Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa leo. Waislam wanajua heshima, umuhimu na maana ya mazishi

Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa leo. Waislam wanajua heshima, umuhimu na maana ya mazishi

Je a sipo zikwa haraka nini hutokea kwa mujibu WA maandiko ya dini?
 
Kuwahi au kutowahi kumzika mtu sio big issue. Kuna jamaa muislam post 10 kaeleza vema sana. Saa zingine mtu kazimia tu we mnawahi kumpiga kituta
.
Kama watu mna uwezo hakuna ubaya kuchelewa kuzika kuwapa nafasi na wengine kushiriki ibada ya mazishi.

Maana kuhudhuria mazishi ni ibada na ukumbusho pia.
Nikikumbukaga Ile ishu ya Fabrice Muamba moyo wake ulivyozima saa 72 angekuwa muislamu angepigwa kituta fasta.

Kuna uwekano mkubwa Kuna waislamu wengi sana wamwzika angali wakiwa hai.
 
Wee unaongea upumbavu Kila kitu kina utaratibu wake pimbi wewe mkristo huo ni utaratibu wa kawaida Kwan ukichelewa kuzikwa na kuwahi Kuna utofauti gan heshima ya mwisho ni ileile tu
 
Hizo zote ni tamaduni, hatutakiwi kugombana kutokana na hizo tamaduni as long as hakuna utaratibu wa mmoja unaomuumiza mwingine. Ukiona unaumia kutokana na utaratibu wa mwingine ujue utakufa mapema maana moyo unasinyaa mda ote
 
Jambo la msingi ni kuwa nakiri mimi ni Muislam na nafuata yale yote niliyoamrishwa, penye kutumia reasoning nitatumia sitapelekeshwa na watu wenye elimu ya kukariri tu.

Kuna mambo mengi tu hayajuwepo wakati wa mtume lakini kwa sasa yanafanyika kwa sababu sio dhambi kuyafanya. Hata hili la kuzika hakuna mahali imelazimishwa kuwa lazima maiti izikwe ndani ya masaa mangapi, Mungu ameacha hilo tulifanye kwa utashi wetu kulingana na mazingira yetu maana yeye ni mjuzi zaidi na ndio maana hakuna dhambi kwa atakayechelewesha maziko.

Zaidi ya hapo asanteni sana mlionitukana kisa tu kutofautiana mtazamo, sio amri yenu ila ni shida ya kukaririshwa bila kufanya tafakuri. Mko radhi kuwanyima weusi wenzenu wenye uhitaji hapo mlipo ili mkatoe hela za utalii huko Saudia muwafurahishe waarab.
 
Usinijazie maswali ili kunitoa nje ya mada tukae hapahapa kwenye lengo la uzi.

Mazishi kufanyika haraka haraka sio sheria kama unavyosema huo ni uzushi unaoleta hapa, lete ushahidi kuwa kuchelewesha kuzika ni dhambi na hukumu yake. Mazishi yalifanyika haraka wakati huko kutokana na hali halisi ya wakati huo, no mortuary, no telephones, no easy access of transportation unadhani wangefanya nini zaidi ya kuzika haraka, nowdays tunaweza kudelay hata siku 2 au tatu kusubiri watu wafike msibani kwa sababu kuna urahisi wa kuhifadhi maiti, usafiri ni wa haraka mfano mtu wa marekani anaweza kufika bongo ndani ya siku moja tu.

Ndio maana hakuna sehemu iliyozuia kuchelewesha kuzika na hata mtume alipofariki hawakumzika harakaharaka hii inaonyesha kuwa sio dhambi kusogeza muda wa kuzika ili kukamilisha baadhi ya mambo.

Kama nyinyi wafia dini mnang'ang'ania kuwa tufuatishe dini bila kufanya reasoning, iweje leo tutumie vipaza sauti badala ya bilal kutumia sauti yake halisi? Kwa nini tunatumia simu hizi wakati hazikuwepo wakati wa mtume? Kwa nini hapa Tanzania now tusitumie usafiri wa farasi kama uliokuwa ukitumika miaka hiyo?
Mwanzo nilikuwa na dhana ya kheri kuwa ni muislam ila nimefatilia mjadala naona kuna ukakasi wa maelezo yako. mdau kasema unagoogle labda huko itafaa kukuweka maana uliposema DINI yako unajisomea mwenyewe hilo tu tayari linakutoa ktk asli ya uislam na hautufundishi hivyo..

