Mzee Wasira amjulia hali Gachuma katika hospitali ya Bugando

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amemjulia hali Mjumbe wa Halmashauri Kuu yaTaifa (NEC), Ndugu Christopher Gachuma ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Bugando jijini Mwanza.

Ndugu Gachuma amelazwa hospitalini hapo baada ya kupata ajali ya gari jana katika Kijiji cha Gesarya, Kata ya Lung’abure, wilayani Serengeti Mkoa wa Mara alipokuwa akielekea katika Ziara ya Makamu Mwenyekiti Wasira

Majeruhi mwengine katika ajali hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Ndugu Kemilembe Ruta pamoja na dereva wa gari hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya hospitali hiyo, majeruhi wote wa ajali hiyo wanaendelea vizuri.

Ndg Wasira amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ambapo kesho atahutubia mkutano mkubwa utakaofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.

 
Hii nyara ya hifadhi ya Gombe mbona inarandaranda uraiani?
 
Thamani ya mtanzanzia asiye na cheo/madaraka haipo.

Sijaona hata dereva akitajwa, ukute hana miguu
 
Madereva wa mawilayani na mikiki ya misafara ya wakubwa, usijekuta incompetence kwa upande wa dereva ndicho chanzo cha ajali.

Hata hivyo yeye na mkuu wa wilaya wametajwa kama miongoni mwa majeruhi.
Sorry mkuu, mimi ndiye sikusoma kwa utulivu. Mniwie radhi
 
Gachuma na Gachagua wa Kenya ni ndugu moja? 😲
 
Mkome
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…