Mzee Warioba akieleza jinsi Zanzibar walivyopora mamlaka ya raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na kujitoa kwenye muungano kinyemela!

Mzee Warioba akieleza jinsi Zanzibar walivyopora mamlaka ya raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na kujitoa kwenye muungano kinyemela!

La sivyo itabaki kuwa jukumu la kila Mtanzania bara kuhakikisha uchaguzi wa 2025 unatoa raisi kutoka Tanzania bara, bila kujali yuko chama gani cha siasa.
Naamini suluhisho lingepatikana hapo kupitia sanduku la kura, ila tatizo ni kuwa mchakato mzima wa uchaguzi (kupiga kura, kuhesabu kura na kutangaza mshindi) unasimamiwa na kudhibitiwa na watu wasio na uzalendo, yaani wezi na wanyang'anyi
 
Hao wezi na wanyang'anyi ni Watanganyika wanaofanya hivyo kwa ajili ya CCM. Labda sasa ni kuwaelimisha wafanye hivyo kwa ajili y Tanganyika
 
Awamu hii kuna mazingira wezeshi ya kuvunja muungano kama ifuatavyo:
1. Zanzibar wamevunja katiba na hakuna kiongozi wa kuwakemea.
2. Rais wa Tanganyika (ssh) yamemzidi nguvu kuyakabili ukizingatia kule Zanzibar dini hairuhusu mwanamke kuongoza wanaume.
 
Mnafiki huyo mzee,jumbe walimvua urais kiujanja ujanja,wakamfunga kifungo Cha nje kigamboni
Kiujanja gani wakati alilotaka kufanya lilijulikana? Yeye alifikiri kuvunja muungano ni suala la yeye kutangaza tu kuwa muungano umevunjika kuanzia sasa Zanzibar imejiunga rasmi na Oman sijui. Kina Seifu wakamripoti. Tena Nyerere alimhurumia akamwacha aishi Kigamboni, maana Zanzibar walimkataa kabisa hawakutaka hata kumwona
 
Awamu hii kuna mazingira wezeshi ya kuvunja muungano kama ifuatavyo:
1. Zanzibar wamevunja katiba na hakuna kiongozi wa kuwakemea.
2. Rais wa Tanganyika (ssh) yamemzidi nguvu kuyakabili ukizingatia kule Zanzibar dini hairuhusu mwanamke kuongoza wanaume.
Hiyo ipo kwenye katiba ya zanzibar ? au ni kihisia ? Vp kuhusu ma RC na ma DC nao hawaruhusu kuongozwa na kina mama wilayani au mkoani
 
Kiujanja gani wakati alilotaka kufanya lilijulikana? Yeye alifikiri kuvunja muungano ni suala la yeye kutangaza tu kuwa muungano umevunjika kuanzia sasa Zanzibar imejiunga rasmi na Oman sijui. Kina Seifu wakamripoti. Tena Nyerere alimhurumia akamwacha aishi Kigamboni, maana Zanzibar walimkataa kabisa hawakutaka hata kumwona
Acha kuparamia mambo,jumbe alitangaza kujiunga na Oman lini?..na kujiunga vipi!?..umelishwa propaganda umevimbiwa
 
Yaani Tanganyika yenye watu zaidi ya milioni 60 inatawaliwa na Wazanzibar yenye watu chini ya milioni 3!

NANI AMETULOGA SISI WATANGANYIKA?

God Bless Tanganyika
Miaka ya 60, Tanganyika ilikua na watu zaidi ya milioni 10, ilikua ikitawaliwa na watu wa Butiama, walikuwa hawafiki hata 10,000. Hapo vipi?
 
Kutotumia busara na hekima hapa maana yake itumike nguvu, aidha ya wananchi mitaani kama ilivyokuwa Misri, Tunisia nk, au mapinduzi ya kijeshi, kama Burkina Faso au Niger. Sasa ndicho tunachotaka kweli?
Mngeonyesha mfano Septemba 21, 2024 ningekuoneni kweli mlidhamiria.
Lakini huku kwenye ukiibod worrior ,aaah.
 