-Zipo tamaduni za kiarabu ambazo uislam umezikuta na zinafahamikwa na SHERIA imezibainisha zinaitwaje...?

- Je ktk hizo tamaduni ni pamoja na mazishi yalikuwa na utaratibu huo alotufunza mtume kabla ya uhuishaji wa uislam...?

-Mafundisho yetu ambayo ni QUR'AN na Sunnah ktk uislam tunafahamu zipo Sheria zilizoletwa zinatofautiana baina yetu sisi waumini na mtume wetu je kuhukumu mazishi ya mtume na kukifanya kama ni kielelezo chako itakuwa sahihi....?
 
Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa Leo , hvyo ndo inavyotakiwa , sisi wakristo ni wakengeufu sana , Hata Biblia haihalalishi kuhifadhi maiti mda mrefu , mfano Yesu alifariki akazikwa sku hyo hyo,

View attachment 2585799

Mlolongo wa mazishi kwetu sisi wakristo ni kama ifuatavyo.:

Mtu anafariki , anahifadhiwa mochwari sku nzima, kesho yake anahifadhiwa tena , sku inayofata watu wanajikusanya , sku inayofata anafanyiwa ibada fupi kanisa la nyumbani na anaagwa , sku inayofata anasafrishwa kwenda kwao , sku inayofata anafikishwa kwao, zinapita sku mbili akisubiriwa mwanae kwani yupo ulaya, baada ya hzo sku mbili sku inayofata inafanyika ibada fupi ( syo fupi kama unavyofkri) anaagwa , na kama makaburi yapo karbu basi huzikwa... Na kama yapo mbali husafrishwa na sku inayofuata huzikwaa... Too long

Watu washalia vya kutosha , watu wamesimamisha shughuli zao zaidi ya wiki wanazurura tuu, gharama zimeongezeka mara dufu mana watu wamekusanyika nyumbani kwake na kule anakozikwa pote lazima wahudumiwe, madaftari ya michango ya uongo na kweli kila kona na watu washapita na rambi rambi , mwisho wa sku familia kuachiwa mzigo wamadeni

Tashrifu hakuwa mtu mdogo ila mazishi yake yamezingatiwa kwa uharaka zaid....

Wakristo tuendelee kuchukua notisi
Kinachokuuma Ni Nini au wewe Ni maiti
 
Watu mnataka kufanya maisha yawe magumu sana,yaani mfano baba yake mtu amemzaa,amemlea kumsomesha etc akate moto ninyi ndugu msimsubiri huyu mwanae aje ashiriki mazishi yake?

Niambie wapi imeandikwa ni dhambi mwili wa marehemu kuhifadhiwa kwa minajili ya kusubiri maziko ya pamoja ndugu wote washiriki.
Hata akija anaongeza nn au anapunguza nn?? Mti ameshafariki ni wajibu astiriwe kwa wakati kwsnza tunapunguza mzigo wa machungu kwa wapendwa,kilele cha msiba ni mazishi mtu anapozikwa kuna ahueni flani mfiwa anapata,nikikumbuka kitimtim cha mazishi ya hayati Magufuli,anazungushwa huku mara kule mpaka mwili unapigwa na vumbi kila wanapoenda familia msiba unaanza upya,mpaka ikawa vurugu badala ya mapenzi,mm nasapoti mtu azikwe kwa hataka na kama itabidi kusafirishwa asafirishwe akazikwe,siyo kumsubiri mtu,hata akifika huyo mtu hakuna kitakchoomgezeka!
 
Jambo la msingi ni kuwa nakiri mimi ni Muislam na nafuata yale yote niliyoamrishwa, penye kutumia reasoning nitatumia sitapelekeshwa na watu wenye elimu ya kukariri tu.

Kuna mambo mengi tu hayajuwepo wakati wa mtume lakini kwa sasa yanafanyika kwa sababu sio dhambi kuyafanya. Hata hili la kuzika hakuna mahali imelazimishwa kuwa lazima maiti izikwe ndani ya masaa mangapi, Mungu ameacha hilo tulifanye kwa utashi wetu kulingana na mazingira yetu maana yeye ni mjuzi zaidi na ndio maana hakuna dhambi kwa atakayechelewesha maziko.

