Corona lilikuwa janga ambalo halikutegemewa na hakuna aliyekuwa na uzoefu nalo!Kila mtu alipambana kwa namna yake kutokana na kutojua ugonjwa huu kwa kina!
Wabunge wa upinzani nao wakaona watoke bungeni kwa muda maana gonjwa lilikuwa limebisha hodi huko!Wengine wakabaki na bahati mbaya wawili wakafa!
Kama walivyofanya wapinzani,JPM naye aliikimbia ikulu ya DSM na kwenda Dodoma,hii ilikuwa baada ya gonjaa kutua dar!Virus walipotinga Dodoma,JPM akakimbilia Chato na akajificha huko kwa zaidi ya mwezi!
Kama huyu mzee anasema tusichague wabunge kwa sababu ya kukimbia Corona,basi awaambie wasimchague JPM pia maana na yeye alikimbia ikulu na kwenda kujificha Chato mpaka alipogundua gonjwa sio tishio!