Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,890
- 26,440
Kuna mwanaJF mmoja hapa amewahi kusema kwamba mzee Uledi ni yule mzee mwenye macho mekundu na ni mwongo sana.
Huyu ni mzee mmojabwapo wa mazee wanounda kamati chini ya mshona viatu ambae hii ni kazi yake ya kujipatia kipato halali kabisa.
Leo mchana huu nimepita pale Tandamti Street na nimempa hizo za JF na mzee akacheka sana.
Kisha nikaamuuliza hizi habari zinazotamba sana kwa sasa huku mitandaoni kuhusu Chato na utendaji wa msemaji wa serikali kuhusu kujibu hoja za mitandaoni.
Akasema" Mitandao ni ya kuiangalia sana yaweza kuwa sumu. Si wafahamu hata mke wa mtu ni sumu ati?
Nikamjibu, sawia.
Mzee Uledi akaendelea;
1. Ukiona baadhi ya viongozi wanajitokeza kujibu hoja za mitandaoni na wakashindwa kufanya hivyo kwa kukosa vigezo na vielelezo.
2. Ukiona watu kama Cyprian Musiba ambae alistaafu kazi ya kujibu hoja mtandaoni kupitia tovuti yake ya YouTube na sasa amerudi tena.
3. Ukiona waziri kama Mwambe anakuja na kutoa kauli za rejareja kuhusu uhaba wa mafuta ya kula nchini wakati nchi hii inalima zao la alizeti kwa wingi.
4. Na mwisho ukiona wizara ya habari kupitia idara yake ya maelezo inaingiliwa na vipindi kama papo kwa papo wakati hiyo ni kazi yake.
Basi ufahamu kuwa Tanzania bado hatujapata watu wenye sifa stahiki za kuwa wasemaji wa serikali.
Sasa mzee Uledi anashauri kwamba nini kifanyike:
1. Masuala yanayomhusu raisi moja kwa moja yanapaswa kujibiwa kwa undani na vielelezo vyote kupitia kurugenzi ya mawasiliano na Ikulu.
Hivi sasa kuna mjadala wenye lengo la kupotosha mitandaoni kuhusu Chato, lakini ukweli unawekwa pembeni kwamba serikali imejenga na inaendelea kujenga hospitali kadhaa za rufaa na imeboresha shule nyingi tu za msingi na serikali hapa nchini.
Kuna hospitali za rufaa zajengwa kule Songwe, Mtwara, Katavi na hospitali za wilaya zote zikiwemo ya Mwananyamala mkoani Dar-es-Salaam zote zinaboreshwa.
Hilo ni eneo mojawapo ya maeneo ambayo serikali inajitahidi kujenga au kuboresha mengine yakiwa mradi wa umeme ambapo vijiji takribani 2500 vinatarajiwa kuwa na umeme kabla ya mwaka 2025.
Miundombinu ingine kama daraja kubwa la Kigongo Busisi katika ziwa Victoria ambalo linatarajiwa kuunganisha nchi za Rwanda, Burundi na Congo DRC ni moja ya miundo mbinu ya kimkakati kuinua uchumi wa sehemu hiyo ya mikoa ya kaskazini magharibi ya Mwanza, Kigoma na Geita na Kagera.
Daraja hili litaokoa watu walokuwa wakifa kila mara kwa kuzama na mitumbwi na pia kuokoa muda wa kuzunguka kupitia njia ya Kamanga.
2. Hoja zingine zinazohitaji ufafanuzi kama ajira, ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi na watumishi wa serikali na zote zahitaji ufafanuzi wa kina na kuelimisha ili kuondoa upotoshaji na uenezi wa chuki unafanywa mitandaoni na wale wapinga maendeleo.
Hivyo mzee Uledi anashauri ama Dr Abbasi kujirekebisha na kuwa anatoa ufafanuzi na kuhakikisha kila chombo cha habari kinatoa ufafanuzi huo na pia kuendesha idara ya habari kimkakati.
Anasema " tuzizoee tu kuangalia wasemaji wa serikali wa nchi zingine na tusiwe tayari kujifunza na kuendana na wakati".
Haya basi, hayo ni maoni ya mzee Uledi na nayaona yana mashiko.
Serikali imekuwa kimya sana na wakti huu ndo yapaswa kuwa "more active" katika kila kijitokezacho kwa minajili ya kupotosha umma.
Kazi na majukumu makubwa ya msemaji wa serikali ni kueneza taarifa (Convey information) kwa umma.
Hivyo kila asubuhi msemaji huyu hujiandaa na taarifa mbalimbali za serikali ili kuzitoa kwa vyombo vya habari Press na wawakilishi (correspondents) wa vyombo vingine vya ndani na nje.
Hii yaitwa "lobby correspondents" na hivyo taarifa zozote mpya au zinazohitaji ufafanuzi huwa ni kazi ya msemaji wa serikali kuzishughulikia.
Hivyo Dkt. Abbasi aamke na asifanye kazi kwa mazoea kungoja vyombo vya habari pengine anavyopendelea yeye vijipeleke ofisini kwake.
Au hata Bwana Msigwa nae apaswa kuwa "more proactive" katika kutoa taarifa au fafanuzi wowote unaohitajika baina ya wananchi na serikali.
Pamoja na kwamba mitandao kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikikaza kamba kufuata sheria na kanuni za mawasiliano, lakini bado serikali inapaswa kuwa makini na kinachoelezwa mtandaoni ili kuweka uwiano wa uelewa baina ya walisha habari na walishwa habari.
Hivi sasa dunia ipo katika sintofahamu kubwa na ugonjwa wa COVID-19 umeshika kasi huku ukiwa unajibadili na kutengeneza virusi wengine ambao wakimwingia mtu basi aweza asionyeshe dalili kabisa za ugonjwa.
Hivyo serikali za nchi maskini au zenye uchumi wa kati kama Tanzania zapaswa kuwa makini na kuwa tayari.