Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa leo. Waislam wanajua heshima, umuhimu na maana ya mazishi

Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa leo. Waislam wanajua heshima, umuhimu na maana ya mazishi

Mimi ni muislam lakini katika suala la kuwahisha mazishi niko kinyume na wengi.

Kuzika haraka mtu anapofariki sio muongozo wa quran bali ni maelekezo ya mtume wetu kutokana na wakati wao hakukuwa na teknolojia ya kuhifadhi maiti ili ikae muda mrefu.

Pia kutokana na joto la huko jangwani ikawa ni rahisi maiti kuharibika upesi, lakini pia kutokana na kukosa mawasiliano ya simu wakati huo ikawa sio rahisi kuwapelekea taarifa watu waliopo mbali ili wawahi mazishi, kwa hiyo mtume kwa hekima akasema kati ya mambo yanayotakiwa kufanywa haraka basi mazishi ni mojawapo.

Sasa kwa kuwa nyakati zimebadilika, teknolojia imekua kwa maana maiti inaweza kuhifadhiwa muda mrefu na pia wafiwa pengine wapo mbali na taarifa wamepata kupitia simu au whatsapp, je kuna ubaya gani kuchelewesha mazishi kwa sababu mazishi pia ni ibada mtu akihudhuria anapata thawabu.

Haya ni maoni yangu binafsi kwa sababu kuna Uislam na Uarabu, kun mambo inabidi kuyafuata kama Uislam unavyosema lakini pia kuna masuala ya utamaduni wa kiarabu ambao huku kwetu hauko applicable sio mbaya kama tutaacha huo utamaduni bila kuathiri dhima ya Uislam.
ndugu yangu katika imani nakushauri ukasome dini kwa kufuata misingi ya Quran na sunna kwa ufahamu wa wema waliotangulia.., itakusaidia na utajua kosa lako kwenye haya maelezo..,
 
Asili ya kukimbilia kuzika haraka siku hiyohiyo ulitoka ktk jamii za kimasikini... Kutokana na kushindwa kuhimili malipo ya kuhifadhi maiti wakashauriwa mtu akifa akazikwe haraka.Jamii haikupenda kuzika haraka ndipo dini ikatumika kushawishi kuzika haraka na jamii husika ikatii dini...

Kabla ya hizi dini binadam alikua anahifadhiwa wiki hadi mwezi bila kuzikwa, na hiyo process ya kuhifadhi maiti iliitwa MUMMIFICATION...

... FOR THE RICH AND THE KING ONLY!
 
Uislam hauendeshwi kwa mawazo na busara zako, uislam unaendeshwa kwa kufata Quran na Sunnah

Katika uislam mambo matatu yanatakiwa yafanywe haraka.
1.Mtu anapohitaji kuoa aozeshwe haraka
2.Mtu anapotaka kuslim asilimishwe haraka
3.Mtu anapo fariki azikwe haraka.

Huo ndo uislam kila kitu kimefundishwa katika uislam had staili ya Kutembea, kula&Kunywa, kuvaa, kulala, kuamka, kiiila kitu kimefundishwa na huo ndo unatakiwa uwe mwenendo wa waislam na siyo burasa zako na maoni yako.
Na wewe ukifa utakamuliwa mavi yote kama mzee tashrif uingie peponi msafi?
 
Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa Leo , hvyo ndo inavyotakiwa , sisi wakristo ni wakengeufu sana , Hata Biblia haihalalishi kuhifadhi maiti mda mrefu , mfano Yesu alifariki akazikwa sku hyo hyo,

View attachment 2585799

Mlolongo wa mazishi kwetu sisi wakristo ni kama ifuatavyo.:

Mtu anafariki , anahifadhiwa mochwari sku nzima, kesho yake anahifadhiwa tena , sku inayofata watu wanajikusanya , sku inayofata anafanyiwa ibada fupi kanisa la nyumbani na anaagwa , sku inayofata anasafrishwa kwenda kwao , sku inayofata anafikishwa kwao, zinapita sku mbili akisubiriwa mwanae kwani yupo ulaya, baada ya hzo sku mbili sku inayofata inafanyika ibada fupi ( syo fupi kama unavyofkri) anaagwa , na kama makaburi yapo karbu basi huzikwa... Na kama yapo mbali husafrishwa na sku inayofuata huzikwaa... Too long

Watu washalia vya kutosha , watu wamesimamisha shughuli zao zaidi ya wiki wanazurura tuu, gharama zimeongezeka mara dufu mana watu wamekusanyika nyumbani kwake na kule anakozikwa pote lazima wahudumiwe, madaftari ya michango ya uongo na kweli kila kona na watu washapita na rambi rambi , mwisho wa sku familia kuachiwa mzigo wamadeni

Tashrifu hakuwa mtu mdogo ila mazishi yake yamezingatiwa kwa uharaka zaid....

Wakristo tuendelee kuchukua notisi
My!:adu

Mtakuja zika ambao hawajafa!
Hasa hii Tabia ya kugusa kifua kuona Kama moyo unadunda!
Jirani yangu walimuwahisha bado mwili wamoto Naona Karna fia kaburini[emoji134]
 
Mimi ni muislam lakini katika suala la kuwahisha mazishi niko kinyume na wengi.

Kuzika haraka mtu anapofariki sio muongozo wa quran bali ni maelekezo ya mtume wetu kutokana na wakati wao hakukuwa na teknolojia ya kuhifadhi maiti ili ikae muda mrefu.

