Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Elimu Elimu Elimu.....alijisemea ELNipo Marangu msibani nimemsindikiza best wangu aliyefiwa na shangazi yake na mazishi ni kesho.
Sasa basi asubuhi ya leo tukiwa hapa msibani kuna mtafaruku mkubwa umetokea baada ya mzee mmoja anayetambuliwa kiukoo kama mzee wa ukoo kusema kwamba baada ya huo msiba atakayefuata kufa ni kaka wa marehemu (baba yake na best wangu).
Baada ya kusema hivyo wana familia walimtaka huyo mzee wa ukoo afute hiyo kauli yake maana haiashirii mema kwa familia...
Mzee wa ukoo akagoma kufuta kauli na badala yake akaongeza kwa kusema kuwa ni yeye ndiye aliyemuua shangazi Kwa hiyo anayefuata ni kaka wa marehemu.
Kauli hiyo iliamsha hasira kwa baadhi ya wana familia hadi wakamvaa na kutaka kumpa kichapo mzee wa ukoo ikabidi wenye hekima waingilie kati na kumchukua huyo mzee na kwenda kumfungia ndani ili kumuokoa na kipigo.
Kwa sasa kuna watu wameandaliwa ili kumhoji aeleze kwa undani amemuuaje shangazi na kwa sababu gani atamuua pia kaka yake.
Ni mzozo mkali, kila mtu ndani ya familia kachachamaa na wanamtaka mzee wamshughulikie kikamilifu... Binafsi nimetoa wazo huyo mzee apelekwe polisi na kufunguliwa mashtaka ya kuua & kutishia kuua.
Kiukweli sijui mila za wamarangu zilivyo maana mie ni mmeru tu wa Tengeru na wazo langu halijaungwa mkono kabisa maana wana ukoo wamekazia kulimaliza hilo jambo kiukoo.
Mzee anaendelea kuhojiwa huko chumbani, nitaleta mrejesho baadae ni nini wamekiamua wana ukoo dhidi ya huyo mzee 'aliyeua'.
Fanya kilichokupeleka uko urudi acha umbea mkuu.Nipo Marangu msibani nimemsindikiza best wangu aliyefiwa na shangazi yake na mazishi ni kesho.
Sasa basi asubuhi ya leo tukiwa hapa msibani kuna mtafaruku mkubwa umetokea baada ya mzee mmoja anayetambuliwa kiukoo kama mzee wa ukoo kusema kwamba baada ya huo msiba atakayefuata kufa ni kaka wa marehemu (baba yake na best wangu).
Baada ya kusema hivyo wana familia walimtaka huyo mzee wa ukoo afute hiyo kauli yake maana haiashirii mema kwa familia...
Mzee wa ukoo akagoma kufuta kauli na badala yake akaongeza kwa kusema kuwa ni yeye ndiye aliyemuua shangazi Kwa hiyo anayefuata ni kaka wa marehemu.
Kauli hiyo iliamsha hasira kwa baadhi ya wana familia hadi wakamvaa na kutaka kumpa kichapo mzee wa ukoo ikabidi wenye hekima waingilie kati na kumchukua huyo mzee na kwenda kumfungia ndani ili kumuokoa na kipigo.
Kwa sasa kuna watu wameandaliwa ili kumhoji aeleze kwa undani amemuuaje shangazi na kwa sababu gani atamuua pia kaka yake.
Ni mzozo mkali, kila mtu ndani ya familia kachachamaa na wanamtaka mzee wamshughulikie kikamilifu... Binafsi nimetoa wazo huyo mzee apelekwe polisi na kufunguliwa mashtaka ya kuua & kutishia kuua.
Kiukweli sijui mila za wamarangu zilivyo maana mie ni mmeru tu wa Tengeru na wazo langu halijaungwa mkono kabisa maana wana ukoo wamekazia kulimaliza hilo jambo kiukoo.
Mzee anaendelea kuhojiwa huko chumbani, nitaleta mrejesho baadae ni nini wamekiamua wana ukoo dhidi ya huyo mzee 'aliyeua'.
wanasiasa ndio waliotufikisha hapo. kufuta kauli tunajiuliza: inawezekanaje kurudisha maneno yaliyokwishatoka!Hakuna kitu kinaitwa kufuta kauli kwakuwa maneno ni kama risasi hayana rivasi yakitoka yametoka
Acha unafiki...Maneno yanafutwa kwa maneno! Ndivyo ilivyo!
Halafu ni cheupe mwenye ndevu nyeupeHuyo mzee ndiyo wanadamu waovu
Tukio la kumkunja mzee wa ukoo lilikuwa ghafla sana so sikuwa nimeandaa camera.Hata kapicha tuone jinsi wanavyompiga
Hata ile chai ya Goodluck Gozbert kuchoma gari si uliinywa...
