Mzee wangu yupo hoi, huenda Serikali ingeweka wazi, Mzee wangu asingeshiriki kuzika rafiki yao aliyefariki kwa changamoto

Mzee wangu yupo hoi, huenda Serikali ingeweka wazi, Mzee wangu asingeshiriki kuzika rafiki yao aliyefariki kwa changamoto

Watu mnapenda propaganda za kijinga sana nchi hii.
Kwahiyo Rais asiposema kuna Corona nyie hamtachukua tahadhari?
Hii nchi imejaa pimbi wengi, kwahiyo unamlaumu Rais kwa uzembe wa baba yako?
Rais kashasema watu wachukue tahadhari na waendelee kumuomba Mungu, nyie mlitakaje ili mchukue tahadhari?
Sikiliza ndugu. Ni vizuri serikali kuanzia shina, mtaa, kata, wilaya, mkoa na taifa wakachukua majukumu yao ya kuonya na kusimamia taratibu za ki afya. Ili wananchi wa wachukuwe tahadhari . Hii ni kwa sababu waTz wamezoea kusimamiwa .

Kosa lilitokea baada kukrash maabara yetu na taratibu za kujikinga na Corona , ikiwemo kuvaa barakoa. InakuwaJe pale kiongozi mkuu anapowabeza viongozi wenzake wanapovaa barakoa ?!
 
Haya ni malipo ya kumdharau Kikwete na kumuita dhaifu, haya sasa Mungu katuletea kichaa lazima tuilipie ili next time tuwe na nidhamu.
Ndugu tusipakane matope, alie sema ni mmoja mtazamo wake kuhusu udhaifu wa Kikwete leo una waunganisha Watanzania wote
 
Watu mnapenda propaganda za kijinga sana nchi hii.
Kwahiyo Rais asiposema kuna Corona nyie hamtachukua tahadhari?
Hii nchi imejaa pimbi wengi, kwahiyo unamlaumu Rais kwa uzembe wa baba yako?
Rais kashasema watu wachukue tahadhari na waendelee kumuomba Mungu, nyie mlitakaje ili mchukue tahadhari?
Ni kweri mkuu. Pimbi kama hawa ni taabu mtupu kwa taifa hili!

IMG_20210218_174254_207.jpg


Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Soma dokezo la huyu Dr. laweza kusaidia
 
Hata wewe unaweza kuwa pimbi pia, Rais kasema tuchukue tahadhari we unatakaje tena?
Vipeperushi? Kwahiyo kama hakuna vipeperushi ndio huwezi kuchukua tahadhari? Pimbi wengi sana hata JF humu
IMG_20210218_174254_207.jpg
 
Wazee wetu wengi sidhani Kama wataelewa wakiambiwa hivyo
Wateelewa si wanaona vifo vya wenzao waliohudhuria misiba ya wagonjwa wa corona?Hili jambo sio siri tena mpaka vijijini!
 
Usiombe yakufike na wewe! Kumuona mpendwa ambaye ni nguzo kuu! Kiunganishi cha ukoo, akiumwa bila matumaini inaumiza sanasana ...moyo unauma , mwili unatetemeka
Rejea nilivyohitimisha!
 
Misiba sahivi siyo ya kuishadadiaaa wazee
Ohooo ukisikia msiba we toa pole tu

Ova
 
Naandika huku naumia sana.

Maisha ya mzee wangu yako hatarini sana anapumua kwa shida sana.

Chanzo cha kuumwa.
Kuna rafiki yao mzee mwenzao alifariki, wakaambiwa kuwa chanzo cha kifo cha huyo rafiki yao ni mapafu.
Kutoka hospital ya Bugando ndugu wa marehemu walipewa mwili kwenda kuzika kijijini geita bila tahadhari wakiamini kafa kwa ugonjwa wa kawaida.

Alipofikishwa huko kijijini, ndipo wazee wenzake wakawa wamejiandaa kumzika mwenzao kama ilivyo ada yao.
Jukumu la kubeba mwili kuzika, lilifanywa na wazee kama ishara ya heshima kwa mwenzao.
Miongoni mwa wazee hao! Na mzee wangu alishiriki.

Msiba ulikuwa na msongamano mkubwa kama ada na mila za vijijini.

Wazee hawa maskini ya Mungu pasipo kujua walibeba mwili bila tahadhari! Hadi atua ya mwisho ya kumzika mwenzao.

Baada ya hapo jioni mzee akanisimulia ilivyokuwa, akadai pia walibeba na jeneza liliwavujia majimaji.
Baada ya siku kadhaa wazee hawa wameanza kuumwa.
Watatu wana hali mbaya sana, na mzee wangu usiku wa kuamkia Leo kabanwa mbavu haswa! Ametumia dawa ya malimao, vitunguu, pilipili na tangawizi lakini hali si hali, kwanza kaanza kuchanganyiwa na haongei tena.
Yuko hospital kalazwa lakini hali ni mbaya sana.
Huenda serikali wangetangaza tahadhari hasa misibani haya yasingetokea.
Huenda serikali ingetangaza wazi misiba ya korona ingezikwa na vijana walivalia kinga.
Hapa najaribu kuwaza kama hali iko hivi, maambukizi yameathiri wangapi kwa uzembe wa serikali?

Hatuhitaji lockdown, lakini chamhimu tamko litoke lifike hata kijijini watu wapewe mbinu.

Imeniuma sana kwa uzembe huu mkubwa! Kama nitapoteza busara za mzee wangu, yamkini na mama yangu atakuwa kaambukizwa maana wanalala pamoja mda wote wa kuuguza.

Yamkini tungeweza kuwalinda wazee lakini watoto wa shule hawa wadogo bado ni Carrier wa kuleta homa hiyo nyumbani.
Serikali ingefunga shule hata kwa miezi miwili ingesaidia kupunguza kasi kama mwaka 2020 sambamba na kuchukua tahadhari.

Utafaa nini utajiri katikati ya misiba?

Serikali ingeweza hata kuja na mikakati, kama hawana pesa za chanjo, wangeipokea hata watu wakachomwa kwa hiari hata kwa malipo tungelipa.

Katiba imuondolee mamlaka mtu mmoja kutegemewa kutoa tamko ili kuliokoa taifa.

Inauma sana.
Hapana! Usikate tamaa huenda mzee wako atapona,siyo kila ugonjwa tunakimbilia kuwaza ni Korona.
 
Back
Top Bottom