TANZIA Mzee Paul Sozigwa, aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Mwalimu Julius Nyerere afariki Dunia

TANZIA Mzee Paul Sozigwa, aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Mwalimu Julius Nyerere afariki Dunia

Mungu akupumzishe kwa amani na tunashukuru sn kwa mchango wako ktk Taifa letu. Unapaswa kupewa heshima ya nchi ktk mazishi yako. Daima tutakukumbuka japo uliyo yasimamia na kuyaamin sina hakika kama viongozi waliopo watayaenzi.
 
Huyu ni nani ?Ndo namsikia Leo aisee.RIP mzee.
Huyu ndiye aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga(nadhani na M/Kiti wakati wa kofia mbili) kipindi ambacho watu walifungiwa kwenye kàchumba kadogo na wakafa kwa kukosa hewa. Ikabidi yeye, waziri wa mambo ya ndani(Rais mstaafu, Mzee Mwinyi), afisa usalama wa wilaya(Lyatonga Mrema), Igp (Philemon Mgaya) na wengine wakajiuzulu nyadhifa zao. Philemon Mgaya ndiye IGP aliyekaa kwenye nafasi hiyo kwa muda mfupj sana baada ya kukumbwa na kadhia hiyo.
 
Inasemekana wakati wa kujadili wagombea urais katika kamati kuu taarifa aliyokuwa ameiandaa ilitupwa kapuni, na hatimaye sekretarati yote ilifungiwa virago baada ya JK kuukwea wenyekiti wa CCM.
RIP mzee wa kusimamia nidhamu. Aliyeitupa taarifa hiyo ni mwenyekiti wa CCM wa wakati huo baada ya kutishwa na vyombo vya intelijensia kuwa mgombea mmojawapo maarufu angehamia upinzani kama jina lake lingeondolewa. Pathetic!!
 
Pumzikakwa Amani Mzee Paul Sozigwa. Ulikuwa na simamo thabiti kutetea na kulinda ukweli, na ni ukweli huo uliogharimu maisha yako ya uzeeni. Uliishi kwa taabu uzeeni kana kwamba hukutumikia Chama na serikali ya nchi hii kwa uadilifu mkubwa. Hakika Mwenyezi Mungu atakulipa kwa mateso uliyopata uzeeni wakati ukimalizia maisha yako hapa duniani.
 
Daah!! Maisha haya we acha tu!! Fanya ufanyalo lakini kwa Mola wako ni marejeo. Masikini mzee wetu sasa anakwenda kukutana na Mola wake ambaye anachohitaji kutoka kwa mzee wetu ni amali zake tu. Mola hataangalia kama yeye alikuwa nani kwenye siasa za Tanzania. Mola wetu tujaalie mwisho mwema na tujaalie tufanye yale tu yatakayokupendeza wewe hata kama binadamu wenzetu watachukia. Amen.
 
Mwanasiasa maarufu mbona mm Ndio namsikia Leo labda kwakuwa mm Sio mwanasiasa

Kama umezaliwa miaka ya mwishoni mwa 90 au hii ya 2000 siyo kosa lako kutomfahamu huyu mzee. Sisi tuliozaliwa enzi zile radio ni moja tu na magazeti hayazidi manne (Uhuru, Mzalendo, Mfanyakazi na Kiongozi), huyu mzee si mgeni machoni na masikioni mwetu.
 
RIP Mzee Sozigwa
Binafsi nitakukumbuka sana kwa utaalamu wako wa fasihi uliouonyesha katika vipindi vyako vya Mazungumzo Baada ya Habari. Yale mazungumzo yako ya Nokora Mpumbavu yaliishia kuwa dira yangu ya maisha kuwa popote nilipo huwa siwezi kusahau nilikotoka.
 
RIP mzee wa kusimamia nidhamu. Aliyeitupa taarifa hiyo ni mwenyekiti wa CCM wa wakati huo baada ya kutishwa na vyombo vya intelijensia kuwa mgombea mmojawapo maarufu angehamia upinzani kama jina lake lingeondolewa. Pathetic!!
Huyo ndiye aliyeanza kuiuza CCM kwa watu maarufu na kutokea hapo CCM ilianza kuwa dhaifu na fedha kuanza kutawala siasa zetu.

Vv
 
Tufafanulie alimpigiaje ,simu wakati miaka kulikuwa hakuna simu za mkononi?
Kwani alieleza kwamba alimpigia simu yako Mkononi?
Kulikuwa na simu za mezani ndugu jiongeze au wewe ni kizazi kipya sana huzijui hizo simu
 
Kama mpaka anakufa alikuwa hajalipwa mafao yake basi tutegemee laana kwa hii nchi yetu.

Mzee amepumzika kwa Amani.

Laana humpata kwa aiombaye,MUNGU awaepushe wanao na wana wa wanao juu ya ombi hili la kipuuzi.Kama hajalipwa kwa dhuluma laana si ya Taifa ni kwa wapuuzi waliosababisha,
 
Back
Top Bottom