Pia kutokana na joto la huko jangwani ikawa ni rahisi maiti kuharibika upesi, lakini pia kutokana na kukosa mawasiliano ya simu wakati huo ikawa sio rahisi kuwapelekea taarifa watu waliopo mbali ili wawahi mazishi, kwa hiyo mtume kwa hekima akasema kati ya mambo yanayotakiwa kufanywa haraka basi mazishi ni mojawapo.

Sasa kwa kuwa nyakati zimebadilika, teknolojia imekua kwa maana maiti inaweza kuhifadhiwa muda mrefu na pia wafiwa pengine wapo mbali na taarifa wamepata kupitia simu au whatsapp, je kuna ubaya gani kuchelewesha mazishi kwa sababu mazishi pia ni ibada mtu akihudhuria anapata thawabu.

Haya ni maoni yangu binafsi kwa sababu kuna Uislam na Uarabu, kun mambo inabidi kuyafuata kama Uislam unavyosema lakini pia kuna masuala ya utamaduni wa kiarabu ambao huku kwetu hauko applicable sio mbaya kama tutaacha huo utamaduni bila kuathiri dhima ya Uislam.
Kasome kwanza dini kijana ndiyo uje na hoja sio hizi hoja za ki uislamu mambo leo/uislamu wa ki liberali (liberal islam) yaani kwamba alichokiongea mtume (hadithi) kisifuatwe kwa sababu zako unazoona wewe ni sawa? Hii dini ni ya Allah( the all knowing) na haiendeshwi kwa hoja za mtu na mtu dini ina misingi yake lazima ifuatwe kama Allah (the all powerful) alivyoweka .

Ingekuwa umesoma angalau quran kidogo ungeelewa kwamba mtum muhammad alikuwa hasemi kwa matamanio yake bali alikuwa anapokea wahyi/ufunuo kutoka kwa yule mwenye nguvu tuangalie hapa surat najm

Quran 53:3-4

{ وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلۡهَوَىٰٓ }
[Surah An-Najm: 3]

3.Wala hatamki kwa matamanio.

{ إِنۡ هُوَ إِلَّا وَحۡيٞ يُوحَىٰ }
[Surah An-Najm: 4]

4. Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa.

Sasa wewe unakuja na uislamu mambo leo unakuja kutaka kubadili mambo yaendane na jinsi akili yako inavyoona nu sawa UTAPOTEA NA KUPOTEZA WENGI.

Kingine Allah (the almighty) anatuambia haya kwenye glorious quran katika surat nisaa aya ya 59

Quran 4:59

{ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَأُوْلِي ٱلۡأَمۡرِ مِنكُمۡۖ فَإِن تَنَٰزَعۡتُمۡ فِي شَيۡءٖ فَرُدُّوهُ إِلَى ٱللَّهِ وَٱلرَّسُولِ إِن كُنتُمۡ تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ ذَٰلِكَ خَيۡرٞ وَأَحۡسَنُ تَأۡوِيلًا }
[Surah An-Nisâ': 59]

Ali Muhsin Al-Barwani:
Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.

Nadhani kumalizia tu Allah ( the merciful one) anatuambia pia katika quran tukufu surat maidah aya ya 49

{ وَأَنِ ٱحۡكُم بَيۡنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَهُمۡ وَٱحۡذَرۡهُمۡ أَن يَفۡتِنُوكَ عَنۢ بَعۡضِ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ إِلَيۡكَۖ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَٱعۡلَمۡ أَنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعۡضِ ذُنُوبِهِمۡۗ وَإِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِ لَفَٰسِقُونَ }
[Surah Al-Mâ'idah: 49]

Ali Muhsin Al-Barwani:
Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu.

N.B
DINI HAIENDESHWI KWA MATAMANIO YETU
 
My!:adu

Mtakuja zika ambao hawajafa!
Hasa hii Tabia ya kugusa kifua kuona Kama moyo unadunda!
Jirani yangu walimuwahisha bado mwili wamoto Naona Karna fia kaburini[emoji134]
Unaweza kuorodhesha majina ya au taja angalau watatu waliowahi kuzikwa kabla ya kufa? Nipo hapa nasubiri
 
Madamu siyo dhambi kuhifadhi mwili kabla ya kuuzika haina shida! La muhimu tu ni kujua kama marehemu alikuwa ametubu dhambi kwa jina la Yesu kabla ya kufa ili aende peponi,(Luka 23:40-43).
Kama alikufa bila kutubu dhambi,hata angezikwa wakati anakata roho haisaidii,maana anakuwa ameenda mahali pabaya motoni,(Luka16:22-31)
 
Unatubu dhambi kwa kiumbe mwenzio yesu,huo ndio ushirikina na ukafiri kimbia haraka
 
My!:adu

Mtakuja zika ambao hawajafa!
Hasa hii Tabia ya kugusa kifua kuona Kama moyo unadunda!
Jirani yangu walimuwahisha bado mwili wamoto Naona Karna fia kaburini[emoji134]
Habari za uongo hizo watu wanajua mtu alie kufa hata alie hai
 
Pointless. Ndo umeongea nini sasa? Huna tofauti na sheikh Kabeke
Hiyo akili ya kujua nimeongea nini unayo? Kama bichwa unatumia kufugia nywele huoni unachoweza kuelewa labda ni kusuka tu? Idiot
 
Wachaga ndo wanakaa na maiti sana.

Hata Bwana Yesu alikufa leo na kuzikwa siku hiyo hiyo
Yesu ilikuwa ni Kwa ajili ya Kuiwahi sabato kwa sababu hawaruhusiwi kufanya kazi siku ya sabato.

Tatizo lenu hata Biblia hamsomi
 
Back
Top Bottom