Mzee wangu yupo hoi, huenda Serikali ingeweka wazi, Mzee wangu asingeshiriki kuzika rafiki yao aliyefariki kwa changamoto

HII habari kama si'' kahawa ya asubuhi'' au'' hadithi za shigongo,'' inasikitisha sana!
 
Watu hatuijaji lockdown lakini ile tamko na zile taarifa za hapa na pale za kujilinda zinatosha... Sasaivi hata vyombo vya habar wanaogop kusema kama kuna mdudu... Emu rudisha kumbukumbu zako mwaka jana mwezi wa tatu corona ilivyotangazwa, hadi vijijini ukienda unakutana nje kwenye magenge kuna ndoo ya maji ya kunawa...sasaivi ukimwambia mtu nawa mikono vaa barakoa anakwambia tuliambiwa hamna corona...hii hali unaionaje?
 
Kufa angekufa tu hata kwa kuchomwa na miiba kwa hiyo kama mpango wa Mungu ni kumuua baba yako na atakufa.
Kwahio wale watoto wanaokufa kwa kubakwa na kuuliwa hio ni plan ya Mungu (duh kweli master plan za huyo Mungu wako leaves a lot to be desired)

Kuhusu kufa kila mtu atakufa.., ila hii isiwe sababu watu kujirusha kutoka kwenye magorofa au kulala barabarani eti sababu mwisho wa siku watakufa...., (every minute kwenye hii dunia wewe kama nguvu kazi ni asset kwa jamii inayokuzunguka) unless otherwise wewe ni mchawi hence kuondoka kwako huenda kukawa ni neema...
 
Watu mnapenda propaganda za kijinga sana nchi hii.
Kwahiyo Rais asiposema kuna Corona nyie hamtachukua tahadhari?
Hii nchi imejaa pimbi wengi, kwahiyo unamlaumu Rais kwa uzembe wa baba yako?
Rais kashasema watu wachukue tahadhari na waendelee kumuomba Mungu, nyie mlitakaje ili mchukue tahadhari?
 

Kipimo ni katika msiba wa Maalim. Waombolezaji walikuwa wameonywa hatari ya kuambukizana wao kwa wao au hata tahadhari za kuchuku?

Hawa jamaa wameasababisha vifo vingi.

Pole sana mkuu.

Mwenyezi Mungu na akamfanyie wepesi mzee wako. Apone upesi na aje kusaidia katika vita vya kuokoa wengine.

Hawa wanaotuhami kwa maombi hali mikono yao imejaa damu hawana lolote!
 
Huyo aliyefariki sababu ya corona ,kama serikali ingekuwa makini asingefikishwa hata huko kijijini kuzikwa.Alitakiwa azikwe na serikali.Rejea mazishi ya mtu aliyefariki kwa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu,ebola n.k
 
Ni kujiongeza tu rafiki, mtu akifa kwa tatizo la upumuaji basi nyie ndugu chukueni tahadhari. Pole sana mtoa mada
 
Kufa angekufa tu hata kwa kuchomwa na miiba kwa hiyo kama mpango wa Mungu ni kumuua baba yako na atakufa.
Unaona je tufanye ni mpango wa Mungu ukanunue kamba ujinyonge?

Hii mijamaa:




na chizi nijo ni mzigo sana kwa taifa hili.
 
Ni kujiongeza tu rafiki, mtu akifa kwa tatizo la upumuaji basi nyie ndugu chukueni tahadhari. Pole sana mtoa mada
Mimi nawashauri wazee kijijini kwetu msiba wowote unaotokea mjini, kama ajali haijahusika, wasihudhurie hata kama waliofariki ni watoto wao.Full Stop!
 
Kwahyo hata ile combine iliyokuleta duniani nayo ni mapimbi sio? Je wajomba zako walioko kiparanga ambapo hakuna hata network zaid ya kusikiliza Radio watajuje kuwa korona ipo ili wachukue tahadhari? Sawa Rais kasema tuchukue tahadhari vipi kuhusu kusambaza vipeperushi huko vijijin kuhusiana na tahadhari za mdudu endelea kula ugali kwa shemeji yako ambae ni kada wa mtukuf
 
nchi za wenzetukatiba zao zinaruhusu kuwa shughulikia viongozi wanao toa maagizo ambayo baadae huleta athari kwa jamii mfano ni govana wa new york

 
Yaani nafsi yangu naipenda sana siwezi kusubiri mtu aniambie nichukue tahadhari. Nyumbani kwangu nina sauti inayosikilizwa na watu wanatii . Tunachukua tahadhari kwa kadri ya uwezo wetu . Inabidi kila mtu ailinde nafsi yake. Usiikabidhi nafsi iendeshwe na serikali shauri lako 🤓🤓🤓
 

Hivi huyu serikali asiyelaumiwa wala kuwajibika kwa anaowasimamia ni nani hasa?

Hivi huyu serikali aliapa kuilinda katiba ambayo inamtaka pia kuhakikisha anawahami vilivyo walio nchini yake kwa kuhakikisha ikiwamo na kuwapa taarifa sahihi na kwa wakati kuhusiana na hatari na namna ya kujikinga na majanga yakiwamo magonjwa? Au amesahau?

Enyi:



Huyu serikali kazi yake nini basi? Kuchukua kodi tu?

Tafadhalini angalieni kauli zenu au japo hata mmweleze kungali asubuhi, karibuni anapoteza uhalali wake.

Huu ndiyo ulio ukweri mchungu kweri kweri.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Pole sana. Mungu ni mweza wa yote pamoja na matibabu endeleeni kumuombea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…