Mzee Warioba akieleza jinsi Zanzibar walivyopora mamlaka ya raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na kujitoa kwenye muungano kinyemela!

Mzee Warioba akieleza jinsi Zanzibar walivyopora mamlaka ya raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na kujitoa kwenye muungano kinyemela!

Mimi nitaendelea na msimamo wangu, kwamba mazingira ya muungano yaliyopo sasa ni muungano jina. Zanzibar wameshajitoa kwenye huu muungano kinyemela, na Tanzania bara inaendelea kuwahudumia na kuwafanya kama taifa kupe kwenye huu muungano. Ndio maana nasema wazi, katika mazingira kama haya yaliyopo, raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hapaswi kabisa kutoka Zanzibar, wala kuwa na watumishi wengi kama ilivyo sasa katika serikali ya muungano kama mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi wizarani, wakurugenzi Tamisemi nk. Kwa vitu walivyofanya Zanzibar katika kuuhujumu muungano ni lazima raisi wa Tanzania atoke Tanzania bara. Mbadala wa hili ni kuwa na serikali tatu, lazima kuwe na serikali ya Tanganyika. Hili halipaswi kuwa na mjadala tena.

Hatuna tatizo na raisi Samia, amefanya mengi mazuri kwa nia nzuri, japo kuna makosa mengi pia. Lakini katika mazingira ya muungano yaliyopo haifai tena yeye kuendelea kuwa raisi wa Tanzania. Kwa kuwa katiba inamruhusu kugombea, jambo la busara ni yeye kujitoa kugombea uraisi wa 2025 ili kutoa nafasi kwa mtu wa Tanzania bara kuwa raisi wa Tanzania. La sivyo itabaki kuwa jukumu la kila Mtanzania bara kuhakikisha uchaguzi wa 2025 unatoa raisi kutoka Tanzania bara, bila kujali yuko chama gani cha siasa.

View attachment 3124746
Kuendelea kukubali hali kama hii kwenye mikutano ya kimataifa ni matusi kwa Watanganyika
 
huu muungano unaonekana ulishakufa kitambo
ila unalazimishwa tu
eti Tanzania bara nyingine Zanzibar,inasikitisha sana
 
Na Jeshi JWTZ walipeleke Zanzibar kisha watangaze muungano umevunjika😀

Ni hivi kamanda, Zanzibar hawawezi kutangaza rasmi bila makubaliano na bara kwamba muungano umevunjika, ndio maana wanauvunja kinyemela na kimyakimya. Wakitangaza rasmi itakuwa uhaini, na itabidi JWTZ waende Zanzibar kuvunja uasi.

Ila sasa, JWTZ hawawezi kuwa deployed kuingia Zanzibar bila amri ya raisi wa Tanzania. Hivyo kama Zanzibar wanataka kutangaza kujitenga ni sasa wakati Tanzania ina raisi wa Zanzibar. Hata hivyo, sidhani kama raisi Samia atazuia jeshi kuingilia kati, kwa sababu Zanzibar wakitangaza kujitenga na yeye akakaa kimya basi itabidi na yeye aondolewe. Kumbuka Samia ni raisi kwa sababu JWTZ walikubali awe raisi. Sehemu moja ambayo raisi Samia anajua hataweza kuiweka kabisa kwapani ni JWTZ. Hili litabaki predominantly la Watanzania bara, hata akiwaambia vijana wote wa Zanzibar wajiunge na JWTZ. Taasisi moja iliyomweka sawa Mwinyi wakati ule ilikuwa JWTZ, wakati wa Generali Mwita Kiaro, na Samia anajua hilo. Kwanza wanajeshi wa Zanzibar maserule sana.
Watakacho kiganya kamwe hakitakuwa uasi, sababu kwa ni jambo la kikatiba. Katiba ambayo wamekuwa wakiitumia kwa miaka kadhaa.
Ikumbukwe, kupitia Katiba hiyo Zanzibar tayari imetangaza mipska yake na ninyi mpi kimya, zanzibar imemuondolea mamlaka rais wa Jamhuri wa Muungano na mpo kimya, Jeshi linamtii rais wa Zanzibar mbele ya Rais wa Muungano. Linampigia mizinga 21 mbele ya rais wa Muungano na ninyi mnaona na mpo kimya.

Zanzibar chini ya Mwinyi ni kama haina kuaminiana, ni kama haijashikana hivyo wanasubiri Mwinyi amalize muda wake waanze kufanya yao.

