Mzee wangu anakaribia kustaafu, uwekezaji upi ni mzuri?

Dhokwa

Member
Joined
Jan 24, 2024
Posts
31
Reaction score
43
Salamu ziwafikie wana Jf wenzangu.
Ninaomba msaada katika uwekezaji wa fedha benki.

Ni hivi mimi nina mzee wangu anayetarajia kustaafu mwaka huu. Sasa kama kijana wake wa pekee na anayeniamini ameniomba nimsaidie namna ya kuwekeza fedha zake kwa ajili ya kufurahia uzee wake.

Sasa mimi cha kwanza kabla ya mengine ninachotamani ni kwamba mzee awekeze fedha zake benki ili ikiwezekana kila mwisho wa mwezi awe kama anapokea mshahara wa kati ya 500,000-700,000 za kitanzania huku ile hela yake aliyohifadhi ikibaki kuwa dhamana yake katika uwekezaji na akiitaka aichukue muda wowote ule.

Nimefatalia kwa umakini sana humu JF uwekezaji wa namna hii mfano, hisa, UTT, fixed account n.k. lakini bado sijapata kile ninachokifikiria kuwa afungue tu akaunti awekeze hela huko kisha kila mwezi awe anavuna kiasi tajwa hapo juu. Sasa maswali yangu ni haya hapa chini.

i. Je Kuna uwezekano wa kupata akaunti ya kuwekeza labda tuseme milioni 20 au 30 za kitanzania na mtu akapata mavuno ya laki 5 Kila mwezi?

ii. Kama ni ndio je ni kiasi gani kinaweza kuleta mavuno ya laki 5 kama jibu ni sio je ni akaunti gani naweza kuwekeza angalau kupata kiasi kizuri kwa mzee kwa kila mwezi?

iii. Je ni benki gani nzuri itafaa Kwa uwekezaji huo kwa ajili ya mzee?

N.B: Kumbuka sitamani uwekezaji mwingine zaidi ya huo hapo juu. naomba ushauri ujikite katika muongozo huo. Natanguliza shukrani zangu.

Soma Ushauri kwa wastaafu na wanaopata hela nyingi kwa mkupuo
 
Duhhhhh..... Hatariz😅🤣😂
 
Yaani unamwambia mtu anastaafu aweke hela yake UTT serious. Mnajua UTT au mnaona mnaandika tu.?
 
Yani milioni 60 upate laki5 kwa mwezi?

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Labda uweke mil.200 ndio unaweza kupata hiyo kiasi Kwa mwezi
 
UTT hii mbeleni naona kuna watu watatoa machozi

Sababu hisa zinaweza shuka...vilevile ongezeko na migogoro duniani na hizi pandemic desease
Kunaweza kuleta mtikisiko wa uchumi kidunia
Kuna watu wameongeza thamani ya mfumo kwa kuingiza pesa ndefu haswa bllion na kitu..

Hawa jamaa siku watatoa na thamani ya kipande itashuka kwa vile speculation upande wa kununua itakuwa chini....Sasa hapa wabongo watajua wamepigwa kumbe hawana uelewa wa soko la hisa ngoja tuone
 
Mkuu si useme tu ni wewe badala ya mzee wako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…