Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa leo. Waislam wanajua heshima, umuhimu na maana ya mazishi

Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa leo. Waislam wanajua heshima, umuhimu na maana ya mazishi

Slowly

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
10,589
Reaction score
35,268
Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa Leo , hvyo ndo inavyotakiwa , sisi wakristo ni wakengeufu sana , Hata Biblia haihalalishi kuhifadhi maiti mda mrefu , mfano Yesu alifariki akazikwa sku hyo hyo,

View attachment 2585799


Mlolongo wa mazishi kwetu sisi wakristo ni kama ifuatavyo.:

Mtu anafariki , anahifadhiwa mochwari sku nzima, kesho yake anahifadhiwa tena , sku inayofata watu wanajikusanya , sku inayofata anafanyiwa ibada fupi kanisa la nyumbani na anaagwa , sku inayofata anasafrishwa kwenda kwao , sku inayofata anafikishwa kwao, zinapita sku mbili akisubiriwa mwanae kwani yupo ulaya, baada ya hzo sku mbili sku inayofata inafanyika ibada fupi ( syo fupi kama unavyofkri) anaagwa , na kama makaburi yapo karbu basi huzikwa... Na kama yapo mbali husafrishwa na sku inayofuata huzikwaa... Too long

Watu washalia vya kutosha , watu wamesimamisha shughuli zao zaidi ya wiki wanazurura tuu, gharama zimeongezeka mara dufu mana watu wamekusanyika nyumbani kwake na kule anakozikwa pote lazima wahudumiwe, madaftari ya michango ya uongo na kweli kila kona na watu washapita na rambi rambi , mwisho wa sku familia kuachiwa mzigo wamadeni

Tashrifu hakuwa mtu mdogo ila mazishi yake yamezingatiwa kwa uharaka zaid....


Wakristo tuendelee kuchukua notisi
 
Hata nyumbani kwako, hakuna maisha sawa na Kwa jirani yako... Swala hilo ni taratibu tu za watu kwa ajili ya ndugu jamaa na marafiki, na haina jambo lingine lolote kama kama dhambi au kivingine, so wao wanafanya hivyo, na upande mwingine unafanya vile na maisha Kwa wote yanaenda sawa tu
 
Sipingi usemalo isipokuwa kwa Yesu, ni vyema tukitambua huyo mtu inasemekana alipigwa sana hivo alikuwa na wounds kwa wakati ule angeharibika siku hiyo hiyo hata sasa mtu wa aina hiyo ni almost impossible kumtunza

lakini sijasema maiti zizikwe haraka au
 
Dini ni itamaduni wa jamii na kila jamii ina tamaduni zake ambazo ndiyo msingi wa maisha yao ya kila siku. Kamwe taratibu za A haziwezi kuwa za B. Waislamu wabaki kwenye utamaduni wao na wakristo vivyo hivyo. Ni mbaya kuchelewesha maiti kwa mwislamu(ndiyo utamaduni na imani yao) ila siyo mbaya kwa wakristo (ndiyo utamaduni na maisha yao). Tusipangiane wala kulazimishana kila mtu abaki kwenye njia yake
 
Mimi ni muislam lakini katika suala la kuwahisha mazishi niko kinyume na wengi.

Kuzika haraka mtu anapofariki sio muongozo wa quran bali ni maelekezo ya mtume wetu kutokana na wakati wao hakukuwa na teknolojia ya kuhifadhi maiti ili ikae muda mrefu.

Pia kutokana na joto la huko jangwani ikawa ni rahisi maiti kuharibika upesi, lakini pia kutokana na kukosa mawasiliano ya simu wakati huo ikawa sio rahisi kuwapelekea taarifa watu waliopo mbali ili wawahi mazishi, kwa hiyo mtume kwa hekima akasema kati ya mambo yanayotakiwa kufanywa haraka basi mazishi ni mojawapo.

Sasa kwa kuwa nyakati zimebadilika, teknolojia imekua kwa maana maiti inaweza kuhifadhiwa muda mrefu na pia wafiwa pengine wapo mbali na taarifa wamepata kupitia simu au whatsapp, je kuna ubaya gani kuchelewesha mazishi kwa sababu mazishi pia ni ibada mtu akihudhuria anapata thawabu.

Haya ni maoni yangu binafsi kwa sababu kuna Uislam na Uarabu, kun mambo inabidi kuyafuata kama Uislam unavyosema lakini pia kuna masuala ya utamaduni wa kiarabu ambao huku kwetu hauko applicable sio mbaya kama tutaacha huo utamaduni bila kuathiri dhima ya Uislam.
 
Watu mnataka kufanya maisha yawe magumu sana,yaani mfano baba yake mtu amemzaa,amemlea kumsomesha etc akate moto ninyi ndugu msimsubiri huyu mwanae aje ashiriki mazishi yake kwani mliambiwa wamegombana?

Niambie wapi imeandikwa ni dhambi mwili wa marehemu kuhifadhiwa kwa minajili ya kusubiri maziko ya pamoja ndugu wote washiriki.
 
Ni ukengeufu hata biblia haijaainisha hvyo, imeainisha vilevile waislamu wanavyofanya
Biblia ya wapi? Leta andiko
Kwan unakuwa umelazimishwa kuhudhuria msiba?

Hakini dini ya kinafiki kama hiyo unayoisifia

Hawa ndo wanaongoza kwa uzinzi na uasherati na ndio makundi mengi ya kigaid ni wao
Na inayokana na msingi wa imani yao
 
Utaratibu wetu wa mazishi unaongeza NATIONAL INCOME kwa asilimia kubwa sana

UNALALAMIKA BASI TU NI KWA VILE HUJATAKA KUWAZA KIKUBWA ZAIDI.

ngoja nikufafanulie..

1. kulaza mwili mochwari, ni hela kwa serikali
2. kuusafirisha mwili from mochwari to home, ni hela kwa Transporter
3. Kuvalisha mwili mavazi makali na bling bling ni hela kwa wafanyabiashara
4.
5.
6.
Yote kwa yote tulia kwenye imani yako
yakikubana baba hamia huko...
 
Tajiri kama huyo anazikwa chap kwa mambo mengi. Watu washafanya mgao wa Mali vichwani mwao halafu wasubirie nini? ukizinduka? Bore wafukie kama ulikuwa bado utasongesha huko mnene kwa mbele....
 
Back
Top Bottom