Tena ili kujihami wala huenda kwanza wakajitoa kwenye Muungano, halafu next move huenda hata wasitangaze kuanzisha nchi badala yake wakaomba na kutangaza kujiunga na Oman
 

Muungano wenywe ni fake tangu mwanzo leo ndio Mzee Warioba unaona?​

Fake kabsaa ,ebu fikiria Mzanzibar anaweza kua mkuu wa wilaya bara ila kamwe mtu wa bara hawez kua kiongoz Zanzibar, Mzanzibar ruksa kununua shamba na kujenga bara ila marufuku mtu wa bara kununua sehem Zanzibar, ni marufuku mtanzania kua Rais Zanzibar ila ruksa Mzanzibar kua Rais bara,,, yaan Kwa kwel tunatakiwa kueleweshwa ,,tujueni katiba ipi inayo prevail kati ya katiba ya Zanzibar na ya jamhuri pale zinapokinzana!!!
 
Katika thread, hasa hii hapa
Inahitaji akili kubwa kiasi gani kuelewa kwamba kwa kuwa Zanzibar wana serikali na Rais wao, Rais wa Tanzania, kimsingi, ni Rais wa bara?
nimeeleza wazi kwamba sio kosa kikatiba kwa raisi Samia kugombea uraisi 2025. Ana haki ya kikatiba kufanya hivyo, lakini itakuwa jambo la busara, kutokana na mazingira yaliyopo, kwa raisi Samia kujitoa kwenye mbio za uraisi 2025, na kisha tutafanya mabadiliko ya Katiba ili kuanzia sasa suala la raisi wa Tanzania libaki kuwa la mtu toka Tanzania bara, isipokuwa kama tutakubali muungano wa serikali tatu.
Tunaweza kumkataa mama ukashangaa limekuja jitu kama "baba Isack" ndo mtahama hii nchi
 
Mtu na nduguye, wakishirikiana na vibaraka wa Tanganyika akina Mwegulu, Majiliwa et al, wameamua kuitumia Tanganyika, kuijenga Zanzibar.

Fikiria watu 0.5% ya population ya Tanzania wanagawiwa 19% ya mikopo na misaada yote, lakini wa kulipa madeni ni Tanganyika! Wazanzibari walikuwa wanapata 4% ambayo bado ilikuwa ni kubwa mno kwa kuzingatia idadi ya watu na ukubwa wa Zanzibar. Cha ajabu, wanayemwita mama, kaongeza mpaka 19%!!, na matanganyika vibaraka na machawa, yanashangilia.
Akina Mwigulu wao kazi kubwa ni kuiba maswala ya nchi baadae hayawahusu
 
Muungan
Hilo sio suala muhimu. Jambo la msingi ni kwamba hizi statements za Warioba ni facts? Kwani hiyo picha hapo juu ya mkutano wa kimataifa na wawakilishi wa Zanzibar na Tanzania ni ya lini Mkuu?
Muungano ni moja ya Tunu ya Taifa letu,lakini hizi kasoro za Muungano zinarekenishika,tuwe na Serikali 3 .ya Tanganyika,Ya Muungano na ya mapinduzi ya Zanzibar,Tayari katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ina kinzana na katiba ya Zanzibar kwa marekebisho yalifanyika mwaka 2010,Katiba ya Tanzania inatambua kwamba Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wakati katiba ya Zanzibar inasema Zanzibar ni NCHI mojawapo inayounda Jamhuri ya Muungano,hivyo Wanzibari wameipa nchi Yao hadhi ya kuwa Nchi..Kwa Sasa Nchi yetu ina amiri Jeshi wakuu 2 ambao Jeshi linakula kiapo Cha utiii kwao..Kitu ambacho ni hatari kwa Ulinzi na Usalama.
 

Muungano wenywe ni fake tangu mwanzo leo ndio Mzee Warioba unaona?​

Huo mbona ni msimamo wake tangia watoe katiba pendekezwa, sema wachache wanaofaidika na mfumo huu, kutumia dola walikuwa wanampiga vibao akitaka kuongea, na wamezima maoni ya tume yake
 
Sio kila kitu kinachowekwa kwenye Katiba ni halali au kinafaa, ndio maana katiba hubadilishwa kila wakati.
sasa vibadilishwe. Vinavyowekwa ni halali ndio mana viliwekwa, sema vinakosa uhalali jinsi majira yanavyobadilika. Sasa majira ni tofauti na enzi za uhiru. Kayiba haina budi ibadilishwe
 
Swala la Watanganyika kuingia Zanzibar kwa masharti linaniacha hoi. Marehemu Mtikila alieleza ukweli.
 
Back
Top Bottom