Mzee wangu yupo hoi, huenda Serikali ingeweka wazi, Mzee wangu asingeshiriki kuzika rafiki yao aliyefariki kwa changamoto

Mzee wangu yupo hoi, huenda Serikali ingeweka wazi, Mzee wangu asingeshiriki kuzika rafiki yao aliyefariki kwa changamoto

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Naandika huku naumia sana.

Maisha ya mzee wangu yako hatarini sana anapumua kwa shida sana.

Chanzo cha kuumwa.
Kuna rafiki yao mzee mwenzao alifariki, wakaambiwa kuwa chanzo cha kifo cha huyo rafiki yao ni mapafu.
Kutoka hospital ya Bugando ndugu wa marehemu walipewa mwili kwenda kuzika kijijini geita bila tahadhari wakiamini kafa kwa ugonjwa wa kawaida.

Alipofikishwa huko kijijini, ndipo wazee wenzake wakawa wamejiandaa kumzika mwenzao kama ilivyo ada yao.
Jukumu la kubeba mwili kuzika, lilifanywa na wazee kama ishara ya heshima kwa mwenzao.
Miongoni mwa wazee hao! Na mzee wangu alishiriki.

Msiba ulikuwa na msongamano mkubwa kama ada na mila za vijijini.

Wazee hawa maskini ya Mungu pasipo kujua walibeba mwili bila tahadhari! Hadi atua ya mwisho ya kumzika mwenzao.

Baada ya hapo jioni mzee akanisimulia ilivyokuwa, akadai pia walibeba na jeneza liliwavujia majimaji.
Baada ya siku kadhaa wazee hawa wameanza kuumwa.
Watatu wana hali mbaya sana, na mzee wangu usiku wa kuamkia Leo kabanwa mbavu haswa! Ametumia dawa ya malimao, vitunguu, pilipili na tangawizi lakini hali si hali, kwanza kaanza kuchanganyiwa na haongei tena.
Yuko hospital kalazwa lakini hali ni mbaya sana.
Huenda serikali wangetangaza tahadhari hasa misibani haya yasingetokea.
Huenda serikali ingetangaza wazi misiba ya korona ingezikwa na vijana walivalia kinga.
Hapa najaribu kuwaza kama hali iko hivi, maambukizi yameathiri wangapi kwa uzembe wa serikali?

Hatuhitaji lockdown, lakini chamhimu tamko litoke lifike hata kijijini watu wapewe mbinu.

Imeniuma sana kwa uzembe huu mkubwa! Kama nitapoteza busara za mzee wangu, yamkini na mama yangu atakuwa kaambukizwa maana wanalala pamoja mda wote wa kuuguza.

Yamkini tungeweza kuwalinda wazee lakini watoto wa shule hawa wadogo bado ni Carrier wa kuleta homa hiyo nyumbani.
Serikali ingefunga shule hata kwa miezi miwili ingesaidia kupunguza kasi kama mwaka 2020 sambamba na kuchukua tahadhari.

Utafaa nini utajiri katikati ya misiba?

Serikali ingeweza hata kuja na mikakati, kama hawana pesa za chanjo, wangeipokea hata watu wakachomwa kwa hiari hata kwa malipo tungelipa.

Katiba imuondolee mamlaka mtu mmoja kutegemewa kutoa tamko ili kuliokoa taifa.

Inauma sana.
 
na mzee wangu usiku wa kuamkia Leo kabanwa mbavu haswa!
Pole sana mkuu, naomba kujua mzee wako alianza direct kubanwa na mbavu au alipitia dalili nyingine za awali kama kuumwa kichwa, homa, kuwashwa koo n.k mana nalivomezeshwa ni kua hii kubanwa mbavu hua ni dalili ya mwisho wakati maambukizi yameadvance sana.
asante.
 
Pole ndugu.

Jambo moja ni lazima kifo kiletwe na sababu ambayo kibinadamu tunasema ingeepukika hua tunasema Kwa nini*********?.*

Embu fikiria nchi zenye lockdown bado watu wapukutika tu je hawa wailaumu serikali? Suala jema ni wenyewe kuchukua tahadhar hasa misibani kwa mtu aliyesadikika kuondoshwa na covid, vaa barakoa, sanitizer mfukoni, kuachiana nafasi na sehemu zingine vivyo hivyo.
Tukiendelea kuilaumu serikali tukiendelea kuisubiri serikali tunaoumia ni sisi wenyewe.

Tuchukue tahadhari kulaumu ni kujiumiza ikiwa mlaumiwa hana limuingialo.

MLINZI WA AFYA YAKO NI WEWE MWENYEWE.
 
Mpendwa usingoje mpaka Serikali jikingeni kwenye Familia uko mkumbushane hata kwa njia ya simu kuvaa barakoa ni lazima kunawa mikono ni lazima Mimi nimekuwa nikimkumbusha mama yangu mara kwa mara maumivu yako ya kuondokewa na mpendwa(japosiombei itokee )wako huwezi kugawana na serikali.
 
Halafu goigoi fulani linacomment mahali huko kuwa serekali itoe miongozo ya nini kwani huwezi kujikinga!😬😬😬Imagine hata mtu akifa kwa Corona hospitalini, hakuna kuambiwa kuwa kafa kwa Corona ili mchukue tahadhari achilia mbali kutahadharishwa kuwa kazikeni kwa tahadhari.Tanzania kipindi hiki imepatikana walahi!🚶🚶🚶
 
pole sana mkuu, naomba kujua mzee wako alianza direct kubanwa na mbavu au alipitia dalili nyingine za awali kama kuumwa kichwa, homa, kuwashwa koo n.k mana nalivomezeshwa ni kua hii kubanwa mbavu hua ni dalili ya mwisho wakati maambukizi yameadvance sana.
asante.
Alianza na dalili kama za U.T.I na maralia!
Lakini ghafla ndo mambo ya kubanwa mbavu yameanza usiku
 
Back
Top Bottom