Muungano wenywe ni fake tangu mwanzo leo ndio Mzee Warioba unaona?​

Kwani ni mara ya kwanza mzee Warioba kulielezea hili? Bhasi wewe utakuwa mgeni katika medani za siasa nchi hii hasa tangia vuguvugu la katiba mpya lilipoanza mpaka kufikia rasimu ya Judge Warioba.
Umesema ni muungano fake tangia mwanzo, wewe ulishachukua hatua gani?
 
Ni kosa la kikatiba, ambapo hatukutarajia raisi kutoka Tanzania bara anaweza kufa akiwa madarakani na makamu wa raisi toka Zanzibar akawa raisi wa Tanzania, katika mazingira ambayo raisi wa Tanzania ni raisi wa Tanzania bara (Tanganyika)
🙋‍♂️✍️🎯👌👊👍👏🤝🙏
 
Mimi nitaendelea na msimamo wangu, kwamba mazingira ya muungano yaliyopo sasa ni muungano jina. Zanzibar wameshajitoa kwenye huu muungano kinyemela, na Tanzania bara inaendelea kuwahudumia na kuwafanya kama taifa kupe kwenye huu muungano. Ndio maana nasema wazi, katika mazingira kama haya yaliyopo, raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hapaswi kabisa kutoka Zanzibar, wala kuwa na watumishi wengi kama ilivyo sasa katika serikali ya muungano kama mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi wizarani, wakurugenzi Tamisemi nk. Kwa vitu walivyofanya Zanzibar katika kuuhujumu muungano ni lazima raisi wa Tanzania atoke Tanzania bara. Mbadala wa hili ni kuwa na serikali tatu, lazima kuwe na serikali ya Tanganyika. Hili halipaswi kuwa na mjadala tena.

Hatuna tatizo na raisi Samia, amefanya mengi mazuri kwa nia nzuri, japo kuna makosa mengi pia. Lakini katika mazingira ya muungano yaliyopo haifai tena yeye kuendelea kuwa raisi wa Tanzania. Kwa kuwa katiba inamruhusu kugombea, jambo la busara ni yeye kujitoa kugombea uraisi wa 2025 ili kutoa nafasi kwa mtu wa Tanzania bara kuwa raisi wa Tanzania. La sivyo itabaki kuwa jukumu la kila Mtanzania bara kuhakikisha uchaguzi wa 2025 unatoa raisi kutoka Tanzania bara, bila kujali yuko chama gani cha siasa.

View attachment 3124746
Kuendelea kukubali hali kama hii kwenye mikutano ya kimataifa ni matusi kwa Watanganyika
JPM ASINGEKUBALI HUU UJINGA
 
JPM ASINGEKUBALI HUU UJINGA
Acha utetezi wa kijinga!
  • Kwani wakati wa JPM, Katiba ya Zanzibar haikuwepo?
  • Kwani wakati wa JPM, Zanzibar haikuwa na Rais wake?
  • Kwani wakati wa JPM, Zanzibar haikuwa na bendera yake?
  • Kwani wakati wa JPM, Zanzibar haikuwa na wimbo wake wa Taifa?
  • Kwani wakati wa JPM, Waziri Mkuu alikuwa na uwezo gani Zanzibar?
  • Kwani wakati wa JPM, Katiba ya Jamhuri ilikuwa na nguvu gani Zanzibar?

french, acheni utoto. CCM kubaki madarakani inahitaji kumiliki vitu kadhaa
  1. Serikali ya Tanzania
  2. Serikali ya Zanzibar
  3. Vyombo vyote vya kutunga sheria Tanzania na Zanzibar
  4. Vyombo vyote vya kusimamia sheria Tanzania na Zanzibar
  5. Vyombo vyote vya kutoa haki Tanzania na Zanzibar
  6. Vyombo vyote vya ulinzi na Usalama Tanzania na Zanzibar
  7. Vyombo vyote vya habari Tanzania na Zanzibar.
Na mwisho, CCM inahitaji idadi kubwa ya wananchi masikini wenye uelewa mdogo!
 
Back
Top Bottom