Zaidi ya hapo asanteni sana mlionitukana kisa tu kutofautiana mtazamo, sio amri yenu ila ni shida ya kukaririshwa bila kufanya tafakuri. Mko radhi kuwanyima weusi wenzenu wenye uhitaji hapo mlipo ili mkatoe hela za utalii huko Saudia muwafurahishe waarab.
Allah hamfichi dhwaliim hadi hapa umejibainisha wewe ni wa dini gani nilitaraji kufanya mjadala nawe ila sio KIISLAMU maana umejipanga kutukana ALLAH akutoe kwenye ukafiri
 
Jambo la msingi ni kuwa nakiri mimi ni Muislam na nafuata yale yote niliyoamrishwa, penye kutumia reasoning nitatumia sitapelekeshwa na watu wenye elimu ya kukariri tu.

Kuna mambo mengi tu hayajuwepo wakati wa mtume lakini kwa sasa yanafanyika kwa sababu sio dhambi kuyafanya. Hata hili la kuzika hakuna mahali imelazimishwa kuwa lazima maiti izikwe ndani ya masaa mangapi, Mungu ameacha hilo tulifanye kwa utashi wetu kulingana na mazingira yetu maana yeye ni mjuzi zaidi na ndio maana hakuna dhambi kwa atakayechelewesha maziko.

Zaidi ya hapo asanteni sana mlionitukana kisa tu kutofautiana mtazamo, sio amri yenu ila ni shida ya kukaririshwa bila kufanya tafakuri. Mko radhi kuwanyima weusi wenzenu wenye uhitaji hapo mlipo ili mkatoe hela za utalii huko Saudia muwafurahishe waarab.

Umezunguka zunguka weee ila hapo mwishoni umejidhihirisha kuwa kweli wewe sii Muislam.

Kwa taarifa yako Hijja ni nguzo ya dini na wala sio utalii!
 
Mimi ni muislam lakini katika suala la kuwahisha mazishi niko kinyume na wengi.

Kuzika haraka mtu anapofariki sio muongozo wa quran bali ni maelekezo ya mtume wetu kutokana na wakati wao hakukuwa na teknolojia ya kuhifadhi maiti ili ikae muda mrefu.

Pia kutokana na joto la huko jangwani ikawa ni rahisi maiti kuharibika upesi, lakini pia kutokana na kukosa mawasiliano ya simu wakati huo ikawa sio rahisi kuwapelekea taarifa watu waliopo mbali ili wawahi mazishi, kwa hiyo mtume kwa hekima akasema kati ya mambo yanayotakiwa kufanywa haraka basi mazishi ni mojawapo.

Sasa kwa kuwa nyakati zimebadilika, teknolojia imekua kwa maana maiti inaweza kuhifadhiwa muda mrefu na pia wafiwa pengine wapo mbali na taarifa wamepata kupitia simu au whatsapp, je kuna ubaya gani kuchelewesha mazishi kwa sababu mazishi pia ni ibada mtu akihudhuria anapata thawabu.

Haya ni maoni yangu binafsi kwa sababu kuna Uislam na Uarabu, kun mambo inabidi kuyafuata kama Uislam unavyosema lakini pia kuna masuala ya utamaduni wa kiarabu ambao huku kwetu hauko applicable sio mbaya kama tutaacha huo utamaduni bila kuathiri dhima ya Uislam.
Pia ambia hao wasilamu kina SSH na wenzie sa hivi mambo yamebadilika Kuna simu Kuna alarm maswala ya kuweka spika nje zinasumbua ..sisi Christin tukisema tuweke spika nje hapatatosha , tunaweka funga JBL,candy double bass nne zinatengenezwa na wakristo wenzetu pakawa hapatoshi
 
Sehemu na wakati ambapo nawakubali sana Waislamu ni kwenye misiba na ndoa, wana unyama mno
Mnoo, kuna ex wangu tulikuwa tunagombana namblock hata siku mbili siku moja akaniambia sio sawa unachofanya siku mbili ni nyingi je nikifa? mie muislam utakuja kuniunblock ukute na kuzikwa nishazikwa.
 
Hata nyumbani kwako, hakuna maisha sawa na Kwa jirani yako... Swala hilo ni taratibu tu za watu kwa ajili ya ndugu jamaa na marafiki, na haina jambo lingine lolote kama kama dhambi au kivingine, so wao wanafanya hivyo, na upande mwingine unafanya vile na maisha Kwa wote yanaenda sawa tu
Kabisa, ndo maana wao pia mke 4 still ana michepuko na huku mke 1 na michepuko. Kila mtu afanye limfaalo.
 
Back
Top Bottom