Kwa nini siku hizi imekuwa kawaida kwa watu kuandika kwa kuchapia kama ulivyochapia wewe kwa mwandiko wa chekechea?Kwanini skuhz imekua fashen tujitungia vistor vya ajabu vya uongoo yan mtu aue mtu alafu ajiiseme kua nimeua na niitau. Huo ni uongo wapumbavu ndo watakubali h stor
KilemaMarangu ya wapi
Nitatizo la.batan za sim yangu ila hata hivyo elim yangu ni darasa la saba la kuunga mie nimeishia la nne mkewaangu kaishia la tatu ndo ukijumlisha unapata la sabaKwa nini siku hizi imekuwa kawaida kwa watu kuandika kwa kuchapia kama ulivyochapia wewe kwa mwandiko wa chekechea?
Sio ajabu wala usisingizie keyboard ya simu yako, watu kama wewe msiojua kupangilia herufi mmejaa tele hapa jfNitatizo la.batan za sim yangu ila hata hivyo elim yangu ni darasa la saba la kuunga mie nimeishia la nne mkewaangu kaishia la tatu ndo ukijumlisha unapata la saba
Hunywagi chai wewe?Chai
Marehemu keshazikwa mkuu.Arest in peace aliyefariki, msitirini kwanza marehemu migogoro yenu itafata.
Pitia mrejesho utaelewa chanzo cha mzee wa ukoo 'kuua'Kuna mawili huwenda Kamuua mtu mwenye nguvu ndio maama anajisema,
Au kuna ndugu wa karibu hawakurishika na kifo chake walienda kwa mtaalamu, mtaalamu akawaamvia aliyehusika atajisema
Uchawi upo sio masihara
Ubaya,ubwela!Nipo Marangu msibani nimemsindikiza best wangu aliyefiwa na shangazi yake na mazishi ni kesho.
Sasa basi asubuhi ya leo tukiwa hapa msibani kuna mtafaruku mkubwa umetokea baada ya mzee mmoja anayetambuliwa kiukoo kama mzee wa ukoo kusema kwamba baada ya huo msiba atakayefuata kufa ni kaka wa marehemu (baba yake na best wangu).
Baada ya kusema hivyo wana familia walimtaka huyo mzee wa ukoo afute hiyo kauli yake maana haiashirii mema kwa familia...
Mzee wa ukoo akagoma kufuta kauli na badala yake akaongeza kwa kusema kuwa ni yeye ndiye aliyemuua shangazi Kwa hiyo anayefuata ni kaka wa marehemu.
Kauli hiyo iliamsha hasira kwa baadhi ya wana familia hadi wakamvaa na kutaka kumpa kichapo mzee wa ukoo ikabidi wenye hekima waingilie kati na kumchukua huyo mzee na kwenda kumfungia ndani ili kumuokoa na kipigo.
Kwa sasa kuna watu wameandaliwa ili kumhoji aeleze kwa undani amemuuaje shangazi na kwa sababu gani atamuua pia kaka yake.
Ni mzozo mkali, kila mtu ndani ya familia kachachamaa na wanamtaka mzee wamshughulikie kikamilifu... Binafsi nimetoa wazo huyo mzee apelekwe polisi na kufunguliwa mashtaka ya kuua & kutishia kuua.
Kiukweli sijui mila za wamarangu zilivyo maana mie ni mmeru tu wa Tengeru na wazo langu halijaungwa mkono kabisa maana wana ukoo wamekazia kulimaliza hilo jambo kiukoo.
Mzee anaendelea kuhojiwa huko chumbani, nitaleta mrejesho baadae ni nini wamekiamua wana ukoo dhidi ya huyo mzee 'aliyeua'.
=============
Mrejesho :
Baada ya kuhojiwa mzee wa ukoo amesema yeye ni mtawala wa ukoo na amemuua shangazi kwa sababu Yeye kama mzee wa ukoo hakupenda kumuona shangazi akiwa mwangalizi wa mashamba ya marehemu kaka zake - shangazi alijikabidhi mashamba ya kaka zake watatu baada ya wao kufariki, na alifanya hivyo pasipo kumshirikisha mzee wa ukoo.
Ni muda mrefu umepita mzee wa ukoo alipomtaka shangazi amkabidhi yeye hayo mashamba ili ayaangalie lakini shangazi akamgomea.
Mzee akakazia kwa kusema kuwa shangazi alikosea sana kumgomea mzee wake wa ukoo so mzee akatumia mamlaka yake na kumwondoa kwa njia ya kifo.....
Mzee akaendelea kuweka wazi kuwa atakayefuata kufa ni kaka wa shangazi - huyu ni kaka pekee aliye hai wa marehemu shangazi ambapo atakufa endapo atajipachika usimamizi wa hayo mashamba.
Baada ya mzee kueleza hayo yote waliokuwa wanamhoji ilibidi waahirishe mahojiano ili mazishi yafanyike leo leo badala ya kesho kisha vikao viendelee baada ya mazishi kuhusu hatima ya ubabe wa huyo mzee wa ukoo.
Mazishi yameshafanyika jioni ya leo na kikao kitafanyika baada ya kuanua tanga.
Mimi nitaanza safari ya kuondoka Marangu kesho alfajiri so yatakayojili huko kwa vikao best wangu atanijulisha nikiwa Tengeru maana yeye atahudhuria vikao vyote.