TANZIA Mzee Paul Sozigwa, aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Mwalimu Julius Nyerere afariki Dunia

Mzee Sozigwa alielewa, aliamini na kutekeleza fikra za Mwalimu. Walipoamua kubadilisha gia ingekuwa vigumu kuendelea naye hivyo akatupwa kama tambaa bovu. Siye wa kwanza kutendewa hayo katika siasa. Historia itatukumbusha vizazi vijavyo.
 
Hawa wazee walikuwa na skills za uongozi na walikuwa imara tatizo lao walikuwa hatengenezi mifumo ya nguvu ili hata wao wakiondoka wanaokuja wasilite mambo yao wafuate mifumo iliyopo.....report yake ya JK ilitupwa coz hakukuwa na mifumo imara ya kiuongozi iliyojengwa....hata sasa tunasifia utendaji kazi wa JPM lkn akitoka hataacha chochote kwa sababu mifumo haijengwi ila ni nguvu ya mtu mmoja.
 
R.I.P mzee Paul Sozigwa tutakukumbuka mzee wetu, haya ndio maisha ya watu wasio na shukrani, tenda wema nenda zako...
Huyu Mzee àlikuwa ni mtu ambaye hakuwahi kuwa mnafiki kwa anacho kiamini! Mara zote alikuwa anasimamia kile anacho kiamini! Kutofautiana mitizamo ni kitu cha kawaida sana katika maisha,mbona hata katika ngazi zetu za kifamilia watoto wanaweza Kutofautiana na Baba au Mama mzazi na maisha yakaendelea! Kuchukiwa kwa mtizamo na fikra binafsi na kumhukumu hii sio haki pia sio sawa haki mbele ya mwenyezi MUNGU! Kanamambo mema huyu Mzee amelifanyia taifa na CCM Jee pia hayo mema waliyasahau? Huyu Mzee familia yake ilikuwa inalalamika muda mrefu kwamba walio na madaraka hawajataka kumsaidia Mzee Sozigwa kimatibabu!anyway sijui sana mambo hayo na ukweli wake pia sio hoja yangu humu jamvini! Ila kama ni kweli?Mzee Sozigwa ameshafariki!jee wao waliomchukia na kumtelekeza kimatibabu kama kweli wapo! Jee wataishi milele??? Hapa uliwenguni sote tunapita tuu tujitahidi sana kuwa wema kwa viumbe vyote vya MWENYEZI MUNGU ili tupate kuwa na mwisho mwema INSHAALAH!
 


That's right, and also walikuwa incompetent and ineffective. Mtu kafanya kazi Ikulu halafu hakuna employment records.

Hivi Ikulu utafanyaje kazi kama vile private caddy boy wa rais bila ajira rasmi ya serikali? Unakuwaje accountable to the rules and laws governing State House staff kama wewe ni some ol' private citizen?

Unapataje security clearance ya kuingia, kushinda na kutoka Ikulu kama sio muajiriwa? Kwa nini hakurasimishwa? Incredibly flatfooted guys.

Msemaji wa Human Resources Ikulu, Bwana Sanga, kasema Sozigwa haonekani kwenye payroll records.

Modern day translation: Mfanyakazi hewa Ikulu.
 
B.mkp enzi hzo alikuwa mzalendo hasa...

R.I.P PAUL

OVA
 
RIP Mzee Sozigwa
Waasisi wa Ujamaa waliosikika sana.
Nakumbuka vipindi vya RTD,kama Mazungumzo baada ya habari,Imeandikwa na Mikingamo.
Wakati Kenya inafunga mpaka wake na Tanzania nayo RTD haikuwa nyuma kuwaita Manyangau.
 

Sahihisho. Wakati huo aliambatana na Rais Mwinyi
 

Rest in peace Mzee wetu
Nilibahatika kukutana nae Ludewa Iringa wakati wa uchaguzi mdogo baada ya kifo cha Haule na kuingia Stanley Kolimba....Kichama taifa mzee ndiye aliyekuwa msimamizi..NI mzee mpole sana mwenye hekima nyingi.
Mimi the mluguru yeye mzalamo.. tulivyokutana huko mbali tukawa ndugu nikawa nampa heshima zake zote.
Alikuja wakati wa kwaresma.. ni RC.. mzee alifunga kiislamu no maji no food hadi 1 usiku... very committed. Familia yangu ilikuwa ikimpikia chakula cha kufuturu.
Baada ya uchaguzi alinitaka niende kukutana nae makao makuu ya chama.. labda leo ningekuwa Bashite namimi.
RIP mzee wangu.. I am glad nilipata kukujua..
 
Kuna mambo ambayo ukiyafikiria kisasa unahisi watu waliishije zamani ila kwa hili Mzee alikua hotelini kulikua na simu landline na kimiti alikua ofisini kuna simu TTCL
Enzi hizo TP&TC.
 
RIP Mzee Sozigwa
Waasisi wa Ujamaa waliosikika sana.
Nakumbuka vipindi vya RTD,kama Mazungumzo baada ya habari,Imeandikwa na Mikingamo.
Wakati Kenya inafunga mpaka wake na Tanzania nayo RTD haikuwa nyuma kuwaita Manyangau.
Paul Sozigwa aliasisi vipi ujamaa?
 
Mbele yake, nyuma yetu.

Poleni sana Wafiwa
 
Tulifahamiana na Binti yake walipokuwa wakiishi kijitonyama! Poleni sana Kina Neema kwa kufiwa na Baba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…