Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna mambo ambayo ukiyafikiria kisasa unahisi watu waliishije zamani ila kwa hili Mzee alikua hotelini kulikua na simu landline na kimiti alikua ofisini kuna simu TTCLTufafanulie alimpigiaje ,simu wakati miaka kulikuwa hakuna simu za mkononi?
Mikingamo RTD kipindi nakumbuka kilikua kinatangazwa ma Seleman HeggaYule Mzee Mkongwe na Gwiji la siasa l za Tanzania Mzee Sozigwa amefariki Dunia.
View attachment 508065
Paul Sozigwa ndiye Katibu wa kwanza wa Rais (IKULU-HABARI).
Mbali na kuwa katibu wa Ikulu, nyadhifa nyingine alizoshika ni Mkurugenzi wa kwanza wa Redio Tanzania(RTD), DO Wilaya ya Kisarawe katika serikali ya kikoloni na katibu Mkuu, Wizara ya Habari na Utangazaji.
Vilevile alishawahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya CCM zikiwemo za Mjumbe wa NEC, CC na M/kiti Tume ya Taifa ya Udhibiti na Nidhamu na M/kiti wa CCM mkoa wa Pwani.
View attachment 508066
Kutoka kushoto: Habib Halala, Paul Sozigwa, Mwalimu J.K. Nyerere, Brig. Hashim Mbita na Benjamin Mkapa mwaka 1985.
Rest in peace Mzee wetu
=======
Byendangwero Said
Kwa maoni yangu, sifa kuu inayompambanua mzee Sozigwa katika maisha yake yote ya siasa hapa alihubiri kile alichokiamini.
Katika miaka ya sabini, akiwa mkugenzi wa Redio Tanzania, alianzisha kipindi redioni kilichojulikana kwa jina la; "Mikingamo" katika mojawapo ya vipindi vyake, alisema kuwa ubepali ulikuwa unyama. Na kweli, mzee Sozigwa hata baada ya kusambaratika kwa siasa ya ujamaa aliendelea kuishi kama mjamaa.
Nakumbuka mwishoni mwa miaka ya 1990, akiwa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM alikuja Bukoba kwa shughuli za kikazi; mh. Kimiti wakati huo akiwa mkuu wa mkoa (k) alimtumia gari ya kwenda kumpokea melini; dereva alipomtafuta katika vyumba vyote vya daraja la kwanza hasimpate akarudi na kuripoti kwa bosi wake kuwa mzee hakuja; kumbe yeye alikuwa amekuja kwenye daraja ya tatu. Baadaye alimpigia mh. Kimiti kumjulisha kuwa alikuwa tayari amewasili na amefikia coffee Tree Inn.
Baadaye wakati tukinywa chai pamoja yule dereva alikuja kuomba msamaha huku akijitetea kuwa alikuwa amepita kwenye vyumba vyote vya daraja la kwanza lakini hakumuona.
Kitu alichomjibu mzee yule ni;"wewe nani alikwambia kuwa chama kina fedha za kupoteza kwa kusafirisha watu daraja la kwanza." Na aliyasema hayo miaka mingi baada ya azimio la Zanzibar kuiweka CCM katika njia ya ubepari.
Wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa urais kupitia CCM wakati wa uchaguzi mkuu wa 2005, sekretariati ya CCM chini ya Philip Mangula iliazimia kuondoa mgombea yeyote atakakayebainika kutoa rushwa kwenye kinyanganyiro.
Mzee Sozingwa akiwa anasimamia idara ya nidhamu katika sekretariati hiyo akalivalia njuga azimio hilo, Nakumbuka wakati Kikwete alipokuja Bukoba kusaka wadhamini, mzee Sozigwa alikuwepo akifuatilia nyendo zote zilizoashiria kuwepo kwa mazingira ya rushwa.
Inasemekana wakati wa kujadili wagombea urais katika kamati kuu taarifa aliyokuwa ameiandaa ilitupwa kapuni, na hatimaye sekretarati yote ilifungiwa virago baada ya JK kuukwea wenyekiti wa CCM.
Huyu alikuwa ni mmoja wa watu wa karibu sana na Baba wa Taifa Mwl Nyerere.Kwani alikuwa na kazi gani?na alistaafu lini ?
Hi inji we isikie tu kuna visasi vya halo ya juu Sana watu wanafanyiwa had I unakaa huwezi amini, unakuwa na thamani pale unapokuwa ofisini tu, ukistaafu tu ndo utaona rangi za binadamu, wengine uliowasaidia kabisa wakikuona kwenye korido wapo tayari kukimbia ofisiAlipew mafao yake?
If my memory serves me well he was Nyerere's press secretary.Wacha kuweka habari za kizushi wewe! Mwandishi wa Rais na Katibu wa Rais ni vitu viwili tofauti. Katibu wa Rais alikuwa Mzee Kasori na pengine Mzee Butiku!
Umejiunga jana JF? Au umezaliwa jana?Alipewa nenda kagawiwe na wew wabongo mnapenda kujua ya wenzenu
Mkuu,umesoma huu uzi kweli?,maana maswali yako yanatia shakaKwani alikuwa na kazi gani?na alistaafu lini ?
Huyu ni nani ?Ndo namsikia Leo aisee.RIP mzee.
Ndio mwenyewe tena ndio mwanzo wakutetereka kwa afya yake kwa kuzungushwa kulipwa .Sijui ataa kama alilipwa kweli ??Kuna wakati alikuwa anayasotea nafikiri..
Sio huyu kweli??