe yeye alikuwa amekuja kwenye daraja ya tatu. Baadaye alimpigia mh. Kimiti kumjulisha kuwa alikuwa tayari amewasili na amefikia coffee Tree Inn.
Baadaye wakati tukinywa chai pamoja yule dereva alikuja kuomba msamaha huku akijitetea kuwa alikuwa amepita kwenye vyumba vyote vya daraja la kwanza lakini hakumuona.
Kitu alichomjibu mzee yule ni;"wewe nani alikwambia kuwa chama kina fedha za kupoteza kwa kusafirisha watu daraja la kwanza." Na aliyasema hayo miaka mingi baada ya azimio la Zanzibar kuiweka CCM katika njia ya ubepari.
View attachment 508073
Wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa urais kupitia CCM wakati wa uchaguzi mkuu wa 2005, sekretariati ya CCM chini ya Philip Mangula iliazimia kuondoa mgombea yeyote atakakayebainika kutoa rushwa kwenye kinyanganyiro.
Mzee Sozingwa akiwa anasimamia idara ya nidhamu katika sekretariati hiyo akalivalia njuga azimio hilo, Nakumbuka wakati Kikwete alipokuja Bukoba kusaka wadhamini, mzee Sozigwa alikuwepo akifuatilia nyendo zote zilizoashiria kuwepo kwa mazingira ya rushwa.
Inasemekana wakati wa kujadili wagombea urais katika kamati kuu taarifa aliyokuwa ameiandaa ilitupwa kapuni, na hatimaye sekretarati yote ilifungiwa virago baada ya JK kuukwea wenyekiti wa CCM.
Enzi hizo TP&TC.Kuna mambo ambayo ukiyafikiria kisasa unahisi watu waliishije zamani ila kwa hili Mzee alikua hotelini kulikua na simu landline na kimiti alikua ofisini kuna simu TTCL
View attachment 508047
Rest in peace Mzee Paul Sozigwa
Paul Sozigwa aliasisi vipi ujamaa?RIP Mzee Sozigwa
Waasisi wa Ujamaa waliosikika sana.
Nakumbuka vipindi vya RTD,kama Mazungumzo baada ya habari,Imeandikwa na Mikingamo.
Wakati Kenya inafunga mpaka wake na Tanzania nayo RTD haikuwa nyuma kuwaita Manyangau.
Asante mkuu kwa masahihisho nilisahau kuwa ulikuwa wakati wa Rais MwinyiAlikuwa na rais Mwinyi, si Nyerere. Walikwenda kuangalia hali kusini baada ya mafuriko.