Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 7,748
- 10,288
Kama kawaida yake Mzee Shomari anauza kahawa huku siasa ni mjadala mkubwa kwenye kijiwe chake. Na ndio maana watu wanamkubali maaana yeye anakutana na wanachi moja kwa moja, tofauti na Chadema na ACT wazalendo ambao wanategemea mitandao kueneza uongo na uzandiki.
Mzee Shomari anasema wapinzani wamekuwa kama timu ya mpira wa miguu ambayo imezidiwa kila idara. Wapinzani wanajiuliza wataanza vipi mpira na nani atafunga goli? Hawana mabeki wala kipa na mfunga goli huku mtanange unakaribia.
Mzee Shomari anahoji watakuwa na nini cha kuhoji? Au cha kuzungumza wakati Ccm chini ya JPM imefanya makubwa? Kila sekta imeimarika elimu, miundo mbinu afya n.k. Swali linakuja watakuwa na kikosi gani cha kupambana na CCM chini ya JPM? Mpaka sasa wanahaha ni mgombea gani watamuweka ili awaondelee aibu ya kutosimamisha mgombea.
Ila kama kawaida Mzee Shomari kaninog'oneza bora wamchukue Membe ili wakate nishai. Maana ni aibu kukosa hata mgombea wa kiti cha urais. Japokuwa ni aibu kuchukua galasa toka Ccm.