Mzee wangu yupo hoi, huenda Serikali ingeweka wazi, Mzee wangu asingeshiriki kuzika rafiki yao aliyefariki kwa changamoto

Pole Sana, chukua tahadhari mapema kabla ya cell Carl haijatanganza
 
WHO walishauri kwamba maiti za Corona zizikwe na watu wa afya na msiba usizidi watu 10.

WHO waliona mbali Sana.

Tatizo Corona imetekwa na siasa uchwara, ujuaji na upotoshaji wa makusudi.
Ushauri mzuri
 
Chukua tahadhari usingoje mpk serikali
Ikuambie nini ufanye

Ova
 
Hili jambo kama halijakukuta unaweza dhani ni Soga tu, ila kama umepitia hata kwenye kutonusa na kupata ladha yoyote utakuwa unamuelewa mtoa uzi. Pole ndugu

Nb. Msagie Karafuu muwe mnamchemshia kama chai.
 
Naandika huku naumia sana.

Maisha ya mzee wangu yako hatarini sana anapumua kwa shida sana.

Chanzo cha kuumwa.
Kuna rafiki yao mzee mwenzao alifariki, wakaambiwa kuwa chanzo cha kifo cha huyo rafiki yao ni mapafu.
Kutoka hospital ya Bugando ndugu wa marehemu walipewa mwili kwenda kuzika kijijini geita bila tahadhari wakiamini kafa kwa ugonjwa wa kawaida.

Alipofikishwa huko kijijini, ndipo wazee wenzake wakawa wamejiandaa kumzika mwenzao kama ilivyo ada yao.
Jukumu la kubeba mwili kuzika, lilifanywa na wazee kama ishara ya heshima kwa mwenzao.
Miongoni mwa wazee hao! Na mzee wangu alishiriki.

Msiba ulikuwa na msongamano mkubwa kama ada na mila za vijijini.

Wazee hawa maskini ya Mungu pasipo kujua walibeba mwili bila tahadhari! Hadi atua ya mwisho ya kumzika mwenzao.

Baada ya hapo jioni mzee akanisimulia ilivyokuwa, akadai pia walibeba na jeneza liliwavujia majimaji.
Baada ya siku kadhaa wazee hawa wameanza kuumwa.
Watatu wana hali mbaya sana, na mzee wangu usiku wa kuamkia Leo kabanwa mbavu haswa! Ametumia dawa ya malimao, vitunguu, pilipili na tangawizi lakini hali si hali, kwanza kaanza kuchanganyiwa na haongei tena.
Yuko hospital kalazwa lakini hali ni mbaya sana.
Huenda serikali wangetangaza tahadhari hasa misibani haya yasingetokea.
Huenda serikali ingetangaza wazi misiba ya korona ingezikwa na vijana walivalia kinga.
Hapa najaribu kuwaza kama hali iko hivi, maambukizi yameathiri wangapi kwa uzembe wa serikali?

Hatuhitaji lockdown, lakini chamhimu tamko litoke lifike hata kijijini watu wapewe mbinu.

Imeniuma sana kwa uzembe huu mkubwa! Kama nitapoteza busara za mzee wangu, yamkini na mama yangu atakuwa kaambukizwa maana wanalala pamoja mda wote wa kuuguza.

Yamkini tungeweza kuwalinda wazee lakini watoto wa shule hawa wadogo bado ni Carrier wa kuleta homa hiyo nyumbani.
Serikali ingefunga shule hata kwa miezi miwili ingesaidia kupunguza kasi kama mwaka 2020 sambamba na kuchukua tahadhari.

Utafaa nini utajiri katikati ya misiba?

Serikali ingeweza hata kuja na mikakati, kama hawana pesa za chanjo, wangeipokea hata watu wakachomwa kwa hiari hata kwa malipo tungelipa.

Katiba imuondolee mamlaka mtu mmoja kutegemewa kutoa tamko ili kuliokoa taifa.

Inauma sana.
Pole sana.Mungu atamponya.
 
Utafaa nini utajiri katikati ya misiba?

Serikali ingeweza hata kuja na mikakati, kama hawana pesa za chanjo, wangeipokea hata watu wakachomwa kwa hiari hata kwa malipo tungelipa.

Katiba imuondolee mamlaka mtu mmoja kutegemewa kutoa tamko ili kuliokoa taifa.

Inauma sana

Pole sana mkuu, katika hatua hiyo tunamuomba Mungu aokoe maisha ya mzee wako.

Katika mambo ambayo yatamfanya huyu "Big boss" asisahaulike milele katika historia ni hili janga la Korona, karibu kila mtu ameguswa kama si ndugu ni jamaa, rafiki, jirani nk, na sisi tuliobaki hai bado ni wahanga wa Corona, tuchukue tahadhari na hapo ndipo Mungu atatusaidia kwa maombi.
 
Leo mzee mbishi kawaambia watu wavae barakoa kujilinda,yaani afya yako mwenyewe mpaka uambiwe na mwanasiasa?...
 
