A
Anonymous
Guest
Baba yangu ni Askari Mstaafu mwenye Namba X_C1611 PC, nyaraka zake zinaonesha aliajiriwa Mwaka 1973, alipostaafu Mwaka 1987 kulitokea mkanganyiko wa cheki yake ya malipo.
Cheki ilipelekwa Singida badala ya Kagera, alipokuja kushtuka baadaye akaifuatilia na kubaini hadi muda anafuatilia tayari alikuta cheki imechacha.
Baada ya kufuatilia kwa miaka mingi hatimaye kuanzia Mwaka 2003 akaanda kupata sehemu ya stahiki zake za kulipwa kila mwezi.
Alipofuatilia kuhoji stahiki zake za Kiinua Mgongo na Malipo ya Pensheni ambayo hajapata kati ya Mwaka 1987 alipostaafu hadi Mwaka 2003 hajapata majibu na hakuna Mamlaka yoyote ambayo inatupa majibu kuhusu hilo.
Mwaka 2017, baba alikutana na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro wakati huo, akamuelezea changamoto yake, Sirro akaahidi kulifanyia kazi na kutoa maelekezo ya Maafisa wake washughulikie.
Lakini hilo halikufanyika, hatukuwahi kupata majibu yoyote na pia hata ile cheki ambayo ilipotea njia nayo hatujawahi kuiona mpaka leo.
Kuna Mwaka tulifika hadi kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu kuwaeleza kuhusu mahitaji yetu wakasema kuwa wao wanadili na Watu ambao hawapati stahiki zao mpaka sasa.
Wakati akiwa katika ajira baba alitumia Cheki Namba70227, alipostaafu alifunguliwa jalada Namba TYR Namba 109313.
Aliandaliwa mafao ya kazi yake kwa kutumia Hundi Namba 616026 mnamo Juni 1987 ambayo ni 22654 80 kwa Hundi Namba 418759 na 418760.
Hivyo, nimalizie kwa kutoa wito kwa Mamlaka zinazohusika kutenda haki kwa mzee wetu kwa kuwa umri wake ni Miaka 93 sasa, kwani amelipambania Taifa kwa miaka mingi, inavyoonekana haki yake aliyostahili kuipata Mwaka 1987 hadi Mwaka 2003 inataka kutapeliwa.