Huko kwenu wazee ndio wanabeba jeneza kupeleka mazikoni, sio vijana! Hao wazee walikuwa wanapokezana jeneza linalowavujia maji vijana wa huko huwa wapi?
Soma mada! Ikumbukwe wazee ndiyo hupanga, waliona fahari kumzika mwenzao kama sehem ya heshima
 
Na hili unailaumu serikari baada ya kumuombea basi kazi.
Pole kwa mzee kuumwa ikawe kheri kwake kua mzima. Amina
 
Kufa angekufa tu hata kwa kuchomwa na miiba kwa hiyo kama mpango wa Mungu ni kumuua baba yako na atakufa.

Sio mpango wa Mungu mtu anapokufa.

𝑬𝒛𝒆𝒌𝒊𝒆𝒍𝒊 18:32 - 𝑴𝒂𝒂𝒏𝒂 𝒎𝒊𝒎𝒊 𝒔𝒊𝒌𝒖𝒇𝒖𝒓𝒂𝒉𝒊𝒊 𝒌𝒖𝒇𝒂 𝒌𝒘𝒂𝒌𝒆 𝒂𝒇𝒂𝒚𝒆, 𝒂𝒔𝒆𝒎𝒂 𝑩𝒘𝒂𝒏𝒂 𝑴𝑼𝑵𝑮𝑼; 𝒃𝒂𝒔𝒊 𝒈𝒉𝒂𝒊𝒓𝒊𝒏𝒊, 𝒎𝒌𝒂𝒊𝒔𝒉𝒊.

Usiwe mpumbavu unaweza kufa kwa ujinga.
𝑴𝒉𝒖𝒃𝒊𝒓𝒊 7:17𝒃 .....𝑾𝒂𝒍𝒂 𝒖𝒔𝒊𝒘𝒆 𝑴𝑷𝑼𝑴𝑩𝑨𝑽𝑼; 𝑲𝒘𝒂𝒏𝒊 𝒖𝒇𝒆 𝒌𝒂𝒃𝒍𝒂 𝒚𝒂 𝒘𝒂𝒌𝒂𝒕𝒊 𝒘𝒂𝒌𝒐?
 
Naandika huku naumia sana.

Maisha ya mzee wangu yako hatarini sana anapumua kwa shida sana.

Chanzo cha kuumwa.
Kuna rafiki yao mzee mwenzao alifariki, wakaambiwa kuwa chanzo cha kifo cha huyo rafiki yao ni mapafu.
Kutoka hospital ya Bugando ndugu wa marehemu walipewa mwili kwenda kuzika kijijini geita bila tahadhari wakiamini kafa kwa ugonjwa wa kawaida.

Alipofikishwa huko kijijini, ndipo wazee wenzake wakawa wamejiandaa kumzika mwenzao kama ilivyo ada yao.
Jukumu la kubeba mwili kuzika, lilifanywa na wazee kama ishara ya heshima kwa mwenzao.
Miongoni mwa wazee hao! Na mzee wangu alishiriki.

Msiba ulikuwa na msongamano mkubwa kama ada na mila za vijijini.

Wazee hawa maskini ya Mungu pasipo kujua walibeba mwili bila tahadhari! Hadi atua ya mwisho ya kumzika mwenzao.

Baada ya hapo jioni mzee akanisimulia ilivyokuwa, akadai pia walibeba na jeneza liliwavujia majimaji.
Baada ya siku kadhaa wazee hawa wameanza kuumwa.
Watatu wana hali mbaya sana, na mzee wangu usiku wa kuamkia Leo kabanwa mbavu haswa! Ametumia dawa ya malimao, vitunguu, pilipili na tangawizi lakini hali si hali, kwanza kaanza kuchanganyiwa na haongei tena.
Yuko hospital kalazwa lakini hali ni mbaya sana.
Huenda serikali wangetangaza tahadhari hasa misibani haya yasingetokea.
Huenda serikali ingetangaza wazi misiba ya korona ingezikwa na vijana walivalia kinga.
Hapa najaribu kuwaza kama hali iko hivi, maambukizi yameathiri wangapi kwa uzembe wa serikali?

Hatuhitaji lockdown, lakini chamhimu tamko litoke lifike hata kijijini watu wapewe mbinu.

Imeniuma sana kwa uzembe huu mkubwa! Kama nitapoteza busara za mzee wangu, yamkini na mama yangu atakuwa kaambukizwa maana wanalala pamoja mda wote wa kuuguza.

Yamkini tungeweza kuwalinda wazee lakini watoto wa shule hawa wadogo bado ni Carrier wa kuleta homa hiyo nyumbani.
Serikali ingefunga shule hata kwa miezi miwili ingesaidia kupunguza kasi kama mwaka 2020 sambamba na kuchukua tahadhari.

Utafaa nini utajiri katikati ya misiba?

Serikali ingeweza hata kuja na mikakati, kama hawana pesa za chanjo, wangeipokea hata watu wakachomwa kwa hiari hata kwa malipo tungelipa.

Katiba imuondolee mamlaka mtu mmoja kutegemewa kutoa tamko ili kuliokoa taifa.

Inauma sana.
Naona umeamua kujifunza kutengeneza hadithi za kufikirika.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Acha ujinga yaanisisitunakufa kwasababu yamtu mmoja heriwangeluhusu chanjo waowasipewe watumie mitishamba inauma sana
 
Back
Top Bottom